Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Kwanza kabisa ni ukweli usiopingika yapo maboresho makubwa yaliyofanywa na Bodi ya mikopo miaka ya karibuni kwa lengo la kuwa mfuko endelevu na kunufaisha Wanafunzi wengi zaidi.
Mabadiliko hayo kwa kiasi kikubwa yamewaumiza walipaji wengi hususani walioanza kulipa kabla ya mwaka 2017.
Kuna mambo makubwa matatu yanayofanya madeni ya walipaji kuonekana ni makubwa kuliko kiasi walichokopeshwa " principal loan"na mambo hayo ni:-
1.Asilimia sita(6%)inayokatwa kila mwaka kwenye kiasi cha mkopo kilichobaki " outstanding loan" baada ya kulipa. Hapa ina maana unapolipa mwaka mzima kiasi kitakachobaki kitatafutiwa asilimia sita na itajumlishwa kwenye deni lako.
2.Asilimia kumi (10%) penalty fee.Wahitimu wa kabla ya mwaka 2016 walipaswa kurejesha mikopo yao kabla ya miezi kumi na miwili kuisha tangu wahitimu chuo na kuchelewa kufanya hivyo ndani ya muda huo wa miezi 12 kunasababisha kukatwa asilimia kumi.
Baada ya mwaka 2017 ipo sheria iliyopitishwa na imefanya wanufaika kuanza kurejesha baada ya miezi ishirini na minne 24( miaka miwili) na miezi hii huanza kuhesabiwa baada ya kuhitimu ( graduation).
3.Asilimia moja 1% ada ya uendeshaji ". Administration fee "Ada hii hukatwa mara moja kwa mwaka kwenye kiasi kikuu(principal loan) cha deni la mkopaji.
Haya ndiyo mambo yanayosababisha tuone madeni kuwa makubwa kuliko kiasi tulichokopa.Ni vizuri tukijenga utaratibu wa kufuatilia ili kufahamu zaidi kwa kutembelea ofisi za bodi ya mikopo.