FAHAMU UNAKABILIWA NA KUTOEPUKIKA

FAHAMU UNAKABILIWA NA KUTOEPUKIKA

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Code:
BARUA YA 53 KWA ULIMWENGU


Maisha kutokuwa na hakika na mabadiliko havipingani, kwakua vyote vipo ili kukamilisha jambo fulani ndani ya Maisha ya kiumbe hai, katika dhana ya kuwepo katika ulimwengu

Hii ndiyo hasa hujibu swali hili, kwanini maisha yanaleta mateso , mateso ya maisha ni somo ambalo unahitajika kujifunza na huondoka pale tu utakapo jifunza vyema somo hilo, lakini si kuwa mateso mengine hayatakuja, fahamu kujifunza katika maisha hakuwezi koma

Unakutana na mateso mara kwa mara kwa sababu ulimwengu unataka uwe na Ufahamu wa sehemu zako ambazo hazijaponywa ili uweze kuziponya katika mwanga wa ufahamu wako. Mateso hayataki kukupa faraja ya uongo, yanahitaji kukupa faraja ya kweli

Hali ya kutoupukika ipo ili kukufanya uharibu kila kitu ambacho umejiambatanisha nacho ndani yako, ndiyo maana hukupa mabadiliko.
Lazima ufahamu majaribio  na dhiki hukufanya utambue asili yako ya kweli, ambayo ni ufahamu safi katika upana wake

Unapo kabiliana na kutoepukika kwa mambo, ni kupewa ujasiri , ujasiri upo ili kumfahamisha mwanadamu yapo mazingira ambayo anastahili kung'ang'ania magumu na kukabiliana nayo na hata apoteze nishati ya kukatishwa tamaa

Unapo kabiliana na kutoepukika kwa mambo ni kupewa hali ya matumaini, yaani  binadamu lazima daima akabiliwe na ukosefu wa usalama na kutokuwa na uhakika wa mara kwa mara,ili ajenge uzio wa matumaini na ajifunze katika namna ya kujenga

Unapo kabiliana na kutoepukika kwa mambo ni kupewa hali ya Imani, Inahitajika akili ya mwanadamu ijikute katika hali hiyo ya kutatanisha ambapo inajua kidogo kuliko inavyoweza kuamini.

Unapokabiliana na kutoepukika kwa mambo ni kupewa hali ya Upendo,hapa mwanadamu anafundishwa jinsi ya kupenda hatima , hapa ni lazima mwanadamu akue akitambua kuwa kuna aina ya mateso ili kuondoka na kuisha ni lazima ajifunze kuyapenda kwanza,si kuyapenda kwa uongo ni katika ukweli ili aingize hali ya kutosha ndani yake

Katika ulimwengu wote, kila kitengo kinachukuliwa kuwa sehemu ya jumla.   Kuishi kwa sehemu hiyo kunategemea ushirikiano na mpango na kusudi la ujumla, hamu ya moyo wote na nia kamili ya kufanya

 Ulimwengu pekee wa mageuzi bila makosa, utakuwa na hukumu zisizo na busara, utakuwa ulimwengu usio na akili huru.   Katika Ulimwengu mwanadamu anayeendelea kubadilika lazima awe na makosa ikiwa anataka kuwa huru, ikiwa anahitajika kujifahamu ni lazima apitie mateso ajifunze kitu

Inakuwa ni makosa pale mwanadamu anapofikiri mateso yapo ili kumuhukumu,hiyo ni hukumu potofu.Basi ni lazima mwanadamu aishi katika ulimwengu ambamo njia mbadala ya maumivu na uwezekano wa kuteseka ni mambo yanayowezekana na kutokea kila wakati kama somo, yaulize maumivu umekuja kunifundisha nini? yauliza mahangaiko umekuja kunipa habari gani ya udhibiti?

KARIBU KATIKA GROUP LA" THE STOIC COMMUNITY "

TUCHAMBUE VITABU VYA FALSAFA NA UKUAJI BINAFSI

TUSOME MAKALA ZA WANAFALSAFA WA USTOA

TUSOME BARUA 365 KWA ULIMWENGU

TUJIFUNZE KUHUSU FALSAFA YA USTOA

KWASASA TUNACHAMBUA KITABU C
 
Back
Top Bottom