Fahamu Mambo 10 Kuhusu El Chapo (The Drug LORD)

Fahamu Mambo 10 Kuhusu El Chapo (The Drug LORD)

Fukara

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2013
Posts
1,625
Reaction score
928
Joaquin Guzman Loera a.k.a El Chapo mzaliwa wa mexico na mfanyabiashara mkubwa wa madawa ya kulevya anayetafutwa na Marekani na Mexico kwa udi na uvumba, leo nimeamua kushare na nyinyi wanaJF kuhusu mafia huyu wakimekiko.

1.Forbes walishawahi kumuweka kwenye listi ya watu wenye pesa nyingi duniani mwaka 2009.

2.Ni miongoni mwa watu wenye nguvu na ushawishi duniani akikamata nafasi ya 67.

3.Alipewa jina la Osama bin Laden wa biashara ya madawa.

4.Ametoka kwenyw familia masikini na amesoma mpaka darasa la 3,akaanza kuuza bangi na baba yake mzazi akiwa na umri wa miaka 15 akamjenga nyumba mama yake.

5.Amekaa gerezani kuanznia mwaka 1983 mpaka 2001 chini ya ulinzi mkali wa wanajeshi na usalama,lakini alitoroka baada ya kuonga dola 2.5m,alipitia kwenye toroli la kukusanyia nguo chafu gerezani.

6.Selo yake ilikuwa tofauti na zingine alipata kila kitu alichokuwa anataka zikiwemo cocaine na malaya na alibadili selo kuwa kama hoteli yenye hadhivya nyota tano.

7.Alipewa jina la "public enemy No 1"nchini marekani na harususiwi kukanyaga nchini humo.

8.Anawake wa 4 na watoto 10 lakini wote wanafanya biashara hiyo ya madawa ya kulevya.

9.Alikuwa akiingia kwenye migahawa au kasino,bar hakuna mtu ataruhusiwa kutoka mpaka yeye amalize kilichompeleka pale..na bili zote watu walizo tumia analipa yeye.

10.Anaulinzi wa zaidi ya rais wa marekani na kwenye mizunguko yake ya kawaida anatembea na walinzi 15 makomandoo.

NB😀onge nono litatolewa kwa atakaye fanikisha kukamatwa kwake dola milioni 5 kwa marekani na 3.8 kwa mexico..jumla dola milioni 8.8..

View attachment 268553

Nawasilisha
 
Asante kwa kunifahamisha juu ya huyu 'mfalme' wa madawa ya kulevya.
Ninapenda sana kiswahili fasaha ndio maana nimeshangaa kwa nini kwenye namba 8 umeweka neno 'lakini'.Neno 'na' lingefaa zaidi kwenye mazingira ya sentenso hiyo!
 
Huyu Siyo tena mhalifu ni hero,very powerful man aise.Nimeona alikovunja na kupita chini kwa chini.Hii dunia we are not equal.Nasikia Kama kashafika kijijini kwao itakuwa ngumu sana kumpata maana wanakijiji wanampenda na hakuna anayethubutu kumtaja KWA police kuwa ameonekana!!!
 
Hiyo namba 4 ndio imeniacha hoi. Kwa ushauri tu, hata kama ukikutana na huyu jamaa jifanye kama hujamuona tu, kwasababu hata huko Mexico hakuna atakayethubutu kupokea hilo donge nono la $5m, maana huyu jamaa anaweza kufagia familia nzima mpaka kuku. Usnitch mbaya wajameni bora ufe masikini tu.
 
dah jamaa maisha magumu ndio yalichochea ila anakua shujaa wa mitaani
 

6.Selo yake ilikuwa tofauti na zingine alipata kila kitu alichokuwa anataka zikiwemo cocaine na malaya na alibadili selo kuwa kama hoteli yenye hadhi ya nyota tano.

Kuna vitu vingine watu wananogesha, mfano hii namba sita. (6). Angalia selo aliyotoroka El Chapo kwenye picha, sasa sijui Hoteli gani ya hadhi ya nyota tano iko hivi.

el-chapo-escape-ap-08-480w.jpg


el-chapo-escape-ap-02-480w.jpg


el-chapo-escape-ap-07-480w.jpg


el-chapo-escape-ap-03-480w.jpg
 
Kuna vitu vingine watu wananogesha, mfano hii namba sita. (6). Angalia selo aliyotoroka El Chapo kwenye picha, sasa sijui Hoteli gani ya hadhi ya nyota tano iko hivi.

el-chapo-escape-ap-08-480w.jpg


el-chapo-escape-ap-02-480w.jpg


el-chapo-escape-ap-07-480w.jpg


el-chapo-escape-ap-03-480w.jpg

Hii ni ni kifungo cha pili
 
Hii biashara ina hela sana, ingekuwa haya madawa hayana madhara kwa vijana wetu nadhani ningekuwa el chapo wa bongo.
 
Hii biashara ina hela sana, ingekuwa haya madawa hayana madhara kwa vijana wetu nadhani ningekuwa el chapo wa bongo.

hivi hujui vitu vya magendo vinaongoza kwa kuwa na faida sana..wakiruhuru kuuza hadharani faida itapungua coz kila mtu atakua na shauku ya kuuza
 
Kuna vitu vingine watu wananogesha, mfano hii namba sita. (6). Angalia selo aliyotoroka El Chapo kwenye picha, sasa sijui Hoteli gani ya hadhi ya nyota tano iko hivi.

el-chapo-escape-ap-08-480w.jpg


el-chapo-escape-ap-02-480w.jpg


el-chapo-escape-ap-07-480w.jpg


el-chapo-escape-ap-03-480w.jpg
Mkuu kumbe hata na wewe umeliona hilo yaani yaliyoongelewa hapo ya kweli ni kama mawili-matatu nyingine zote ni fix kama kumjengea mama yake akiwa na umri wa miaka 15 wakati akiwa na umri huo ndio aliacha kulima shamba la bangi la baba yake na kuanzisha lake.

Alafu hana wake wanne bali amekuwa na mahusiano na wanawake wanne kwa vipindi tofauti.
 
Back
Top Bottom