KIMOMWEMOTORS
JF-Expert Member
- May 17, 2018
- 358
- 675
Mwingine kaulizia iwapo anaweza kuchukua Brevis au la.
Kwa mtu ambaye hafaham chochote kuhusu gari hii akiniomba ushauri nitamuelekeza yafuatayo na kumpa wazo mbadala la gari ambazo zinaendana na gari hii kama ifuatavyo:
Brevis ina sifa ya kuwa gari nzuri ya Saloon yenye uwezo wa safari ndefu ambayo ilitengenezwa mwanzo mwa mwaka 2000 kabla hayajatoka matoleo mengine yanayofanana na hii kwenye injini kama Mark X na baadae Crown.
Ni gari yenye Cc 2500 na ambayo kama utaitunza vizuri kwa kuatisha service zake basi itakutunza pia.
Changamoto ya gari hii kubwa ninkwenye mafuta, mfumo wake wa injini sio rafiki kwenye kubana matumizi makubwa ya mafuta haswa kama unaishi mkoa wenye foleni kubwa, lakini pia unaponunua gari hii kwa gharama kubwa leo utakapohitaji kuiuza baada ya muda fulani thamani yake huwa inaporomoka sana kwa kuwa watu wengi kwa sasa hawapendi gari zenye matumizi makubwa ya mafuta kama Brevis. Iwapo huwazi kuja kuiuza basi unaweza kuinunua na itakufaa zaidi kwenye safari ndefu, ila iwapo utafikiria kuiuza vizuri ujiandae kisaikolojia kuuza kwa bei ya chini sana ikilinganishwa na aina nyingine za magari.
Iwapo unataka gari ambayo inafanania ndani na hii na ambayo pia inaweza safari vizuri lakini hutumia mafuta ya wastani basi nitakushauri Mark 2 GX 110 yenye CC 2000. Lakini pia kama utata kutunza zaidi thamani ya pesa yako na kuuza gari hiyo kwa haraka na bei nzuri basi nitakushauri upate Premio ya CC 1800 injini ya 1ZZ ambayo ni Vvti.
Hizi gari zote yaani Brevis, Mark 2 na Premio zina gharama inayoshabihiana unapoziagiza. Kwa wastani zote huanzia 12.3m ingawa Premio muda mwingine hushuka zaidi.