Fahamu mawazo 10 yatakayo kusaidia kutengeneza kipato cha ziada

Fahamu mawazo 10 yatakayo kusaidia kutengeneza kipato cha ziada

Mapensho star

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
3,052
Reaction score
4,104
Kipato cha ziada huwa kinapatikana kutokana na uwekezaji na maandalizi tokea mwanzo.Baada ya kuwekeza mda na kufanya kazi kwa bidii ndipo pato huanza kupatikana itakuletea mapato thabiti bila kutumia nguvu
Tukiongelea kutokana na uzoefu wa mtu, kuongeza kipato cha ziada inasaidia kuogeza pato lako la kila siku na kukuza uchumi wako
Ikiwa unataka kupata kipato cha ziada hapa nataka ujue kitu gani unatakiwa ukijue kwanza

Vipato vyote vya ziada vinatokana na mambo haya mawili
1)uwekezaji wa pesa
2)uwekezaji wa muda
Hauwezi tengeneza kipato cha ziada kama hautotaka kutumia njia angalau moja kati ya hizo mbili
Kuna mawazo mbalimbali ambayo yatakusaidia kupata kipato cha ziada kutokana na kuwekeza pesa au muda

Mawazo ya kupata kipato cha ziada kutokana na kuwekeza muda
Hii ni aina kipato ambacho inahitajika ukitolee jasho na kuwekeza muda badala ya kutumia pesa kuja kutengeneza pesa baadae

Kwa kuwekeza muda ideas nyingi za kutengeneza kipato cha ziada zinapatikana kwa kuanzisha blog au website

1.Kuuza vitabu online
Kuuza vitabu imetawala siku za hivi karibuni kam vile unavyonunua kitabu kwenye website kubwa kama Amazon na wewe unakuwa na nafasi ya kuuza ni rahisi sana kabla haujasambaza unahitaji kuandika,kuedit na kutengenezea cover
usifikirie utapata mafanikio mara moja unahitaji muda kutafuta masoko ili kutengeneza kipato cha ziada

2.Kuuza kozi mtandaoni
Ni online platform ambayo inamfanya mtu kuchukua video ya kozi ambayo inakuwa na masomo mengi badala ya wewe kuwa mtumiaji anza sasa kuwa mtengenezaji wa video za kozi za masomo mbalimbali ambazo utawafanya watu wanunue ikiwa una ujuzi wa jambo fulani utakuwa na nafasi kubwa kubwa zaidi

3.Kuuza picha
Pengine inaweza kukushangaza kuona baadhi ya blog au website unayoipenda mda mwingine hata magazeti kutumia picha zako
Kuna website ambazo uta submit picha zako na utapata commission kwa kila mtu ambaye ananunua picha zako kuna site zifuatazo ambazo unaweza kuuza picha zako
12 Most Profitable Places to Sell Your Photos Online
4.kuwa na hati miliki ya videos youtube
Huu ni mradi ambao unakuwa kwa kasi unaweza ukatengeneza videos yoyote unayopenda inaweza kuwa muziki,vichekesho,muvi au video yeyote utayopenda then utaweka youtube mapato utayapata kutokana na watu kuclick matangazo yanayoonekana kwenye videos
5.Tengeneza App
Fikiria ni watu wangapi siku za hivi karibuni wanamiliki smartphone utakuja kuona ni idadi kubwa ya watu wanadownlod apps
Apps inawapa watu urahisi wa kuishi inaweza kuwa inawaweka watu pamoja au app ambayo ipo kwa shughuli muhimu
Pesa utapata iwapo utakua na account ya admob, fbads au kampuni yoyote inayohusika na kutoa matangazo kwenye mobile apps na ukiwa umeruhusu matangazo yao yaonekane kwako.
6.Nunua blog
Kuna maelfu ya blogs zinatengenezwa kila mwaka na kuna nyingi zinatelekezwa ,Ikiwa utanunua blogs kutokana na traffic unaopata tayari utaanza kutengeneza pesa
Blog nyingi zinalipwa na Google adsense mapato unayapata kwa mwezi pia badala yakununua blog unaweza ukatengeneza yako ukatengeneza kipato kizuri zaidi
7.Uza bidhaa zako mtandaoni
Kwa hii njia ya kuongeza unaweza ukatengeza website kwa ajili ya kuuza bidhaa zako au ukatumia mitandao kama facebook na instagram kuuza bidhaa kiurahisi
8.Network marketing
9.Car wash
10.Design T-shirts
Kuna site kama cafe press zinawawezesha watumiaji kudesign T-shirts endapo zitakuwa maarufu utafanya mauzo na utapata kipato chako
Pia Amazon wanafanya hii biashara inaitwa Amazon Merch ambayo ni rahisi una upload picha yako uliyodesign
 
Hii car wash inaongelewa sana siku hizi
 
vipi kuuza lubricants na oil mbalimbali, hasa kuanzisha kaduka kadogodogo kwa wenye mitaji midogo...
 
Pamoja na mawazo mazuri yooote yanayoweza kutolewa humu, binafsi, narudia tena binafsi, naaamini kwamba, wazo moja kubwa ambalo ukiwa nalo na ukiunganisha na mawazo mengine mengi ukafanikiwa ni TRUST...!!! Pigania kuwa trustworthy kwanza, then everything will fall in place...!!!

Kitu kingine cha kupigania ni FAHAMIKA NA WATU WENGI POSITIVELY...!!! Watu wengi wakikufahamu positively, ni rahisi kuja kukuungisha katika biashara yako. Hata ukiwa na hiyo car wash, kama hufahamiki na huaminiki, ni kazi bure. Ni rahisi kwenda kuosha gari yangu sehemu mbili, 1. kwa mtu ninayemfahamu (kufahamika), na 2. Sehemu ambayo naamini hawataniibia hata nikiacha laptop yng kwny gari (trust).

Pamoja na hilo, CHEKA NA WATU...!!! Sio unakuwa na biashara ila muda wite umekunja uso utafikiri umedhulumiwa chenji...!!! Cheka na wateja wako, no matter una biashara gani. They are the reason why wewe umefungua hiyo biashara.

Hayo ni mawazo yangu binafsi...!!! I stand to be corrected..!!!
 
vipi kuuza lubricants na oil mbalimbali, hasa kuanzisha kaduka kadogodogo kwa wenye mitaji midogo...
Funguka mkuu ikoje hyo biashara lubricant na oil unazitoa wapi wateja wakubwa wakinan
 
vipi kuuza lubricants na oil mbalimbali, hasa kuanzisha kaduka kadogodogo kwa wenye mitaji midogo...
Funguka mkuu ikoje hyo biashara lubricant na oil unazitoa wapi wateja wakubwa wakinan
 
Funguka mkuu ikoje hyo biashara lubricant na oil unazitoa wapi wateja wakubwa wakinan
hapa nazungumzia vilainishi na engine oil kama za oryx, caltex, total n.k.
mara nyingi huduma hizi zinapatikana kwenye filling stations.
so, vipi ukianzisha duka dogo la rejareja hasa kwa wenye mtaji mdogo...?
 
Back
Top Bottom