Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Kusimamia familia ndogo ya duma kunaweza kuonekana kuwa ni jambo jepesi na rahisi kwa mama duma, lakini kila siku ni changamoto ya kimyakimya yenye kuhitajiuvumilivu sana. Alfajiri, anaamka, akifahamu kuwa hatma ya watoto wake ipo mikononi mwake.
Watoto wake, wakiwa bado wamejaa nguvu, wanaruka-ruka kumzunguka, wakicheza bila kufahamu kuwa kuna hatari kubwa juu yao. Anawaruhusu wacheze, akijua kwamba michezo hii ni mafunzo muhimu kwa maisha yao ya baadaye. Lakini anakaa macho: kwani simba au fisi anaweza kutokea wakati wowote.
Jua linapofikia kilele chake, ndipo yeye huanza kuwinda. Watoto hujificha kwenye kichaka kinene, mioyo ikidunda kwa msisimko wakisubiria chakula.
Baada ya kukimbizana kwa kasi ya umeme, anarudi, akihema lakini akiwa mshindi, akiwa na tunzo ya swala ili kulisha watoto wake wenye njaa. Usiku unapoingia, familia hiyo ndogo hutembea pamoja, watoto hao wakiwa kwenye tumbo lenye joto la mama yao.
Mama duma anabaki macho, na kwa uangalifu sana hata akiwa na uchovu, macho yake yamefumba nusu lakini silika yake ni huwa macho. Kwa sababu kwake, kulinda watoto wake sio jukumu - ni sababu yake ya kuishi.