Fahamu zaidi kuhusu Vanguard na Rav 4 model ya 2009- 2014

Inaanzia hapo kwenye 23m na mda mwingine inaweza kuanzia hata kwenye 22.5. Sisi hatuweki cha juu bali tunapiga hesabu zote hizi kwa uwazi kabisa ili mtanzania apate kilicho bora kwa gharama nafuu na wakati huo huo akituwezesha kukua zaidi
MKUU,

SASA KAMA HAMPIGI CHA JUU,
FAIDA YENU MNAIPATAJE?

KWA MFANO GHARAMA YA KUAGIZA GARI KWA MFANO Allion MPAKA INAONGIA ROAD NI 10 M.

NA NYINYI NA MNAILETA KWA MTEJA KWA 10 M. HIYOHIYO BILA ONGEZEKO LOLOTE AU INAKUWAJE HAPO?

NIPE MWONGOZO MKUU,
ILI HUU MWAKA UKIPINDUKA NIJE NIJILIPUE NA BABYWALKER MOJA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toyota ni moja ya Makampuni makubwa zaidi ya uzalishaji magari Duniani na wamejikita zaidi katika utengenezaji wa magari yenye uwezo mkubwa na imara lakini bila kuyasahau ya wastani yenye uwezo wa kawaida na ubora wa.

Kwa ufupi, zifuatazo ni baadhi ya tofauti za Magari haya mawili yaani Toyota Vanguard na Rav 4 model za kuanzia 2009 mpaka 2014

1. Injini

Ni ngumu kuzitofautisha injini hizi mbili kwa kua zote zina mwendo na uwezo mzuri. Rav 4 ina injini ya 2.5L ambayo ni Cylinder/Piston 4. Gari hiyo ina injini yenye Cc 2400 ikiwa na 4WD au AWD.

Wakati Vanguard ina injini za Cc 2400 mpaka 3500 na unaweza kuitumia kwa 4WD na 2WD

2. Magumizi ya Mafuta

Hakuna tofauti kubwa kwenye matumizi ya mafuta haswa kwa hizi za Cc 2400 kwa Cc 2400 kwa kua zote huenda kati ya kilomita 12 mpaka 13 kwa lita moja ya Petrol

3. Idadi ya Viti

Idadi ya viti ni moja ya vitu vya kuzingatia unapofikiria kuchagua gari za muundo huu. Rav 4 ina viti 5 wakati vanguard ina viti 7 jambo linalopelekea nafasi ya mizigo kua ndogo huku nafasi ya mizigo katika Rav 4 ikiwa ni kubwa zaidi

4. Uwezo wa Gari

Vanguard inaonekana kua Imara na yenye nguvu zaidi kuliko Rav 4. Nguvu ya Rav 4 kwa kawaida haizidi HP 170 wakati ya Vanguard ni mpaka HP 270 jambo linaloifanya itawale zaidi barabarani

5. Gharama za Uagizaji

Uzoefu katika hizi gari mbili unaonesha kua zinatofautiana kati ya milioni 1 mpaka milioni 3 kutegemea na mwaka kwa kua zina ushuru tofauti. Mara nyingi Rav 4 huagizwa kwa jumla ya gharama za Tsh 23.5 wakati Vanguard huanzia 25.5m

Hitimisho

Kwa kua sasa unajua machache kuhusu gari hizi mbili yaani Rav 4 ya 2009 mpaka 2014 na Vanguard, na kwa kua zote zinaonekana kua sawa kwenye baadhi ya vitu huku zikitofautiana kwenye mambo machache, sasa kazi ni kwako kuamua kuchagua aina ya gari unayoipenda zaidi kulingana na maelezo hayo.

Imtotolewa na Uongozi wa Kimomwe Motors (T) Ltd waagizaji wa Magari
0746267740

View attachment 1286696View attachment 1286697

Mbona hamjaisema rave yenye 1AZ cc 2000 ?? Rav za mwaka huo zinakuja na engine zaidi ya tano hadi diesel ziko we umekalia kwenye ile ya cc 2400
 
Kluger ni maboresho ya Harrier Old Model boss. Zote ni gari nzuri kwenye upande wa uimara na zinakaribiana kwa sehemu kubwa hata gharama za matengenezo na vipuri. Zote ni nzuri sana kwenye Rough Road ingawa kwenye upande wa stability iwapo kwenye mwendo Kluger inaonekana kuboreshwa zaidi haswa kwenye uimara kwa kua huanza kua nyepesi ikifika 140 speed wakati Harrier ikiwa kwenye 120 speed huanza kua nyepesi kidogo

Kluger ni larger alternative ya RAV4 na sio maboresho ya harrier haviusiani kabisa.mmm
 
Naomba unisaidie uchaguzi mzuri kati ya subaru forester xt na subaru isiyo na turbo, suzuki grand vitara na nissani xtrail new model , naomba chaguo hapo lipi ni zuri hasa kwa mtazamo wako na uzoefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kluger ni larger alternative ya RAV4 na sio maboresho ya harrier haviusiani kabisa.mmm

Kluge ni hurrier wewe acha ubishi soma Wikipedia

Rav4 ni vanguard in other hand soma uelewe brother

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Toyota ni moja ya Makampuni makubwa zaidi ya uzalishaji magari Duniani na wamejikita zaidi katika utengenezaji wa magari yenye uwezo mkubwa na imara lakini bila kuyasahau ya wastani yenye uwezo wa kawaida na ubora wa.

Kwa ufupi, zifuatazo ni baadhi ya tofauti za Magari haya mawili yaani Toyota Vanguard na Rav 4 model za kuanzia 2009 mpaka 2014

1. Injini

Ni ngumu kuzitofautisha injini hizi mbili kwa kua zote zina mwendo na uwezo mzuri. Rav 4 ina injini ya 2.5L ambayo ni Cylinder/Piston 4. Gari hiyo ina injini yenye Cc 2400 ikiwa na 4WD au AWD.

Wakati Vanguard ina injini za Cc 2400 mpaka 3500 na unaweza kuitumia kwa 4WD na 2WD

2. Magumizi ya Mafuta

Hakuna tofauti kubwa kwenye matumizi ya mafuta haswa kwa hizi za Cc 2400 kwa Cc 2400 kwa kua zote huenda kati ya kilomita 12 mpaka 13 kwa lita moja ya Petrol

3. Idadi ya Viti

Idadi ya viti ni moja ya vitu vya kuzingatia unapofikiria kuchagua gari za muundo huu. Rav 4 ina viti 5 wakati vanguard ina viti 7 jambo linalopelekea nafasi ya mizigo kua ndogo huku nafasi ya mizigo katika Rav 4 ikiwa ni kubwa zaidi

4. Uwezo wa Gari

Vanguard inaonekana kua Imara na yenye nguvu zaidi kuliko Rav 4. Nguvu ya Rav 4 kwa kawaida haizidi HP 170 wakati ya Vanguard ni mpaka HP 270 jambo linaloifanya itawale zaidi barabarani

5. Gharama za Uagizaji

Uzoefu katika hizi gari mbili unaonesha kua zinatofautiana kati ya milioni 1 mpaka milioni 3 kutegemea na mwaka kwa kua zina ushuru tofauti. Mara nyingi Rav 4 huagizwa kwa jumla ya gharama za Tsh 23.5 wakati Vanguard huanzia 25.5m

Hitimisho

Kwa kua sasa unajua machache kuhusu gari hizi mbili yaani Rav 4 ya 2009 mpaka 2014 na Vanguard, na kwa kua zote zinaonekana kua sawa kwenye baadhi ya vitu huku zikitofautiana kwenye mambo machache, sasa kazi ni kwako kuamua kuchagua aina ya gari unayoipenda zaidi kulingana na maelezo hayo.
View attachment 1286696View attachment 1286697
Vanguard beininacheza 35-40m TZS
 
Naomba pia mwenye knowledge kuhusu tofauti Kati ya harrier na kluger atudadavulie hapa Kama huyu ndg yetu alivyofanya
 
Back
Top Bottom