Offshore Seamen
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 5,489
- 14,091
Jettisoning ni kitendo cha hiari cha kutupa mizigo baharini wakati meli inaendelea na safari ili kutoathiri usalama wa meli na wafanyakazi endapo kuna hali mbaya baharini na kuweka sasa stability ya meli.
Mizigo inayotupwa baharini kutokana na hiki kitendo inaitwa Jettisan.
SABABU ZA KUFANYA JETTISON
Sababu kuu ni kulinda usalama wa meli na wafanyakazi kwa kuipunguzia meli mizigo na kuifanya ipate stability.Meli nyingi zinazobeba mizigo sehemu ya juu ya meli(Deck Cargo) ndio mizigo yake inatupwa.Meli ambazo hubeba magogo ya miti,mbao,vyuma vikubwa vya ujenzi na mizigo mingine ambayo huwekwa sehemu ya juu ya meli(deck floor).
Meli za magari,mafuta,kontena na shehena(Bulk Carrier) hizi huwa hawatupi mizigo sababu zimejengewa matenki ya ziada kwa ajili ya kuzipa stability. Kontena kuangua baharini ni bahati mbaya baada ya meli kupigwa na dhoruba Kali na kupelekea lock za kushika kontena kuachia.
ULIPAJI WA MIZIGO ILIYOTUPWA
Mizigo yote itakayotupwa kwa hiari(Jettisan) wahusika watalipwa kupitia sheria ya General Average Law. General Average Law inataka kila mwenye mizigo na mmliki wa meli kuchangia asilimia kadhaa ili kufidia kiwango cha hasara ya mizigo uliotupwa baharini. Hivyo mtu mwenye mizigo hapaswi kuofia kuhusu mzigo wake.
VIGEZO VYA KUFANYA ULIPWE FIDIA YA MZIGO
Ili uweze kulipwa fidia ya mzigo wako kupitia sheria ya General Average Law ni lazima ajue kuwa mzigo wake ulipakiwa sehemu ya juu na sheria za kampuni ya hiyo meli iliyobeba mzigo wake inakubali kulipa fidia ya hasara ya mizigo itakayotupwa baharini (Jettison).
Deck Cargo- Ni ile mzigo ambao huwekwa sehemu ya juu ya meli kutokana kutoweza kuwekwa ndani, mfano mbao, matanki ya ujenzi na vifaa vikubwa vya ujenzi.