Njuka II
JF-Expert Member
- Feb 25, 2019
- 414
- 733
Habari,
Leo nimeona niwaelimishe ndugu zangu namna ya kujua idadi ya tofali zinazohitajika katika ujenzi wa nyumba.
Katika somo hili, tutatumia ramani ya chumba kidogo cha mita 3 kwa mita 3, chenye madirisha mawili (urefu mita 1.2, upana mita 1) na mlango mmoja (urefu mita 2.4, upana mita 0.9)
Kawaida vipimo vya tofali ni 0.450m urefu, 0.230m upana na 0.120/0.125/0.150m unene.
HATUA ZA UKADIRIAJI
1. Tafuta jumla ya urefu wa kuta zako ( Total Length of the wall)
Tukitumia mfano wa chumba chetu hapo juu, jumla ya urefu wa kuta zote (L) utakuwa
L= 3m+3m+3m+3m
L= 12m
2. Tafuta idadi ya tofali zitakazoweza kujenga mstari (kozi) mmoja wa tofali
Ili kuweza kujua idadi ya tofali zikakazoweza kujenga kozi moja ya tofali, chukua jibu ulilopata katika hatua ya kwanza kisha gawanya na urefu wa tofali moja ambao ni 0.45m
Idadi ya tofali kwa kila kozi, N = L÷0.450
N = 12m/0.45m
N = 26.6 = 27
Kila kozi (mstari) zitatumika tofali 27
3. Tafuta jumla ya tofali zote zitakazohitajika kujenga nyumba nzima.
Hapa sasa utaamua ujenge kozi ngapi, lakini kwa kawaida katika msingi watu wengi hupendelea kujenga kozi 8 mpaka 10 au na zaidi inategemea na eneo lilivyo au ramani yako ilivyo (sisi tutatumia kozi 8) na katika kuta za juu, watu wengi hupendelea kujenga kozi 12 mpaka 14 (sisi tutatumia kozi 12)
Jumla ya kozi zote itakuwa
Kozi 8 za msingi + Kozi 12 za kuta za juu = kozi 20
Jumla ya tofali zote, No. = kozi 20 × tofali 27
No. = tofali 540
4. Toa tofali za Madirisha na Milango
Hapa itabidi utafute eneo (surface area) la madirsha na milango
Jumla ya eneo la madirisha = 1.2m × 1.0m ×2 = 2.4m²
Jumla ya eneo la milango = 2.4m × 0.9m = 2.16m²
Jumla ya eneo lote = 4.56m²
Eneo la tofali moja likiwa limesimamishwa = 0.45m × 0.23m = 0.1035m²
Idadi ya tofali za kutoa katika madirsha na milango = 4.56m²/0.1035m² = 44
JUMLA YA TOFALI ZOTE, N = 540 - 44 = 496
Imeandikwa na Njuka II
Kwa hesabu mbali mbali zinazohusu ujenzi, tuwasiliane
ebusiness.excel@gmail.com
Sent using Jamii Forums mobile app