Fahamu namna timu ambazo hazitaanzia hatua ya awali mashindano ya klabu bingwa Afrika zinavyopatikana

Fahamu namna timu ambazo hazitaanzia hatua ya awali mashindano ya klabu bingwa Afrika zinavyopatikana

kwa kuongezea, kwa timu zinazoshiriki CCL msimu huu wa 23-24 Simba ni ya 7!

juu yake kuna Raja na Berkane ambao hawatashiriki CL kulingana na nafasi walizopo kwenye ligi yao ya ndani, hivyo ni sahihi kusema Simba yupo namba 7 kwa timu zilizopo CL
Simba ni ya 7, na juu yake kuna Zamalek na Raja ambazo hazishiriki champions League, hivyo kwa timu za CL Simba wanashika namba 5. Kuna uwezekano mkubwa Simba ikainzia round ya pili. Mwaka huu kila timu shiriki lazma iwe na timu ya kike, zipo timu zitashindwa na usishangae hata Yanga anaweza kuanzia round ya pili
 
Kuna kundi kubwa la watu wamekuwa wamekariri tu kuwa msimu fulsni timu nane hazitoanzia hatua ya awali lakini hajui hata ni vipi inapatikana na pia hajui kama idadi aliyotaja inaweza kuwa sahihi au isiwe sahihi.

Sasa uzi huu faida kwa member anayeongoza kwa nyuzi za udaku, uongo na fitna na pia na wachambuzi na wana michezo mbalimbali wasiojua ni kwanini kuna timu zinatokea hazianzii hatua ya awali.

Shirikisho la soka barani Africa (CAF) ina jumla ya wanachama 54, na katika hao kuna wanachama 12 ambao wanapaswa kuingiza timu mbili mbili katika mashindano ya klabu bingwa, na wanachama 42 waliobaki wao wanaingiza timu moja moja tu klabu bingwa.

Katika mashindano ya klabu bingwa timu zinapaswa kutoana ili zibakie timu 32 ambazo zitacheza mtoano ili zipatikane timu 16 za kucheza hatua ya makundi.

Kutoanza kwa baadhi ya timu katika hatua ya awali ni kutokana na wanachama wengine kutoshiriki michuano ya klabu bingwa kutokana na sababu zao mbalimbali ikiwemo uchumi, na miindo mbinu yao hivyo kutokuwasilisha timu zao kucheza michuano hiyo.
Laiti kama ikitokea kuwa wanachama 52 wameamua kushiriki michuano ya ngazi ya vilabu, itafanya kuwe na idadi ya timu zifuatazo;
Association 12 timu mbili mbili = timu 24
Association 40 timu moja moja = timu 40
Hivyo jumla itakuwa ni timu 64 zitakazoshiriki klabu bingwa
Kwa mazingira ya namna hiyo ikitokea, hakutakuwa na timu yoyote amvayo haitoanzia hatua ya awali. Timu zote zitapaswa kucheza kwanzia hatua ya awali, kisha zitatoana na kubakia timu 32 ambazo zitacheza hatua inayofuata.

Naomba nije kumjibu GENTAMYCIME hoja yake ya kwamba Simba na timu zingine saba hazitaanzia hatua ya awali.

Cha kwanza ieleweke kuwa kuelekea msimu wa 2023/2024 zitachukuliwa performance ya misimu mitano ambayo itaanzia msimu wa 2018/2019 mpaka msimu wa 2022/2023 ambapo Simba inashika nafasi ya 9, hivyo haitokuwa Simba na timu 7 kwasababu Simba haishiki nafasi ya 8 bali ilipaswa kusemwa Simba na timu 8. Tuje sasa kwenye uhalisia je ili Simba isianzie hatua ya awali msimu ujao ni mazingira yapi yatokee?

Ni endapo itatokea timu 55 pekee zinazoshiriki michuano ya klabu bingwa msimu wa 2023/2024 badala ya timu 64, kwa maana ya wanachama 43 pekee ndio walioshiriki michuano ya CAF ngazi ya vilabu kati ya wanachama 54.

Kutokana na mazingira ya hapo juu, endapo wanachama ataongezeka kutoka kwenye hiyo idadi ya 43 ndivyo na idadi ya timu ambazo hazitoanzia hatua ya awali zitapungua. Na endapo idadi ya wanachama kutoka 43 watazidi kupungua, itasababisha idadi ya timu zisizoanzia hatua ya awali kuongezeka.

Mwisho nahitimisha kuwa hakuna msimamo au guarantee ya kuanzia hatua ipi katika michuano ya klabu bingwa mpaka ijulikane wanachama wangapi watashiriki michuano ya klabu bingwa msimu husika.
Hapa Yanga mwenzangu bora ungenyamaza tu umekuja kutudhalilisha Yanga wote. Unazidi kuwapa kichwa jamaa . Ranks zinaonesha wameshika nafasi ya ngapi. Au unataka tu kukazia watucheke zaidi?
 
[emoji120][emoji120] Mkuu wewe ni mpenzi wa mpira, nashukuru kwa masahihisho hapo kwenye raundi ya timu 8. Ni vigezo vipi vitakavyotumika kuzipata timu za kucheza hiyo raundi ya timu 8?
sio kwa ubaya lakini,, kwann asiwe yanga sasa, awe simba??
 
Hapa Yanga mwenzangu bora ungenyamaza tu umekuja kutudhalilisha Yanga wote. Unazidi kuwapa kichwa jamaa . Ranks zinaonesha wameshika nafasi ya ngapi. Au unataka tu kukazia watucheke zaidi?
Sasa kuwapa kichwa kivipi? Kama wamefanya vizuri ni haki yao kujivunia sasa kwanini tunaonee wivu kwa kusema nawapa kichwa? Na sisi ndio tupambane tufike mbali klabu bingwa ili tutambe na rank.
Kwenye rank ambayo itakayotumika katika mashindano ya msimu unaoanza Simba ipo nafasi ya 9.
 
kifupi ushiriki wa simba kwa kuto kuanzia hatua ya mtoano itatokana na idadi ya timu zitakazothibitisha kishiriki mashindano, timu zikiwa nyingi na idadi ya timu zinazotakiwa kuingia direct kwene makundi zinapungua.
sio ubora wa timu ndio una determine kuingia direct makundi, bali idadi ya timu shiriki ndio inapelekea timu kucheza playoff
Nadhani huyu ndio ka summarize vyema kabisa uzi wa mleta mada.
 
Sasa kuwapa kichwa kivipi? Kama wamefanya vizuri ni haki yao kujivunia sasa kwanini tunaonee wivu kwa kusema nawapa kichwa? Na sisi ndio tupambane tufike mbali klabu bingwa ili tutambe na rank.
Kwenye rank ambayo itakayotumika katika mashindano ya msimu unaoanza Simba ipo nafasi ya 9.
But mbona naona kwenye rank wapo nafasi ya 7 na teams zinazocheza Super League hazitashiriki hatua za mtoano?
 
Naomba kupewa ufafanuzi kuhusu kilichoandikwa!
Kilichomaanishwa ni kwamba baadhi ya timu kutoanzia hatua ya awali, itatokana na idadi ya timu zitakazoshiriki michuano ya klabu bingwa.
Jumla za timu zinazotakiwa kushiriki michuano ya klabu bingwa ni timu 64, kinachosababisha timu zingine zisianzie hatua ya awali ni idadi ya timu kutotimia 64.

Mfano ikitokea timu zipo 60 ni lazima timu 4 zisianzie hatua ya awali kwasababu kutoka 64 hadi 60 zimepelea timu 4.

Mfano ikitokea timu zinazoshiriki klabu bingwa zipo 50, ni lazima timu 14 hazitoanzia hatua ya awali kwasababu kutoka kwenye timu 64 hadi 50 zimepelea timu 14.

Ikitokea timu 64 zinashiriki klabu bingwa, basi timu zote zitaanzia hatua sawa sawa kwasababu hakuna upungufu wa timu. Uwingi na uchcche wa timu hutokana na idadi ya wanachama wa CAF watakaoshiriki michuano ya kimataifa ngazi ya vilabu
 
[emoji120][emoji120] Mkuu wewe ni mpenzi wa mpira, nashukuru kwa masahihisho hapo kwenye raundi ya timu 8. Ni vigezo vipi vitakavyotumika kuzipata timu za kucheza hiyo raundi ya timu 8?
maana yake zitacheza 8 ili kupata 4 ambazo zitaungana na 60 kutengeneza 64,.....
 
Simba ni ya 7, na juu yake kuna Zamalek na Raja ambazo hazishiriki champions League, hivyo kwa timu za CL Simba wanashika namba 5. Kuna uwezekano mkubwa Simba ikainzia round ya pili. Mwaka huu kila timu shiriki lazma iwe na timu ya kike, zipo timu zitashindwa na usishangae hata Yanga anaweza kuanzia round ya pili
mpk sasa ni ya 9 mkuu, ila ukiondoka berkane, raja, (labda na hao zamaleki maana last month naangalia ligi yao ilikua bado) basi simba atakua wa 6!
 
Back
Top Bottom