Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Ndugu uliyeanzisha uzi huu nataka nianze kutoa pongezi za dhati kwa uzi huu ulioanzisha ambao naamini utakuwa na manufaa makubwa kwa watu wengi.
Niko katika tafakari za kuanzisha michakato ya ujenzi, maswali yangu:-
1. Ni kiwanja chenye ukubwa gani kinafaa kwa ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu nyumba ya kawaida kabisa ya kitanzania.
2. Faida za ujenzi wa interlocking bricks (Dodoma).
Ninabaki nikiwa na moyo wa Shukrani nikisubiria majibu.
 
Minimum angalau kiwe na 400sqm ili ubakiwe na space ya kufanya vitu vingine.
Angalau kiwe na sqm 400 , ili ubakiwe na space ya kufanya mambo mengine.

Interlocking sijaona faida yake mpaka Leo. Nawashauri wateja wangu kutumia block.

Pia ujenzi wa Dodoma una gharama kulinganisha na Dsm
 
Watu wengi huwa wagumu kukubali mabadiliko, teknologia za ujenzi zimebadilika ila wengi bado tumebaki nyuma. Kuna ujenzi wa kutumia panels, interlocks bricks n.k

Faida za interlock bricks;
1. Matofari yanatumia kiasi kidogo cha saruji katika utengenezaji wake. Mfano mfuko 1 wa saruji unatoa tofari 75 hadi 90.
Pia katika kujenga inatumia kiasi kidogo cha saruji kutokana na mfumo wa kufungamana (locks) hivyo kusaidia kuokoa gharama za matumizi ya saruji na mchanga.

2. Ujenzi wa namna hii hauna ulazima wa kupiga plasta hivyo kuokoa gharama za saruji, mchanga, gharama ya fundi na gharama zinazohusiana na plasta kama skimming, white Cement, Gypsum powder, rangi n.k

3. Faida nyingine utapata nyumba yenye muonekano mzuri isiyokua na joto kali ndani.

Kwa ujumla ujenzi huu upunguza gharama za ujenzi kwa 30% hadi 40%.

 
Sitaki kuharibu biashara za watu lkn msimamo wangu kwa client ni kuwa ni bora kutumia block. Hata wewe najua unafahamu ni nini kinatokea baada ya mfupi kupita kwenye hayo majengo.
 
Mungu akubariki. Ni mwl mwema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…