Fahamu nuksi, balaa na mikosi unayoweza kusababisha wewe mwenyewe bila kujua

Fahamu nuksi, balaa na mikosi unayoweza kusababisha wewe mwenyewe bila kujua

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Kufanya mapenzi chooni au baharini, sehemu hizi si nzuri kwa sababu zinamilikiwa na majini na nyumba za viumbe visivyoonekana. Ikitokea ukafanya mapenzi sehemu hizo wao huvuta picha kuwa unaleta dharau kwao ni sawa na mtu atoke huko na mgomvi wake kisha ajae apiganie ukumbini kwako, unaweza kuwafanya vyovyote utakavyo. Hapa pia najumusiha madhara ya zinaa.

Pale unapokuwa unashiriki tendo na MTU ambaye si mke wako ikiwa mtu huyo alirogwa au ana vifungo mwilini mwake au ana jini mahaba, haviwezi kukuacha salama ni lazima vikupate tu. Na ukirejea nyumbani unamletea mwenzio ile nuksi.

Vitu vyote vinavyohusika na chooni huwa ni miliki ya majini hawa majini wabaya ikiwa pamoja na ndoo za chooni na makopo sabuni hivi vtu kama utaviacha choon kutwa nzima alafu usiku ndo ulale navyo ndani kwako ndani ya wiki matokeo utayaona mfano utatembea na bahasha sana kuomba kazi lakini chanzo ni wewe mwenyewe kuchukua milki za watu kuweka ndani kwako.

Jambo jengine kuchukua vitu kwenye milki isyo ya kawaida. Nimeongelea chooni na baharini lakini hawa viumbe wana sehemu zao ambapo watu huenda kufanya maagano nao kwa mahitaji yao maalumu sehemu hizo ni njia, panda makaburini, maeneo ya miti mikubwa kama mibuyu nk. Sasa ukikuta kitu chochote kimewekwa au kutupwa katika hizo sehemu kiache kama kilivyo vinginenvyo utakuwa unautafuta ubaya ambao haujakusudiwa.

Ikiwa utakuta fedha sehemu hizo iwe noti au coins usiokote hilo ni kafara maagano tayari yashafanyika, ikiwa utakuta hirizi au tarasimu pia achana nayo usikanyage wala usiguse wapo waliopooza miili kuvimba miguu lakini uchawi hawakukusudiwa wao ila wameingia sehemu sizo. Ikiwa utakuta nyungu au vyungu usiviruke pita kando kabisa.

Kuna watu wanafanya mapenzi juu ya makaburi, wanakojoa au kujisaidia haja kubwa chini ya miti mikubwa ambayo ni makazi ya hawa mabwana wasioonekana. Wanaweza kukuvaa ndo ukasikia kakumbwa na jini kwenye mti mkubwa au wakakupa nuksi kila unachofanya hakifanikiwi.

Hata ukijisaidia kwenye maji
ambayo watu wanakunywa kwa makusudi Mungu hukulaani pia unapata nuksi kubwa tu haitoki mpaka visomo tena sio siku moja na utoe sadaka.

Usipende kuacha vyakula wazi usiku halafu asubuhi una mpango wa kukila tena si vizuri kiusalama kula vyakula vinavyolala wazi usiku kucha ,sababu wachawi wana kawaida wanapoingia katika nyumba ya mtu na kumaliza kufanya yao wanatia sumu za kichawi katika vyakula vinavyolala wazi.

Mambo muhimu yakuzingatia usipige mswaki kwa mkaa, usiokote shanga cheni, hirizi wala kitu chochote usichokifahamu na kukitumia. Ukimaliza kufanya mapenzi jisafishe hata kama ni gest.

Usichukue mke wala mume wa mtu, kile kiasi au raha unayoipata umedhulumu haki ya mwenzio Mungu huanza kukunyoosha hapahapa ikiwa hujafanya toba.
 
Mashetani yapo kila pahala na ni wengi mara 200 zaidi ya ujumla wetu wanadanu nao ndio wameanza kuikalia hii dunno, ndio maana ardhi yoyote ile kabla ya kufanya lolote lile tends to beg the unknown ancestry of that certain piece of land,ajabu ni kwamba duniani kote unknown ancenstry chakula Chao ni maziwa mtindi fresh, ulaya mpaka uchina na Marekani.
 
Hzi zote chenga tupu mkuu , cha msingi ni kuomba Mungu tuu akunusuru , kwenye Mapito yako duniani, mapito yaliyojaa taabu na kukosea kwingi , huwez fata hayo masharti yote uliyoyasema , kama sabuni tunaacha bafuni, anakuja mwingine kwenye familia anatumia na lyf linasonga , cha msingi watu waendelee kuchapa kazi , unapopitia magumu usiwe mwepesi wa kusema sjui mashetani sjui Mungu nafanya hv ,

(Mungu ni roho , na mashetani ni roho) means wapo kila sehemu , hat kwenye nyumba za Ibada , ukiona mambo yanaenda ndivyo sivyo , songa mbele mana hzo ni nyakat ngumu tuu na zinapita , na kila mwahadamu atazipitia Kwa style yake , fanyeni kazi Kwa bidii na malengo.

Bila kukata tamaa mambo yataenda vizuri tu, msala wa nuksi tushakuwa nao tangu Adam alipotenda dhambi the rest is about fighting.
 
mashetani yapo kila pahala na ni wengi mara 200 zaidi ya ujumla wetu wanadanu nao ndio wameanza kuikalia hii dunno, ndio maana ardhi yoyote ile kabla ya kufanya lolote lile tends to beg the unknown ancestry of that certain piece of land,ajabu ni kwamba duniani kote unknown ancenstry chakula Chao ni maziwa mtindi fresh, ulaya mpaka uchina na Marekani.
Mtindi tunajimwagia ama tunakunywa kujiswafi
 
Back
Top Bottom