Fahamu mbinu zilizotumika kuwadhibiti watumwa kipindi cha utumwa na jinsi zinavyofanya kazi mpaka sasa

Fahamu mbinu zilizotumika kuwadhibiti watumwa kipindi cha utumwa na jinsi zinavyofanya kazi mpaka sasa

chofachogenda

Senior Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
107
Reaction score
199
FAHAMU MBINU ZILIZOTUMIKA KUWADHIBITI WATUMWA KIPINDI CHA UTUMWA NA NAMNA ZINAVYOFANYA KAZI SASA

Kwa kuanza kwanza inabidi tufahamu biashara ya utumwa ni kitu gani?

Biashara ya utumwa ilikuwa ni biashara ambayo ilihusisha kukamata, kuuza na kununua watu na kuwatumia kama watumwa.

Biashara hii ilikuwa infanyika duniani kote hapo kipindi cha zamani lakini leo ningependa hasa kugusia kuhusiana na Trans- antlantic slave trade ambayo inakadiriwa waafrika takribani milioni 10 mpaka 12 walisafirishwa kutoka Africa mpaka bara la Amerika kupitia bahari ya Antlantiki toka karne ya 16 na kuisha karne ya 19.

Na hii ndio imesababisha kwa kiasi kikubwa uwepo wa watu weusi katika America hivi ni vizazi vya watumwa ambao babu zao walipelekwa kule kipindi cha biashara hii haramu ya utumwa

Lakini lengo la uzi huu sio kuongelea hasa kuhusiana na namna biashara ilivyofanyika la hasha, lengo langu hasa ni kuonyesha namna gani wazungu walifanikiwa kukaa ama kuwadhibiti watumwa wasilete uasi bila shida kwa kutumia mbinu mbalimbali hasa kubwa ikiwa ni kwa kutumia udhibiti wa akili (mind control)

Moja kwa moja twende katika kuangalia ni mbinu gani hasa ambazo hawa wamiliki wa watumwa walikuwa wakizitumia ili kuendelea kuwafanya watumwa kubaki kuwa watumwa

1. Kuondoa utambulisho wao

Kitu cha kwanza kabisa wakati zile meli zilipokuwa zinafika katika maeneo husika wale waafrika walikuwa wanaamuriwa kuondoa vitu vyote ambavyo vinawakumbusha kuwa wao ni nani au wametokea wapi na hapa kwa mlioangalia movie ya roots mnaweza ona Kintakunte alivyolazimishwa kubadili jina na kuitwa Thobias ingawa leo sisi tunaona ufahari kuitwa majina ya kizungu na kiarabu na sio majina yetu ya asili hatujui kwamba majina yetu yamebeba utambulisho wetu na kila jina lina nguvu yake hujiulizi kwa nini tukibatizwa au kusilimu unapewa jina la kizungu au kiarabu unajua kwamba ukisikia neon Chong Li ushajua kwamba huyu ni mchina bila hata kumuona itoshe kusema sisi watumwa pasipo na minyororo.

Cha kwanza kabisa walikuwa wanavuliwa nguo zote na kunyolewa vipara (Hii mbinu hata jeshini inatumika)

Hii ilikuwa na namna moja tu ya kufanya watumwa wajue kwamba vyovyote ulipokuwa umetoka ama ulikuwa kiongozi au mtu mashuhuri kwenye kijiji chako ndio basi tena hauna unasaba na huko ulipotoka bali wewe sasa hivi ni mali ya mtu na umekuja kuanza maisha mapya kama mtumwa katika eneo husika.

Hadi sasa ni watumwa na tumepoteza utambulisho wetu kama waafrika Zaidi ya kuwa wafuata mkumbo tu huku tukiwa na nywele bandia za kizungu, tumejichubua ngozi, dini za kuletewa, mavazi ya kizungu n.k hawa jamaa kweli wametuweza

2. Kuwatenga waafrika waliokuwa wanaongea lugha moja ili wasiweze kuwasiliana na kupanga aina yoyote ile ya uasi.

Kwa hiyo lugha zote za kiafrika zilikuwa ni marufuku katika maeneo ya watumwa na lugha pekee iliyokuwa inaruhusiwa mfano kwa watumwa wa marekani ilikuwa ni kiingereza peke yake.

Kwa sababu hii wale watumwa ambao ndio walikuwa wanakuja au watumwa wapya walikuwa hawawezi kusoma ama kuandika kiingereza na ilibidi wafundishwe na watumwa ambao wamezaliwa hapo (watumwa ambao wamezaliwa kwenye eneo la slave master).

Kwa hiyo wale watumwa ambao wamezaliwa utumwani walikuwa wanawaona wale watumwa wapya kama vilaza kitu ambacho kiasi Fulani kilitengeneza matabaka kama mjuavyo umoja ni nguvu utengano ni udhaifu maana hapa kondoo walikuwa wanachunga kondoo na kumpunguzia kazi mchungaji.

Kwa msisitizo hebu tuangalie maisha yetu ya leo tu mtu anayejua kiingereza ndio anaoneka msomi na ameenda shule na yule ambaye hajui anaonekana sio msomi na hi ipo kote nchi zilizotawwaliwa na mfaransa waafrika wanaoongea na kukijua kifaransa wanaona maisha wameyapatia, ukienda nchi iliyotawaliwa na ureno hivyo hivyo sasa tuna Anglophone na Francophone ndani ya Afrika n.k

Kama unafikiri upo huru ni unajifurahisha tu na ukifikiri hili jambo ni bahati mbaya ni sawa pia ila tambua kwamba hivi vitu vilianza kufanyiwa mazoezi na baade tukaletewa na kukubali kwa hiari yetu huku tukiona ufahari

anglop.jpg


3. Kutengeneza hofu kuu miongoni mwa watumwa

Katika namna ya kuhakikisha kwamba mtumwa anatawalika kwa urahisi na haleti upinzani wa aina yoyote basi mojawapo ya njia iliyoukuwa inatumika ilikuwa ni kutengeneza hofu kwa kumshughulikia ipasavyo mtu yoyote ambaye alikuwa anaonesha aina yoyote ya utovu wa nidhamu.

Hii mbinu ilisaidia kwa kiwango kikubwa kutengeneza utii na nidhamu miongoni wa watumwa Mfano mtumwa ambaye alikuwa anaonekana mkorofi alikuwa anafungwa kwenye mikono yake kamba ambayo pia inafungwa kwa farasi wawili tofauti ambao wana amrishwa wakimbie pande mbili au unafungwa kwenye mti na kuchapwa mijeledi ya kutosha mbele ya watumwa wenzake tofauti mpaka yule mtu anachanika kati kati na kufa wakati huo watumwa wenzake wakiangalia basi hicho kitendo kitachukuliwa kama kitendo cha wamama kuchunga watoto zao wasifanye kitendo chochote cha uasi maana kitawakuta kitu kibaya hivyo kufanya kizazi cha watumwa kutii mabwana zao kizazi hadi kizazi.

Hii mbinu ya kutengeneza hofu unatumika mpaka leo katika kuwatawala watu sio hapa tu mpaka huko nchi za nje ili serikali ziweze kufanya mambo yao kwa urahisi ndio chanzo cha kuanzishwa hata kwa vikundi vya kigaidi maana mtakapoogopa mwisho wa siku mtakubaliana kwa urahisi na pendekezo lolote ambalo serikali itakuja nalo na mtaambiwa ni kwa usalama wenu haijalishi hilo pendekezo kama litapora uhuru wenu ama la

fano ilipoingia corona na kutangaziwa idadi ya vifo nani asiyeogopa kufa kila siku kuna watu hapahapa kwetu walikuwa wanaomba wafungiwe ndani ila baada ya kuondolewa hofu maisha yalirudi kama kawaida.

a mfumo unaotumika na wakubwa wa dunia ni kutengeneza tatizo ambapo kwenye jamii kutazuka taharuki ama watu watareact alafu watakuja na suluhisho (problem-reaction-solution). Na hofu ndio msingi mkuu.

SLAVE 3.jpg


4. Kutenganisha wanafamilia

Kwa kifupi kipindi cha utumwa watu walichukuliwa kama wanyama tu kwa hiyo kama wewe ambavyo kuku wako akitotoa watoto unamnyang’anya vifaranga ndio kitu kilichokuwa kinafanyika anaingia slave master anachukua mtoto wako ambaye anaenda kulelewa sehemu nyingine kabisa na kwenda kufundishwa tamaduni nyingine kabisa na ulikuwa huwezi fanya kitu chochote kitu ambacho kilikuwa kinawaumiza sana kisaikolojia watumwa na hii ilisaidia sana kwa sababu wale watumwa waliotoka afrika walishindwa kuwapa ujuzi au elimu kuhusiana na wapi walipotoka hivyo wanakua hawajui chochote kuhusiana na Africa au sehemu walipotokea.

Kwa sasa shule pamoja na Tv na mitandao ya kijamii ndio inayotunyangánya watoto wetu ambapo watoto wanajifunza mambo yote huko wakati wazazi tukiwa busy na harakati za maisha matokeo yake watoto wanafundishwa huko historia zinazotukuza wazungu na vizazi vyao, tunaona ufahari kupeleka watoto English medium wakati mwanao hajui kuongea kisambaa ambacho ndio asili yake, atafundishwa maisha ya kizungu ya kula kwa uma ndio ustaarabu, huku mitandao ikimfundisha namna ya kutumia madawa na kuangalia staili za ngono wakati huo huo tunapotezea kuhusu jando na unyago na bado unajiuliza kwa nini ndoa za siku hizi hazidumu.

Itoshe kusema wewe bado ni mtumwa sema tu ni mtumwa wa kisasa

5. Kutumia Ngono kama chombo cha madaraka na udhibiti

Kipindi cha utumwa wale wazungu walikuwa wanaangalia mbegu bora kama sasa hivi tunavyopandisha beberu kubwa na jike lililonona ili kupata mtu ambaye atakuwa na sifa hizo au kupata mbegu bora nzuri Zaidi.

Kilichokuwa kinafanyika ni kwamba alikuwa anachukuliwa dume ambalo lina misuli na limepanda hewani labda kutoka katika shamba moja(plantantion) au eneo moja ili kwenda kufanyishwa ngono na mwanamke ambaye nae atakuwa na mwili mkubwa na wenye nguvu ili wwapate mbegu bora ya watumwa kwa hapo baadae, kwa hiyo ilikuwa haijalishi mnajuana au hamjuani, mnapendana ama la ila mwanamke utaletwa chini ya usimamizi wa wazungu jamaa atafanya ngono nae alafu akipata mimba na kujifungua yule motto atachukuliwa.

Lakini njia nyingine iliyokuwa inatumika ni kulipwa kwa vijana wa kizungu ambapo walikuwa wanalipwa kiasi cha $ 20 kwa kipindi hicho ili kufanya mapenzi na watumwa ili kupata watoto ambao ni nusu mzungu nusu muafrika ambao tunaita half cast yaani mtoto ambaye ni mchanganyiko wa mzungu na muafrika hawa watoto baadae walikuwa wanatumika kama wasimamizi katika mashamba huko hivyo ule mfumo wa kondoo wa kuchunga kondoo wenzao ukawa unaendelea huku slave master wakila bata, hawa watoto ambao ni mixer walikuwa wanapewa hadhi kidogo ukilinganisha na wale black pure.

Lakini pia ukiachana na hilo wale watumwa wa kiume walikuwa wanaingiliwa kinyume na maumbile hii mbinu ilikuwa inajulikana kama “breaking the buck”mbele ya familia zao na mbele ya watumwa wenzao na hii mara nyingi ilifanyika kama kulikuwa na aina fulani ya upinzani eneo hilo hivyo atachukuliwa mtumwa wa kiume mmoja anaye ana nguvu atachapwa mijeledi baada ya hapo ataingiliwa kinyume na maumbile baadae yule slave master atawaalika na wenzie kutoka sehemu nyingine naye watamlawiti hii kitu ilikuwa inawaathiri sana kisaikolojia wale watumwa walioingiliwa na kuona wamepoteza nafasi yao kama wanaume katika jamii na kupelekea baadhi yao kujiua hii ilitengeneza hofu kubwa sana baina ya watumwa hivyo kuwa wapole au mwanamke kubakwa mbele ya mume wake na hii kiasi fulani lishusha sana suala la kujiamini kwa mwanaume aliofanyiwa kitendo hicho na kufanya wanawake zao kutokuwa secure na hali iliyopelekea baadhi ya watumwa kuwa michepuko ya slave master kwa ajili ya kupata aina fulani ulinzi ambayo waume zao wameshindwa ku offer.

Hii kwa sasa kuingiliwa kinyume na maumbile huwa inafanyika kwa namna nyingi lakini wanatumia sana movies kuingiza vitendo hivi kweny jamii yetu mpaka akili zetu zikubaliane kuwa ni kawaida na kweli naona watu wengi wa mijini washaanza kuona ni jambo la kawaida na kama zamani watu walikuwa wanaangalia mwenzao akifanyiwa hivyo ndivyo hivyo leo unavyokaa sebuleni kwako na kuangalia hizo sizoni (season) zilizojaa ushoga na usagaji na kupelekea baade kuiga na kufundishwa kuwa proud na hilo tatizo ambalo kimsingi ni la akili na sio kimwili badala ya kulitafutia ufumbuzi anaambiwa alikumbatie.
View attachment 1796279

6. Mfumo wa kubagua watumwa kulingana na rangi zao

Kama nilivyoeleza hapo juu kulikuwa na mfumo wa kulipa wazungu hasa wanafunzi kwenda kuzaa na watumwa kwa ajili ya kupata watoto ambao watakuwa ni mchanganyiko wa rangi yaani baba mzungu mama mswahili kazi kubwa ya hichi kizazi cha half cast au mulatoes ni kuja kuwa wasimamizi wa mashamba na wengine walitumika kama vimada (concubines) wa slave masters.

Hivyo hawa walikuwa wamewekwa daraja la juu kidogo la wale slave wale weusi tii wenyewe wanapenda kusema walikuwa ni “house nigger” yaani zao hasa za kinyumbani nyumbani wakati wenzangu na mimi hawa waliitwa “field nigger” hawa ndio waliokuwa wanapambana mashambani huko.

Hii mbinu ilitumika kwa ajili ya sababu kadhaa ikiwemo kutengeneza ile kitu inaitwa divide and rule lakini pia kuwakumbusha watumwa kwamba nani ana mamlaka kwenye eneo husika yaani umezalishwa bila ridhaa yako umenyonyesha motto baada ya hapo unanyangánywa na huyo motto baadae anatumika kuwagandamiza nyinyi wenyewe.

Hapa kulikuwa na mgawanyo huu hapa

Mzungu akizaa na muafrika hawa mtoto wao alijulikana kama Mulatoes mfano Bob Marley au Obama n.k

Alafu Huyu mtoto wa aliyezaliwa na mzungu na muafrika yaani akija kuzaa na mzungu pure huyu aliitwa Quadram mfano tuendelee na Bob Marley alipozaa na Cindy Breakspeare ambaye ni mzungu pure wakamzaa Damian Marley ambaye huyu sasa ndio Quadram

Alafu huyu Damian Marley akizaa na mzungu yule mtoto wao anakuwa Actrum

Yaani hapo kuna ½ , ¼, 1/8 na kuendelea madaraja yao yalikuwa juu kulingana na daraja uliopo ila kumbuka hawa wote walikuwa wanajulikana kama Nigger tu mbele ya wazungu.

Ndio maana Jay Z katika wimbo wake The story of O.J anasema light nigga, dark nigga, faux nigga, real nigga, rich nigga, poor nigga, house nigga…. Still nigga, still nigga”

Na hapa ndio kulikuwa na kitu kinaitwa “one drop rule” huu ulikuwa ni mfumo ulioasisiwa hapo marekani hasa kipindi hicho wa kuwatenganisha watu kulingana na rangi zao za kwa hiyo hata kama babu wa mababu zako alikuwa mweusi au bibi wa mabibi zako alikuwa mweusi wewe race classification yako ni mweusi au black ndio maana Obama tunamuita ni mweusi au Mariah Carey ni mweusi ingawa hawa wakija huku kwetu tunawaita wazungu.

Kwa hiyo sio lazima uwe mweusi wa rangi ila kama una asili ya weusi kwenye uzao wako (invisible blackness) wewe unabaki ni mweusi tu. Hili lipo wazi tu sehemu nyingi ambapo kuna wazungu ma watu weusi mpaka leo hii katika dunia ya utandawazi bado muafrika anakandamizwa kulingana na rangi ya ngozi zao na hata hapa kwetu kwenye weusi tii basi yule ambaye anaonekana mweupe(light skinned) basi ndio anaonekana mzuri na kupelekea dada zetu wengi kukosa kujiamini na rangi zao nyeusi na kuishia kujichubua kwa kuamini kwamba watakuwa warembo zaidi nah ii ndio uzuri wa mfumo ni kuuanzisha tu na ukianza kufanya kazi basi unakuwa automatic na watu watadhani wanafanya kwa hiyari yao kumbe la kuna nguvu inawasukuma bila kutambua nii ndio maana halisi ya mind control

bob marly - Copy.jpg


7. Kulazimisha watumwa kuwa wakristo

Watumwa walipofika katika eneo husika katika eneo husika kitu cha kwanza ilikuwa ni kubatizwa na kuwa wakristo. Unafikiri hawa wazungu pamoja na unyama wao wote walitaka waafrika waende mbinguni?

Jibu ni hapana ila hapa dini ilitumika kama nyenzo ya kuwa dhibiti (control) watumwa huku maandiko ya biblia yakitumika katika mbinu hiyo. Hii ni kwa sababu watumwa wakristo wamefundishwa kwenye biblia kwamba wawaheshimu na kuwatii mabwana zao (waefeso 6:5, wakolosai 3:22-24 na maandiko mengi ambayo yalikuwa yanahalalisha utumwa Kwa hiyo walikuwa wapo radhi kuvumilia yote wanayokumbana nayo sababu ya kristo, na pia walikuwa wakiamni kwamba watapata ukombozi kupitia kristo kwa hiyo kulikuwa hakuna haja ya kutumia nguvu kwa hiyo waliendelea kubaki na tumaini la uongo huku wakiendelea kuwa kondoo watiifu kwa kutumia maandiko mbalimbali ktoka kwenye biblia na kwa kiasi kikubwa mbinu hii sio tu ilipunguza upinzani lakini pia ilitwaa uhuru wa kuabudu wa waafrika wa kuangalia msaada kutoka kwenye mizimu yao au dini zao lakini wakawa wanasubiri ukombozi kutoka kwa yesu wa kizungu.

Hii mbinu iliendelea kutumika mpaka kipindi ambacho wazungu walipokuwa wanajiandaa kuja kutawala afrika na moja ya vitangulizi wa ukoloni walikuwa ni wamisionari na kazi yao ilikuwa ni moja tu kuwaandaa wafrika kwa ajili ya ukoloni na mpaka leo tena waafrika hatuhitaji tena hatuhitaji wakoloni tena ili kuziendeleza hizi dini bali tutachagishana wenyewe tukijenga kanisa na misikiti na huku macho yote kwa mabwana zetu ambao wametuletea dini ambao nao wanaonekana sasa hawana mpango nayo kivile ndio maana leo ikipigana Israel na Palestina leo watu huku kwetu wanatetema kwa hasira na kutoleana povu kuliko wakipigana Congo ama Afrika ya kati.

Na Leo Afrika imejaa Makanisa na misikiti na ikiwa inanuka ufukara tukingojea ukombozi kutoka juu badala ya kujishughulisha. Kuna jamaa aliwahi kusema wakati waafrika (wakristo) wakisema tunalindwa na Mungu wa Israel huko Israel kwenyewe wanajilinda kwa makombora ya kutisha badala ya kusubiri Mungu wao awalinde.

KIla kitu cha jadi kinaonekana ni ushirikina ndio maana leo ukiunga mkono nyungu unaonekana ni mshirikina na haujui lolote kuhusu sayansi ila nyungu hiyo ikiitwa jina la kizungu kwa jina la steam therapy wenyewe wanasemaga lugha ya kitaalam na wangekuwa wanatumia wazungu na hatuweki kwenye sufuria ila kimtambo fulani hivi kila mtu angeona fahari kutumia.

Si unaona raha mfumo hiyo yani unauseti alafu mambo yanajiseti…kifupi tunasema alinunua babu mpaka mjukuu analitumia.

nyngu 2.jpg
nyungu - Copy.jpeg




Kwa kifupi hizo ni baadhi ya mbinu ambazo zzilitumika ili kuwafanya waafrika watawalike (mind control) na ukiangalia kwwa jicho la tatu ni mbinu hizohizo ndio zinaendelea kutumika mpaka sasa zikiwa na maboresho kulingana na muda tu na sasa hivi haitumiki nguvu kubwa ili zifanye kazi tunazibeba kwa hiyari yetu na kudhani ni ufahari.

BENJAMINS
 
Walikuwa wana lazimishwa kuwa Wakatoliki, make enzi hizo Dini ilikuwa ni hio pekee yake Kabla ua wakina Mariton Luther kujana zile movement zao karine ya 16 na kupelekea Uprotestant kuenea hadi Marekani
 
Nini kifanyike?
Anza wewe tupa hata hiyo simu unayotumi maana ni utumwa kutumia vitu vya wazungu. Vua hizo nguo vaa magome ya miti au ngozi.
 
Back
Top Bottom