Fahamu tunda aina ya Durian.

Fahamu tunda aina ya Durian.

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Miaka ya 90 Kijijini Sengerema tulikuwa na kawaida ya kwenda kuwasalimia na kuwapa hai wazee, tukifunga shule basi kesho yake asubuhi ni safari kwenda kijijini kusalimia, na kuishi kidogo na Babu na Bibi. Maisha ya kijiji yaikuwa mazuri sana kwa kiasi chake, hakuna umeme, na ikifika saa 2 kila mtoto kulala na asubuhi sana ukiamka ni kwenda kusaidia kukamua maziwa ng’ombe, kama sio kushika majani na kufukuza nzi kwenye mwili wa ng’ombe basi siku hiyo bahati itakuwa juu yako kuachiwa ukamue maziwa, lilikuwa jambo la kipekee sana kupeleka maziwa kwa babu, maziwa ambayo umekamua mwenyewe.
1727294940536.png

Ukiachana na shughuli ya kukamua maziwa, ilikuwa ni kawaida kumuona Bibi akipika ugali wa mhogo na kuchemsha samaki kisha watoto tunaitwa, na kuanza kula kisha tunafungulia ng’ombe na kuwapeleka machungani, hapo ndo tulikuwa tunapimwa uhodari wako katika kuongoza kundi la ng’ombe 30, mbuzi 10 na kondoo zipatazo 12.

Njia ambayo mnatakiwa kupita sio njia nyeupe, ni njia yenye utata sana, kila kona kuna mashamba ya watu tena yenye mazao, shughuli ya kuwaongoza mpaka kufika machungani sio shughuli nyepesi.

1727295009621.png

Ugali mliokula asubuhi na samaki basi wazee wanajua kuwa hamtosikia njaa mpaka ifikie jioni saa 11 mkiwa mnarudisha ng’ombe nyumbani. Mara kadhaa tulikuwa tunajikuta unapigika njaa moja takatifu sana, kiasi tukaanza kutafuta matunda porini huko, wakati ng’ombe wanaendelea kula nyasi sisi tupo na harakati za kutafuta matunda ya kupoza njaa zetu. Kuna nyakati tulikula mpaka matunda ya kiwano, haya matunda yalikuwa hayana urafiki na mtu ambaye hana ujasiri.

1727295079276.png

Leo nimekutana na hili tunda ambalo hata wanyama ukiwapatia basi ni sawa na kutangaza vita kwao, tunda lenye harufu kali sana, kisayansi linaitwa Durio zibethinus na ni tunda ambalo linapatikana kiasili maeneo ya Borneo pamoja na Sumatra.

1727295391029.png

Wakazi wa Indonesia pamoja na visiwa vya Sunda ambavyo vinapatikana Magharibi mwa Indonesia wamekuwa wakilipatia sifa sana tunda hili, wamelipatia jina kuwa ni King of Fruits, maeneo kama Bangka Belitung, visiwa vya Riau, Enggano, Mentawai, Nias pamoja na Simeulue wamekuwa ni wapenzi wakubwa wa tunda hili ambalo wengi tunalifahamu kwa jina la Durian.

Kumekuwa na video nyingi katika mitandao ya kijamii, Tiktok, Facebook, Instagram pamoja na Youtube wakionesha namna tunda hili ni tunda la ajabu na kipekee sana, video zkionesha watu wakifanya challenge ya kula tunda la Durian, tunda ambalo linatosha kumfanya mpaka paka kujenga bifu na wewe, harufu yake ni kali isiyo na mfano.

1727295213649.png

Durian ni tunda ambalo sio la kurukia juu juu kama unakula ndizi mbivu. Ngozi yake ya ndani inatosha kumfanya mtu kulitamani ila punde tu baada ya kusikia harufu basi utapata hali ya kichefuchefu na kutamani kutapika kabsa (waswahili wanasema kurudisha chenji).

Kuna iana zaidi ya 100 za tunda hili la Durian, huku aina maarufu zaidi zikiwa ni Durio graveolens, Durio kutejensis pamoja na Durio oxleyanus huku Durio testudinarius pamoja na Durio dulcis zikiwa ni aina ambazo zimeanza kupata umaarufu mkubwa hivi karibu ukiachilia mbali Durio zibethinus. 2017 Thailand alishika nambari moja kwa kuzalisha kiwango kikubwa cha matunda haya huku akiwa amezalisha tani zaidi ya laki saba kwa mwaka.

1727295105434.png

Ajabu ni kuwa tani laki nne zilikwenda kwa Uchina pekee. Malaysia pamoja Indonesia wanafuata kwa uzalishaji ambapo wanazalisha tani laki 265 kila mmoja kwa mwaka. Kwa upande wa Australia wao wanazalisha pia matunda ya Durian ila ni aina tofauti kwani wao wanazalisha Durian sita tofauti na ile aina kuu ya Durio zibethinus.

1727295283178.png

Ukifika Singapore hawaruhusu watu kubeba matunda ya Durian ndani ya usafiri wa umma kwa hofu ya kuwafanya watu kukereka na harufu kali ya Durian. Marehemu Alfred Russel Wallace aliwahi kusema ukweli na kuweka wazi kuwa kwa yeye binafsi Durian ni tunda lenye harufu mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani. Richard Sterling alienda mbali zaidi na kudai kuwa harufu ya Durian ni sawa na mchanganyiko wa harufu ya poop ya kitimoto, vitunguu vilivyooza pamoja na soksi zilizovunda.

1727295342382.png

Kwa sasa bei ya kilogramu moja ya Durian ni 15,422.40, Je Ukipewa tunda la Durian utakula? Na kama utakula je unaweza kula matunda mangapi?​
 
Miaka ya 90 Kijijini Sengerema tulikuwa na kawaida ya kwenda kuwasalimia na kuwapa hai wazee, tukifunga shule basi kesho yake asubuhi ni safari kwenda kijijini kusalimia, na kuishi kidogo na Babu na Bibi. Maisha ya kijiji yaikuwa mazuri sana kwa kiasi chake, hakuna umeme, na ikifika saa 2 kila mtoto kulala na asubuhi sana ukiamka ni kwenda kusaidia kukamua maziwa ng’ombe, kama sio kushika majani na kufukuza nzi kwenye mwili wa ng’ombe basi siku hiyo bahati itakuwa juu yako kuachiwa ukamue maziwa, lilikuwa jambo la kipekee sana kupeleka maziwa kwa babu, maziwa ambayo umekamua mwenyewe.
View attachment 3106741

Ukiachana na shughuli ya kukamua maziwa, ilikuwa ni kawaida kumuona Bibi akipika ugali wa mhogo na kuchemsha samaki kisha watoto tunaitwa, na kuanza kula kisha tunafungulia ng’ombe na kuwapeleka machungani, hapo ndo tulikuwa tunapimwa uhodari wako katika kuongoza kundi la ng’ombe 30, mbuzi 10 na kondoo zipatazo 12.

Njia ambayo mnatakiwa kupita sio njia nyeupe, ni njia yenye utata sana, kila kona kuna mashamba ya watu tena yenye mazao, shughuli ya kuwaongoza mpaka kufika machungani sio shughuli nyepesi.

View attachment 3106745

Ugali mliokula asubuhi na samaki basi wazee wanajua kuwa hamtosikia njaa mpaka ifikie jioni saa 11 mkiwa mnarudisha ng’ombe nyumbani. Mara kadhaa tulikuwa tunajikuta unapigika njaa moja takatifu sana, kiasi tukaanza kutafuta matunda porini huko, wakati ng’ombe wanaendelea kula nyasi sisi tupo na harakati za kutafuta matunda ya kupoza njaa zetu. Kuna nyakati tulikula mpaka matunda ya kiwano, haya matunda yalikuwa hayana urafiki na mtu ambaye hana ujasiri.

View attachment 3106750

Leo nimekutana na hili tunda ambalo hata wanyama ukiwapatia basi ni sawa na kutangaza vita kwao, tunda lenye harufu kali sana, kisayansi linaitwa Durio zibethinus na ni tunda ambalo linapatikana kiasili maeneo ya Borneo pamoja na Sumatra.

View attachment 3106764

Wakazi wa Indonesia pamoja na visiwa vya Sunda ambavyo vinapatikana Magharibi mwa Indonesia wamekuwa wakilipatia sifa sana tunda hili, wamelipatia jina kuwa ni King of Fruits, maeneo kama Bangka Belitung, visiwa vya Riau, Enggano, Mentawai, Nias pamoja na Simeulue wamekuwa ni wapenzi wakubwa wa tunda hili ambalo wengi tunalifahamu kwa jina la Durian.

Kumekuwa na video nyingi katika mitandao ya kijamii, Tiktok, Facebook, Instagram pamoja na Youtube wakionesha namna tunda hili ni tunda la ajabu na kipekee sana, video zkionesha watu wakifanya challenge ya kula tunda la Durian, tunda ambalo linatosha kumfanya mpaka paka kujenga bifu na wewe, harufu yake ni kali isiyo na mfano.

View attachment 3106759

Durian ni tunda ambalo sio la kurukia juu juu kama unakula ndizi mbivu. Ngozi yake ya ndani inatosha kumfanya mtu kulitamani ila punde tu baada ya kusikia harufu basi utapata hali ya kichefuchefu na kutamani kutapika kabsa (waswahili wanasema kurudisha chenji).

Kuna iana zaidi ya 100 za tunda hili la Durian, huku aina maarufu zaidi zikiwa ni Durio graveolens, Durio kutejensis pamoja na Durio oxleyanus huku Durio testudinarius pamoja na Durio dulcis zikiwa ni aina ambazo zimeanza kupata umaarufu mkubwa hivi karibu ukiachilia mbali Durio zibethinus. 2017 Thailand alishika nambari moja kwa kuzalisha kiwango kikubwa cha matunda haya huku akiwa amezalisha tani zaidi ya laki saba kwa mwaka.

View attachment 3106753

Ajabu ni kuwa tani laki nne zilikwenda kwa Uchina pekee. Malaysia pamoja Indonesia wanafuata kwa uzalishaji ambapo wanazalisha tani laki 265 kila mmoja kwa mwaka. Kwa upande wa Australia wao wanazalisha pia matunda ya Durian ila ni aina tofauti kwani wao wanazalisha Durian sita tofauti na ile aina kuu ya Durio zibethinus.

View attachment 3106762

Ukifika Singapore hawaruhusu watu kubeba matunda ya Durian ndani ya usafiri wa umma kwa hofu ya kuwafanya watu kukereka na harufu kali ya Durian. Marehemu Alfred Russel Wallace aliwahi kusema ukweli na kuweka wazi kuwa kwa yeye binafsi Durian ni tunda lenye harufu mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani. Richard Sterling alienda mbali zaidi na kudai kuwa harufu ya Durian ni sawa na mchanganyiko wa harufu ya poop ya kitimoto, vitunguu vilivyooza pamoja na soksi zilizovunda.

View attachment 3106763

Kwa sasa bei ya kilogramu moja ya Durian ni 15,422.40, Je Ukipewa tunda la Durian utakula? Na kama utakula je unaweza kula matunda mangapi?​
Duh....basi hilo litakuwa tunda- Mavi😂maana umesema linanuka sana.
 
Back
Top Bottom