Fahamu utajiri wa kudumu uliojificha kwenye zao la Parachichi Mkoani Njombe

Mna mpango gani kwa sehemu zingine kutanua masoko ,maana hiyo ardhi ya Njombe kununua ni sawa!Ikiisha je?
 
Hiyo mikoa mingine mna mpango gani mkuu?!
 


habari naweza kupata namba zenu za simu?
 
Agriworth nimelima kama ekari 8 Rungwe ambazo nimezipanda mwaka huu, January hii, je mnakuja kununua matunda huku pia!? Yatakapokomaa!?
 
Msalimie Mr.Lugenge mkuu hapo mfiriga.
 
Kweli parachichi ni zao linalo ibukia kuweza kutajirisha wakulima.
Lakini sisi tulio jitosa huko hofu yetu pekee ni maamuzi ya serikali huko mbeleni.
Tumeona mifano ya mazao ya korosho na kahawa.

Ukisha sikia serikali ina sema zao fulani ni zao la mkakati, omba Mungu hiyo mikakati isiathiri bei na kuharibu mfumo ulio anza kujejinga wenyewe.

Wafanya maamuzi angalieni. Watu tunawekeza huku vya kutosha halafu kesho mnafanya maamuzi yanayopelekea au bei kushuka au wanunuzi kupotea.

Hatuna cha kuwafanya lakini tutasononeka.
 
Nikweli...
Ila we lima tu...
 
Thanks
 
Agriworth nimelima kama ekari 8 Rungwe ambazo nimezipanda mwaka huu, January hii, je mnakuja kununua matunda huku pia!? Yatakapokomaa!?
Jiunge na UWAMARU AMCOS ambayo ni Ushirika wa Wakulima wa Maparachichi Rungwe hawa wamepata mnunuzi ambaye ni Avo Africa wapo Makambako wana kiwanda cha mafuta na pia wanasafirisha nje ya nchi. Kwa maelezo zaidi njoo dm
 
@agriworthtz Huduma yenu bado inaendelea mkoani njombe ama mmesogeza na mikoa mingine?

Halafu kwa kilimo cha parachichi mtaji wake ni shs ngap na masoko yake mengine ni yapi?
 
Na shida na mtu aliye njombe anafanya kilimo cha Parachichi...kindly DM me
 
Hili binafsi sidhani kama litatokea. Nalima avocado pia ila sidhani kama mambo yalotokea kwenye Kahawa na Korosho yatajirudia huku...nadhani haitatokea maana ni mwaka zaidi ya wa 10 sasa market trends za Hass avocado hazijateteleka sana...sanasana bei imepanda zaidi wakulima wanafaidi.
 
Jidanganye; china imefanya majaribio ya hass na ikafanya vizuri hivyo wameamua kulima mahekari lukuki a, vayo inasemekana in time zitaathiri soko la wakulima wa Africa
 
Nachukizwa sana na dhuluma inayofanywa kwa wakulima mkoani Njombe
Shida iko hiviiiii
Kuna makampuni sijui mashirika mengiii yamejitokeza kama uyoga.... kikubwa wanachofanya vikundi hivi sijui mashirika hayo ni kuwadanganya wakulima kuwaibia pasipo wao kujua
Semina nyiiingi mwisho wa semina mnauziwa sijui mbolea (mtaambiwa imetoka Marekani- mmarekanj analima parachichi wapi kama sio kuwadanganya wakulima!)

Kuna uchafu unaitwa vibinjo kazi yao kuwatafutia wanunuzi (how???) kwa nini watafutiwe wanunuzi? Halafu bei anapanga mnunuzi (utaona kabisa hii dhuluma) halafu mnunuzi ananunua matunda anayotaka yeye mengine anayaacha yaozee shambani

Ninyi ndio mlipashwa kuwatetea wakulima hawa sio kuwauzia watu maeneo na kuwapa sijui elekezi la zao la parachichi....



Waziri husika anapashwa kufuatilia Kilimo mikoa mikuu inayozalisha mazao ya chakula na biashara.....
 
Jidanganye; china imefanya majaribio ya hass na ikafanya vizuri hivyo wameamua kulima mahekari lukuki a, vayo inasemekana in time zitaathiri soko la wakulima wa Africa
Msemakweli Ni Mpenzi Wa Mungu
 

UNAWEZA KUYATAJA HAYO MASHIRIKA? NINACHOFAHAMU MIMI, PARACHICHI INAPANDWA KWA MBOJI/MBOLEA YA MIFUGO, DAP, NPK, TSP AU MINJINGU-MOHP. HAKUNA MBOLEA YA AJABU. HATA DAWA WAKULIMA WANASHAURIWA WATUMIE DAWA YA ASILI MFANO PILIPILI.
(Je hujui kuwa Marekani wanalima Parachichi?)

Kuna uchafu unaitwa vibinjo kazi yao kuwatafutia wanunuzi (how???) kwa nini watafutiwe wanunuzi? Halafu bei anapanga mnunuzi (utaona kabisa hii dhuluma) halafu mnunuzi ananunua matunda anayotaka yeye mengine anayaacha yaozee shambani[/QUOTE]
SIJUI KWA NJOMBE, ILA KWA TUKUYU WANANUNUA KILA KITU KWA MKATABA, KUNA USHINDANI.

Ninyi ndio mlipashwa kuwatetea wakulima hawa sio kuwauzia watu maeneo na kuwapa sijui elekezi la zao la parachichi....[/QUOTE]

(Ni vizuri kama wakulima wakiwa kwenye umoja wa Ushirika wanaweza kujadiliana Bei na kutafuta elimu zaidi).


Waziri husika anapashwa kufuatilia Kilimo mikoa mikuu inayozalisha mazao ya chakula na biashara.....[/QUOTE]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…