Fahamu ujenzi wa SGR unavyoendelea

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
TANZANIA :- FAHAMU UJENZI WA SGR UNAVYOENDELEA

Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) ambapo ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam - Morogoro (km 300) umefikia asilimia 90.34 na kipande cha Morogoro - Makutupora (km 422) asilimia 57.57.

Aidha, tayari Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa kipande cha Mwanza - Isaka (km 341) wenye thamani ya shilingi trilioni 3.07; na kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa vipande vya Makutupora - Tabora (km 294) na Tabora - Isaka (km 133) na hapo baadaye kujenga njia ya Tabora - Kaliua - Kigoma (km 411) na Kaliua - Mpanda (km 207).

Katika kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021 jumla ya shilingi bilioni 596.8 zimetumika katika utekelezaji wa mradi huu alisema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
 
Umeelezea kifupi ila vizuri sana maeneo utakapopita huo mradi, serikali isikae kulia lia itafute pesa wakamilishe huo mradi, waanze kwa kupunguza posho za wabunge kwa siku, wabunge wakipiga kelele wapunguziwe na mishahara yao, kama bado haitatosha wauze angalau ndege tano za ATCL.
 
πŸ™πŸ™πŸ™
 
Serikali ya Kenya ilimtuma waziri wake wa mambo ya nje juzi kuja kuomba mkopo wa shilingi trillion tatu. Waziri wetu wa fedha alisema watawapa huo mkopo kwa masharti nafuu sana.

Wakati huo huo serikali ya Tanzania imetoa msaada wa shilingi bilioni Saba kwa saccos za wajasiriamali nchini Israel. Waziri mkuu wa Israel ameishukuru serikali ya Tanzania na kutuhakikishia atadumisha utafiki uliopo Kati ya serikali hizi mbili.
 
Duh hii ni kweli kabisa
 
Kweli kanda ya Kaskazini mwendazake alikuwa hatupendi. Yani miji ya kimkakati (strategic regions) kama Arusha, Tanga na Kilimanjaro aligoma kabisa kuweka hata robo kilometer ya SGR?

Hatari sana yule mzee kwa ukanda na ukabila.

Nateseka kutokea kanda maalum.
 
Hizi bange bora tu zihalalishwe ili tusivutie toilet πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Lakini mkuu si unakumbuka tren iliyo kua haitembei miaka mingi yeye kafanya itembee
 
Endapo mradi wa Bagamoyo ukijengwa, basi hiyo SGR itakuwa haina kazi tena, sivyo?
 
Lakini mkuu si unakumbuka tren iliyo kua haitembei miaka mingi yeye kafanya itembee
Sawa ila hiyo treni haina tija kwa maendeleo katika karne hii ya 21.

Haiwezekani treni itumie masaa zaidi ya 12 kwa umbali wa kilometer 600 wakati kuna treni zinazoweza kutumia masaa matatu tu umbali huo huo.

Hayo matreni ya zamani yangewekwa tu kwenye museums kama kivutio cha utalii.
 
Ngoja tusubiri upepo wa mama
 
Swala la kusubiri
Ndio ujue kuna watu ni wendawazimu nchi hii, hata Magufuli alishasema mbona, ni walevi na mataahira. Ujenge Bagamoyo halafu SGR inafanya kazi gani, itabeba nini toka Dar port? Au ndio tusema pesa zote za SGR ndio zimepotea bure?

Mwingine anaeshindwa kutumia akili zake vizuri anataka tuachane na Rufiji, ina maana pesa zote tulizotumia zimepotea bure?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…