Swali zuri mkuu
1.Kwa treasury bills minimum ni 500000/= kwa mafungu ya 10000/= mfano unaweza wekeza 550000/= na sio 555000/=
2.Kwa treasury bond minimum ni 1m kwa mafungu ya 100000/= mfano 1500000/= na sio 1550000/=
Kuwekeza kwenye hz dhamana za serikali kuna faida zifuatazo.
1.Serikali haitegemei kukiuka mategemeo ya wadai wake wakati wa malipo( hapa hata tuingie kwenye vita pesa yako utalipwa tofauti na commercial banks ni 50/50).
2.Dhamana za serikali zinahamishika hapa unaweza kuziuza DSE kabla ya mda wake kuiva
3.Dhamana za serikali zinaweza kutolewa kama dhamana kwa ajili ya mkopo(yaani ukishawekeza unaweza kupata mkopo bank yyte kulingana na pesa ulizowekeza,,kama umegundua ktu hapa unawekeza kwenye dhamana then unaenda kuchukua mkopo unapiga biashara unatengeneza faida mara mbili wakati bank unawalipa mdomdo mangi)
4.Faida inayopatikana katika uwekezaji wa dhamana inaridhisha) hakuna commercial bank yyte utakayowekeza upate interest kama za BOT na wengi ni matapeli maana walishanifanyia umafia that's why nimewekeza huku
Karibu.
Sent using
Jamii Forums mobile app