Fahari wawili wakipambana ziumiazo ni nyika

Fahari wawili wakipambana ziumiazo ni nyika

WARIOBA

New Member
Joined
Feb 20, 2013
Posts
1
Reaction score
0
Fahari wawili SERIKALI vs WALIMU

Hivi karibuni tumeshudia malumbano ya kimasilahi baina ya walimu na serikali na hatimaye kupelekana mahakamani na serikali kupinga kisheria walimu kuendelea na mgomo, walimu wakakubali kuacha mgomo wa wazi na kuendelea na mgomo baridi tunaoushuhudia leo kupitia matokeo mbalimbali. waliofaulu kutoka primary kwenda Secondary walichaguliwa hadi wa max 70, serikali ilikubaliana nalo na hata matokeo haya ya secondary wenye credit 2 ambazo zinatengeneza kombi kwa kuungwa na D moja wachaguliwe waendelee na kidato cha tano. hakuna ujanja zaidi bali kukubali kusonga hivyo hivyo huku tukizidi kutengeneza WATAWALIWA NA WATAWALA.

Kuna kila sababu ya serikali kukaa na walimu tena kutafuta suluhu ya changamoto hii ili kuwanusuru watoto wetu.

TUTAWAPELEKA WAPI, KILA MTAA VILIO, HURUMU SIMANZI ZIMETAWALA.

SALUMU
BUSEGA
SIMIYU
 
Ni kweli matokeo haya yanazidi kuongeza gap kati ya watawala na watawaliwa au walionacho na wasiokuwa nacho. Ukiangalia shule nyingi ni za kata na zipo vijijini. Tangu awali ipo gap kati ya mjini na vijijini lakini ilikuwa inapunguzwa na mambo kama haya ya ufaulu mzuri katika shule za vijijini. Panazidi kuwepo ugumu kwa mtu anayeishi kijijini kuwa na watoto watakaoendelea na masomo ya juu na mbaya zaidi watoto hao ni semi illiterate watakao kuwa mzigo kwenye vijiji na taifa kwa jumla
 
Back
Top Bottom