Fahamu Mgogoro wa Taliban na Afghanistan

Malengo makuu ya Marekani iliyowafanya wao wapeleke majeshi Afghanistan karibu malengo yote yalitekelezwa.
Malengo makuu ya Marekani kupeleka Majeshi Afghanstan takribani yote yalitimia , jambo liliobaki ni kuandaa mpango na makubaliano ya kuondoa majeshi yao kutoka Afghanistan baada ya miaka mingi majeshi yao kuwepo Afghanistan.
Mkuu, 'Abdul Nondo', nawe unaamini malengo yalifikiwa?

Malengo yangefikiwa, hali ya Marekani kuondoka isingekuwa ya vurugu kiasi hiki kinachoonekana.

Huu ni mfano mwingine wa kushindwa kufikia malengo yaliyowapeleka huko.

Bado kuna maswali mengi ambayo hayana majibu katika andiko lako. Nguvu ya Taliban nchini humo inatokana na nini?

Ni kitu gani hasa kinachowafanya wawe na nguvu, kuna makundi ya raia wa nchi hiyo wanaopenda sana aina yao ya uongozi?

Haya, kuna haya mengine ya pembeni: M7 anachukuwa wakimbizi wa Afghanistan, bila shaka kwa kitita alichoahidiwa kupewa! Dunia hii haiwezi kuishiwa na vituko kamwe!
 
Sheria zenu za kiislam za kutesa na kuuwana ndio zinachochea mauji maeneo mengi duniani ,Kama dunia isinge kuwa na uislam ingekuwa salama sana


USSR
Kwanza Taliban hawafuati sheria za Kiisilamu Bali Mila zao.

Kwa Dunia Ya sasa hakuna Nchi inayofuata sheria za kiisilimu 100% ila zipo zinazofuata kwa Asilimia kadhaa, na jambo moja ambalo ni Fact nyingi Zina Maisha Mazuri.

Nenda Middle East Angalia Qatar, UAE, Saudia, Oman Etc

Nenda Nchi za South East Asia Angalia Malyasia, Indonesia, Brunei etc.

Nchi zote hizo zimefanikiwa Kutengeneza welfare state, na ndio Uisilamu unavyofundisha. Wanamaisha Mazuri sana ni nadra kukuta watu Wana Umasikini wa kupindukia.

Hizi ni nchi na umasikini

Utaona Nchi zenye masikini wa chache nyingi ni za kiisilamu, na nchi zenye masikini wengi ukikuta za kiisilamu basi ni zile zilizogubikwa na Vita.
 

kwaiyo unataka kusema uisilamu inabidi ubadilike kutokana na maitaji ya dunia
 
kwaiyo unataka kusema uisilamu inabidi ubadilike kutokana na maitaji ya dunia
Uisilamu hauhitaji kubadilika ila kila unavyo embrace Uisilamu ndio jinsi unavyopata state inayojali wananchi,

Kwa Historia ya Uisilamu kuna kipindi cha Abbasid Nchi inakuwa na hela mpaka anakosekana masikini wa kupewa zaka.

Ndio maana unakuta hizi Nchi zenye waisilamu wengi zikiwa na Rasilimali kidogo tu Basi Nchi nzima inakomboka.

Angalia Nigeria ama Gabon na wao Wana mafuta pia, Nigeria Ni nchi ya 10 Duniani kuwa na Mafuta mengi na ya kwanza Africa nzima, Wanazalisha Mabilioni ya Barells ya Mafuta.

Kwa Siku Nigeria wanazalisha kama Barell 2.5 million za mafuta, kwa bei ya Dola 66 tunaongelea mamia ya Billioni kwa siku na Trilioni zinazokaribia 100 kwa mwaka toka bidhaa moja tu.

Lakini Angalia Maisha ya watu wao, ni hovyo kabisa, masikini kulinganisha na Nchi zenye Mafuta Nyingine. Ila wangekuwa na mfumo wa welfare na kuachana na ubepari leo wangekuwa mbali.
 
Safi mzeee...sijawahi kujua kuwa upo jf...naomba uandike makala kuelezea urafiki ulikuwepo baina ya osama,mullah omar na marekani kabla hawajagombana
 
Pmj sana mkuu uko vzr Sana
siku moja nikiwa na ole sabaya usku kati ya saa nne usku mwak jan mwez wa tano HV ole sabaya alikupigia simu na ulifurahi Sana [emoji38][emoji38] naomba usibishe mmkuu sabay alikuwa na nmba zako anapenda kukupigiaa Sana kukusihii kuacha kumkosoa jiwe ....au siwew
 

kwanini haujagusia swala la terrolism???
 
kwanini haujagusia swala la terrolism???
Ni Terrorism sio Terrolism.

Mkuu definition Ya Terrorism ni mtu anaetia hofu, huwa hawa wanaua ama kufanya Uhalifu Bila Material gain, Taliban sio Terrorist sababu inajulikana kabisa wa nataka Nchi hawa ni waasi,

Kuhusu Uisilamu na ugaidi Almost Maeneo yote yenye ugaidi kuna mkono wa USA na washirika wake.

Miaka kadhaa iliopita Libya, Iraq, Syria, Yemen, Somalia na kwengineko zilikuwa ni nchi zenye Maendeleo na maisha yanakwenda kama kawaida, hao jamaa kuingia Affairs za watu na kupindua viongozi, kufadhili makundi na kuua Raia wasio na hatia ndio wanaleta machafuko kila eneo.

Kuhudumia Jeshi mkuu si jambo la kitoto, tunazungumzia matrilioni ya Hela, wanajeshi most of times hawazalishi imagine umlishe, umvishe, umnunulie silaha, umlipe etc unafkiri tu somewhere unaweza ukaanzisha kikundi cha ugaidi ukawa na silaha na funds za kuweka watu kambini bila ufadhili?

Magaidi wengi wanafadhiliwa na Nchi kubwa na Historia Angalia vikundi vingi vya ugaidi zamani vilikuwa funded na USA. Hata hawa wetu AL shabaab ukiangalia Historia yao imeanzishwa na mwanadada Samantha.

Tafuta Makundi yote ya kigaidi kuanzia Hao kina isis mpaka huku kwetu Al shabaab wanaua zaidi waisilamu kushinda watu wowote, zaidi ya Asilimia 90 ya watu wanaouliwa ni waisilamu, why vikundi vimavyojinasibisha na Uisilamu vinaua kila siku waisilamu na hata havitetei haki za waisilamu.

Kama kweli kuna vikundi vya waisilamu
1. Palestine wasingekuwa wanaouliwa vile.
2. Tumeona Myanmar waisilamu wanavyochinjwa kwa maelfu
3. Tunaona Uyghur China waisilamu wanavyoteswa.

Kote huko husikii vikundi vya waisilamu wala hakuna anaewatetea, ila kina Isis Wana operate Maeneo ambayo ni almost 100% waisilamu na wanaua waisilamu, huoni hizi ni danganya toto tu?.
 
nikadhani sasa naenda kupata uchambuzi wa maana kumbe habari ni zile zile ambazo kila mtu anazijua hkn uchambuzi wowote wa maana ulioufanya hpo zaidi kuzipata kwa kifupi sn kwenye blogs uchwara
 
Nashukuru nimepata mwangaza kidogo
Nini maoni yako kuhusu Serikali ya Wataleban itakuwa ni ya namna gani?
 

Shukrani kwa majibu mazuri JF inaitaji watu kama wewe, kaswali kangu ka mwisho, nini mtazamo wako juu ya bakwata unazani inalinda na kutetea uisilamu na waisilamu kama inavyotakiwa?
 
Sasa wewe ndio hueleweki kabisa nadhani una mihemko ya hali ya juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…