Fahamu zaidi kuhusu madini ya Tanzanite

Fahamu zaidi kuhusu madini ya Tanzanite

Adam k.m

Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
21
Reaction score
4
124919_f520.jpg

Tanzanite ni madini yenye mchanganyiko wa rangi ya bluu na zambarau. Madini haya ni ya kipekee kwa Tanzania kwani hayana chanzo chochote duniani isispokuwa kile cha Mererani mjini Arusha, Tanzania.

Madini haya yaligundulika mwaka 1967 lakini yakajipatia jina hilo mwaka 1969 kutoka kwa Henry Platt, makamu wa rais katika kampuni ya Tiffany and Co. Juhudi za kutafuta soko la madini haya lilipa jina la Tanzanite umaarufu ndani ya mda mfupi hadi kutumika katika soko la madini kidunia.

Kinachovutia zaidi kwenye madini haya ni uzuri wa rangi yake. Yapo madini haya yenye rangi ya bluu hadi yalio na rangi ya zambarau. Rangi yake hubadilika badilika kadiri unavyolitazama kupitia pembe tofauti.



blogger-image--1359849879.jpg



Tanzanite hutumika kama urembo katika bangili, cheni na hereni. Halitumiki sana kwenye pete kutokana na kua na ugumu mdogo pamoja na uwezo wa kuchubuka kirahisi.

Bei ya Tanzanite kwa sasa inaanzia tsh.3,000,000 hadi 10,000,000 kwa kila gram.
 
hayo madini yameshaisha , yamebaki mashimo tu
 

Kuna siku utabisha hata visivyobishika! Tanzanite si mimea kuwa itaota tena na si wanyama kuwa watazaana tena !!! Once is gone is gone forever zitabaki story na mashimo ya kufuga panyabuku na panyaroad waliopokwa utajiri wao kwa tamaa ya wachache1407421719865.jpg1407421784241.jpg
 
Mkuu hii bei ya gram 3,000,000 mpka 10m ni ya kuuzia hapa tz au nje ya nchi
 
Nashangaa yanakotoka Tanzanite watu ni masikin lakin Tanzanite ni biashara inayowatajirisha watu marekani,south africa,india etc

Umesahau Kenya.Nasikia walisha wahi kupewa zawadi ya ndege kutokana na biashara hiyo
 
Back
Top Bottom