Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Wote tunafahamu kuwa Baking Soda hutumika katika uandaaji wa vyakula kama keki na mikate. Lakini huwa na matumizi mbalimbali ya nyumbani ikiwemo kuwa mbadala wa kusafishia kinywa kwa kuwa na uwezo wa kuua bakteria.
Pia, baking soda ni nzuri kwa kuondoa madoa sugu. Inaweza kuchanganywa na sabuni kwa ajili ya kufua nguo, kusafisha mazulia, vyoo, na masinki. Hutumika kuondoa harufu mbaya kwenye jokofu, microwave na hata katika usafishaji wa viatu.
Baking soda ni njia bora ya kuondoa mabaki ya dawa za kuulia wadudu kwenye matunda na mboga kwa kuosha na machanganyiko wa maji ya moto.
Pia inatumika kung’arisha vifaa vya chuma kama vijiko, uma, na sufuria kwa kuchanganya na sabuni pamoja na maji ya moto kwa matokeo bora.
Kana una sinki limeziba unaweza kuzibua kwa kutumia mchanganyiko wa baking powder na vinegar saa kadhaa kisha mininia maji ya moto ili kuzibua uchafu.
Mchanganyiko wa baking soda na chumvi pia husaidia kufukuza wadudu kama siafu, sisimizi, na mende nyumbani, hivyo kuimarisha usafi na usalama.