Kulingana na hali na wakati uliopo, kumekuwa na changamoto kubwa haswa upande wa ukuaji wa biashara na pia namna ya kutengeneza ukaribu na wateja. Ili biashara yoyote iweze kukuwa na kutengeneza faida ni lazima pia iongeze wingi wa wateja na pia kufanya wateja waendelee kuwepo kwa kuimarisha mawasiliano nao, kutoa offers mbali mbali na pia kutatua matatizo yao kwa wakati.
Kwanini Biashara nyingi zina aanguka ?
- Kupuuzia Matatizo ya wateja
- Kutofuata Ushauri na Mapendekezo ya watuamiaji wa huduma
- Kutokuwa na mawasiliano imara na wateja
Mbinu Sahihi ya kuimarisha Biashara yako
Kuna Mitandano kadhaa kwa lugha ya kigeni inaitwa Business Directory. Leo nitaongelea mtandao unaoitwa Bizyciti.
Business Directories - Hii ni mitandao inayosaidia wamiliki wa biashara kuweka biashara zao, ili ziweze kuonekana duniani kote. kwa mfano Yellopages, Directory ya Tanzania, na zoomtanzania.
Kwa kutumia mitandao hii unaweza kukuza biashara yako kirahisi na kisasa zaaidi
BizyCiti - Business Directory for Africa
Huu ni mtandao umeanzishwa kwa ajili ya wamiliki wa Biashara barani Africa. Nia yake kuu ni
- Kusaidia wafanya biashara kukua nje ya mipaka ya nchi zao
- Kuwezesha mfanyabiashara Kufanya biashara popote na wakati wowote
- Kupata maoni au reviews kutoka kwa watumiaji wa huduma
- Kutoa offers na kutangaza kuduma
- Kuwasiliana na wateja wakati wowote - unaweza kupokea message na kujibu
- Kuweka taarifa za kampuni yako - kama picha, mawasiliano, Eneo la biashara
- Unaweza kutangaza biashara yako na pia kutoa offers kwa wateja wako
- Na pia unapoweka biashara yako kwenye mtandao huu inapata nafasi kubwa ya kuonekana google, na pia kuaminika zaidi
- Wateja wanaweza kutoa maoni moja kwa moja kwenye ukurasa wa biashara