Kwenye bandiko lako kuu, ukubali umetoa tafsiri isiyo sahihi kitaaluma (uchumi na usimamizi fedha) ila inakidhi uelewa wa mtu wa kawaida kuhusu mapato na matumizi.
Kitaaluma maneno hayo yanatumika katika mizania ya kifedha (Balance Sheet) ambayo inatamka kwamba:
Assets = Equity + Liabilities
Assets ni mali yote, inayobadilika (current asset) km pesa taslimu, na isiyobadilika (fixed asset) km nyumba, ambayo anamiliki mtu/ kampuni nk. Mali hii imepatika aidha kutokana na mtaji (equity) ya mmiliki au madeni (liabilities).
Hivyo utajiri (networthness) wa mtu ni mali aliyokuwa nayo na siyo biashara anayoifanya yenye faida au kuwa na ukwasi wa kifedha.