Dogoli kinyamkela
JF-Expert Member
- Nov 21, 2024
- 618
- 1,440
Changamoto kubwa ya wengi si kushindwa kufanya meditation, bali ni kitopata matokeo ya nia zao za kumeditate.
Mabingwa wa meditation kila wakati wanasisitiza faida zitokanazo na meditation, lakini sijaona hata mmoja akitaja hasara na kutoa suruhu kwa wanaofanya hivyo bila kuona mabadiliko yoyote, au kuona matokeo ya dhahiri.
MUNGU.Akinipa fursa nitaposti madhara ya meditation, sababu hakuna kisicho na madhara ukitumia vibaya, acha leo nitoe sababu za wanaohisi hawaoni matokeo.
Baada ya visa vya wanaoshindwa kuwa vingi nilirejea katika chanzo na haya ni sehemu ya niliyopata.
Mlango wa tano wa fahamu, chakra ya tano, kanisa la tano au kinara cha tano.
Katika Biblia ni kanisa lililoko Sardi.
Katika mwili wako mlango huu upo eneo lilipo koo.
Eneo lenye kuupa mwili uwezo wa kujielezea wenyewe pia kukuwezesha wewe kujielezea na Kubwa usilojua ndiyo mlango ambao unawezesha mwili kujilinda na hatari usizoziona, mambo ya kichawi, mapepo, machale n.k.
Mlango huu ukiwa wazi muhusika huwa muwazi, mkweli popote na kwa kila jambo, na maneno yake huchukuliwa kwa uzito mkubwa.
Mtu Ambaye mlango huu uko wazi mbali na kwamba hawezi kusema uongo, ukweli huohuo ambao unaweza kumdhuru mwenyewe, humfanya kutoka salama katika jambo baya.
Ndiyo wale wanaosamehewa katika jambo zito walilolifanya, kwa sababu walisema ukweli.
Mbali na hilo ni eneo zinakozalishwa hisia, taarifa dalili za mwili, dalili nzuri na mbaya juu ya jambo fulani na hata kukulinda na hatari zisizoonekana.
Mlango huu ukiwa wazi hulogeki, wala hudhuriki na vitu vibaya visivyoonekana.
Mfano wachawi wakikuvamia usiku utaamka gafla, na usingizi hauji mpaka watu au vitu vibaya viondoke au hali kuwa shwari.
Eneo hili ndiko hutokea nguvu zinazoweza kukukinga na madhara upitapo maeneo yenye roho wabaya Bila kunaswa.
Ni sehemu ya kazi za mlango wa tano, Sababu si sehemu ya mada wacha niendelee na vilivyo sehemu ya Mada.
Kila mtu ana ishara fulani za kimwili, zinazomsaidia kupata taarifa fulani kabla ya Jambo kutokea.
Mfano, kuna watu wakikaribia kupata pesa au kupoteza, huwashwa viganja vya mikono, kope za jicho hucheza n.k.
Mwingine kope, sikio, unywele hucheza akikaribia kupata taarifa ya msiba, harusi, au taarifa fulani mbaya au nzuri.
Zipo ishara nyingi zenye kutoa taarifa Ya yajayo kwa kila mwili wa mtu na ni mwili husika ndiyo unajua maana ya kila ishara Au aina ya taarifa.
Wanaojua ishara hizi, hutoa taarifa kabla ya tukio.
Mfano mimi, mboni ya chini ya jicho la kushoto ikicheza/ kuvuta, lazima msiba utokee.
Hilo ujue usijue lipo, ujue usijue hutokea. Busara ni kujua maana ya taarifa za mwili wako ili ujue kinachokujia mbele, Bila kupiga ramli kwa waganguzi.
Ishara kila mtu anazo, wengi hawajui tu ishara zao ni zipi, Sababu ishara zinatofautiana kati ya mtu na mtu.
Kwa kutojua ishara, alama au lugha ya mwili wako, ni sawa na kushindwa kusikia sauti ya Mungu baba, au Kristo walioko ndani yako, hivyo kukosa masikilizano baina yako wewe wa nje na wewe wa ndani.
Tukirudi kwenye meditation, nako pia tumetofautiana namna ya kupokea matokeo, sababu ya utofauti wa lugha Za miili.
Huyu atapata matokeo ndani ya meditation, na yule nje ya meditation.
Nikiwa na maana kuna wanaopewa matokeo katika maono, ndoto, moja kwa moja, kupitia mtu mwingine n.k.
Hivyo Namna mwingine anavyoweza kupata matokeo inaweza kutofautiana sana na wewe.
Mwili wa mtu ni kama mashine au mtambo ambao unaweka mzigo huku, matokeo unayapata upande mwingine.
Kama kupakua kitu U tube, unapakua kitu huku unakikuta katika eneo fulani la hifadhi.
Kama ni video ina sehemu yake, picha zinasehemu yake, nyaraka na kila kitu kina sehemu yake kinakohifadhiwa.
Kama hujui una weza tafuta kitu katika simu yako na usijue kimehifadhiwa wapi, sababu hujui wapi kwa kupata unachokikusidia kinachoingia na kutoka ndani ya simu.
ishara za mwili hutoa taarifa kupitia mwili bila ubongo, ikiwa na maana ni tendo ambalo liko nje ya uwezo wa mtu.
Katika mlango huohuo ndipo hupitia pia taarifa au maelezo ya kimungu ya moja kwa moja, yanayochakatwa kupitia ubongo.
Taarifa au maelezo hayo ambayo huletwa kupitia ubongo, unaweza kuyaona moja kwa moja kupitia mlango wako wa asili wa mwili wako.
Nimesema mlango wa asili wa mwili wako, nikimaanisha kila mmoja ana mlango wake wa asili wa kupokea maelekezo ya moja kwa moja ya kiMungu.
Katika post ya meditation, nilisema kuna wakati ambao anayemeditate anaweza kuona maono au kupata majibu umo ndani ya meditation.
Hili linawahusu wenye mlango wa asili wa maono, ( wenye uwezo wa kuwasiliana na roho).
Wengine wana milango ya asili ya ndoto.
Mtu huyu akimaliza kumeditate matokeo yake kwa ufasaha atayaona kupitia ndoto, kwa namna tofauti tofauti
Wenye asili ya akili au mawazo.
Mtu huyu akimeditate, matokeo yake yatakuja kwa kuzama katika fikra na kila atakachojiuliza kuhusiana na ombi lake, ataona anapata majibu, na kila kitu kinafunguka kirahisi.
Tuwe pamoja
SISI NI AFRIKA TU UMOJA.