Fahamu namna ya ukadiriaji tofali katika ujenzi

Ili niweze kufanya makaridio inabidi niwe na ramani yenye vipimo, kama ni vyumba viwili tu vilivyoungana vyenye urefu na upana wa futi kumi kumi utahitaji uwe na mawe ya ujazo wa 4m³ . Kina cha msingi futi 2, upana futi 1
Asante sana
 
Mkuu unaweza kukutumia ramani ya nyumba yenye vipimo na ukafanya makadirio ya tofali!!??
 
Habari,

Leo nimeona niwaelimishe ndugu zangu namna ya kujua idadi ya tofali zinazohitajika katika ujenzi wa nyumba.
Katika somo hili, tutatumia ramani ya chumba kidogo cha mita 3 kwa mita 3, chenye madirisha mawili (urefu mita 1.2, upana mita 1) na mlango mmoja (urefu mita 2.4, upana mita 0.9)

Kawaida vipimo vya tofali ni 0.450m urefu, 0.230m upana na 0.120/0.125/0.150m unene.

HATUA ZA UKADIRIAJI
1. Tafuta jumla ya urefu wa kuta zako ( Total Length of the wall)
Tukitumia mfano wa chumba chetu hapo juu, jumla ya urefu wa kuta zote (L) utakuwa
L= 3m+3m+3m+3m
L= 12m

2. Tafuta idadi ya tofali zitakazoweza kujenga mstari (kozi) mmoja wa tofali
Ili kuweza kujua idadi ya tofali zikakazoweza kujenga kozi moja ya tofali, chukua jibu ulilopata katika hatua ya kwanza kisha gawanya na urefu wa tofali moja ambao ni 0.45m

Idadi ya tofali kwa kila kozi, N = L÷0.450
N = 12m/0.45m
N = 26.6 = 27
Kila kozi (mstari) zitatumika tofali 27

3. Tafuta jumla ya tofali zote zitakazohitajika kujenga nyumba nzima.

Hapa sasa utaamua ujenge kozi ngapi, lakini kwa kawaida katika msingi watu wengi hupendelea kujenga kozi 8 mpaka 10 au na zaidi inategemea na eneo lilivyo au ramani yako ilivyo (sisi tutatumia kozi 8) na katika kuta za juu, watu wengi hupendelea kujenga kozi 12 mpaka 14 (sisi tutatumia kozi 12)

Jumla ya kozi zote itakuwa
Kozi 8 za msingi + Kozi 12 za kuta za juu = kozi 20

Jumla ya tofali zote, No. = kozi 20 × tofali 27
No. = tofali 540

4. Toa tofali za Madirisha na Milango

Hapa itabidi utafute eneo (surface area) la madirsha na milango
Jumla ya eneo la madirisha = 1.2m × 1.0m ×2 = 2.4m²
Jumla ya eneo la milango = 2.4m × 0.9m = 2.16m²
Jumla ya eneo lote = 4.56m²

Eneo la tofali moja likiwa limesimamishwa = 0.45m × 0.23m = 0.1035m²

Idadi ya tofali za kutoa katika madirsha na milango = 4.56m²/0.1035m² = 44

JUMLA YA TOFALI ZOTE, N = 540 - 44 = 496

Imeandikwa na Njuka II
Kwa hesabu mbali mbali zinazohusu ujenzi, tuwasiliane
ebusiness.excel@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu vp kuhusu ukadiriaji wa bati?
 
mkuu vp kuhusu ukadiriaji wa bati?

Click hiyo link hapo juu then soma comment no 6 utapata idea, ila kama ni kwa hiki chumba cha uzi huu idadi ya bati ni Bati 12
 
Jioni tutaendelea na makadirio ya bati pamoja na mbao, subscribe ili upate notification ya new content
 
Habari,

Leo nimeona niwaelimishe ndugu zangu namna ya kujua idadi ya tofali zinazohitajika katika ujenzi wa nyumba.
Katika somo hili, tutatumia ramani ya chumba kidogo cha mita 3 kwa mita 3, chenye madirisha mawili (urefu mita 1.2, upana mita 1) na mlango mmoja (urefu mita 2.4, upana mita 0.9)

Kawaida vipimo vya tofali ni 0.450m urefu, 0.230m upana na 0.120/0.125/0.150m unene.

HATUA ZA UKADIRIAJI
1. Tafuta jumla ya urefu wa kuta zako ( Total Length of the wall)
Tukitumia mfano wa chumba chetu hapo juu, jumla ya urefu wa kuta zote (L) utakuwa
L= 3m+3m+3m+3m
L= 12m

2. Tafuta idadi ya tofali zitakazoweza kujenga mstari (kozi) mmoja wa tofali
Ili kuweza kujua idadi ya tofali zikakazoweza kujenga kozi moja ya tofali, chukua jibu ulilopata katika hatua ya kwanza kisha gawanya na urefu wa tofali moja ambao ni 0.45m

Idadi ya tofali kwa kila kozi, N = L÷0.450
N = 12m/0.45m
N = 26.6 = 27
Kila kozi (mstari) zitatumika tofali 27

3. Tafuta jumla ya tofali zote zitakazohitajika kujenga nyumba nzima.

Hapa sasa utaamua ujenge kozi ngapi, lakini kwa kawaida katika msingi watu wengi hupendelea kujenga kozi 8 mpaka 10 au na zaidi inategemea na eneo lilivyo au ramani yako ilivyo (sisi tutatumia kozi 8) na katika kuta za juu, watu wengi hupendelea kujenga kozi 12 mpaka 14 (sisi tutatumia kozi 12)

Jumla ya kozi zote itakuwa
Kozi 8 za msingi + Kozi 12 za kuta za juu = kozi 20

Jumla ya tofali zote, No. = kozi 20 × tofali 27
No. = tofali 540

4. Toa tofali za Madirisha na Milango

Hapa itabidi utafute eneo (surface area) la madirsha na milango
Jumla ya eneo la madirisha = 1.2m × 1.0m ×2 = 2.4m²
Jumla ya eneo la milango = 2.4m × 0.9m = 2.16m²
Jumla ya eneo lote = 4.56m²

Eneo la tofali moja likiwa limesimamishwa = 0.45m × 0.23m = 0.1035m²

Idadi ya tofali za kutoa katika madirsha na milango = 4.56m²/0.1035m² = 44

JUMLA YA TOFALI ZOTE, N = 540 - 44 = 496

Imeandikwa na Njuka II
Kwa hesabu mbali mbali zinazohusu ujenzi, tuwasiliane
ebusiness.excel@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
haya bana
 
Yah it makes sense japo sasa tiresome kwa nyumba kubwa yenye vipatition vingi
Na ndo maana QS wanapiga hela kwa vile wapo wanaoona hii ni kazi kubwa.

Kifupi unatafu jumla ya eneo la kuta zote kwenye nyumba then unagawa kwa eneo la tofali moja.

Au kwa njia nyepesi kama alivyofanya mtoa mada, jumlisha urefu wa kuta zote za nyumba, then uzidishe mara kimo cha kuta (assumption ni kwamba kuta zote zina kimo sawa au kimoja). Hapo utakuwa umepata jumla ya eneo la kuta za nyuma nzima, then gawa kwa eneo la tofali moja.
 
Habari,

Leo nimeona niwaelimishe ndugu zangu namna ya kujua idadi ya tofali zinazohitajika katika ujenzi wa nyumba.
Katika somo hili, tutatumia ramani ya chumba kidogo cha mita 3 kwa mita 3, chenye madirisha mawili (urefu mita 1.2, upana mita 1) na mlango mmoja (urefu mita 2.4, upana mita 0.9)

Kawaida vipimo vya tofali ni 0.450m urefu, 0.230m upana na 0.120/0.125/0.150m unene.

HATUA ZA UKADIRIAJI
1. Tafuta jumla ya urefu wa kuta zako ( Total Length of the wall)
Tukitumia mfano wa chumba chetu hapo juu, jumla ya urefu wa kuta zote (L) utakuwa
L= 3m+3m+3m+3m
L= 12m

2. Tafuta idadi ya tofali zitakazoweza kujenga mstari (kozi) mmoja wa tofali
Ili kuweza kujua idadi ya tofali zikakazoweza kujenga kozi moja ya tofali, chukua jibu ulilopata katika hatua ya kwanza kisha gawanya na urefu wa tofali moja ambao ni 0.45m

Idadi ya tofali kwa kila kozi, N = L÷0.450
N = 12m/0.45m
N = 26.6 = 27
Kila kozi (mstari) zitatumika tofali 27

3. Tafuta jumla ya tofali zote zitakazohitajika kujenga nyumba nzima.

Hapa sasa utaamua ujenge kozi ngapi, lakini kwa kawaida katika msingi watu wengi hupendelea kujenga kozi 8 mpaka 10 au na zaidi inategemea na eneo lilivyo au ramani yako ilivyo (sisi tutatumia kozi 8) na katika kuta za juu, watu wengi hupendelea kujenga kozi 12 mpaka 14 (sisi tutatumia kozi 12)

Jumla ya kozi zote itakuwa
Kozi 8 za msingi + Kozi 12 za kuta za juu = kozi 20

Jumla ya tofali zote, No. = kozi 20 × tofali 27
No. = tofali 540

4. Toa tofali za Madirisha na Milango

Hapa itabidi utafute eneo (surface area) la madirsha na milango
Jumla ya eneo la madirisha = 1.2m × 1.0m ×2 = 2.4m²
Jumla ya eneo la milango = 2.4m × 0.9m = 2.16m²
Jumla ya eneo lote = 4.56m²

Eneo la tofali moja likiwa limesimamishwa = 0.45m × 0.23m = 0.1035m²

Idadi ya tofali za kutoa katika madirsha na milango = 4.56m²/0.1035m² = 44

JUMLA YA TOFALI ZOTE, N = 540 - 44 = 496

Imeandikwa na Njuka II
Kwa hesabu mbali mbali zinazohusu ujenzi, tuwasiliane
ebusiness.excel@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo tofali unazipanga hivi hivi bila Mortar??
 
Back
Top Bottom