Mwanamke anatakiwa amsaidie mwanaume wake kuona na kupata fahari kwa kuwa na mkewe huyo, familia, nyumbani n.k
1.Jua kupendeza badala ya kuchekesha. Mfanye mwanaume wako apende na afurahie kuongozana/kuonekana na wewe bila woga wala aibu. Sio mtu tumbo ni kubwa kuliko kiwiliwili cha chini lakini bado unavaa nguo za kubana na kuchora mpaka wanaokuangalia wanakuonea aibu, mumeo ataona nini? Uso umepambwa kama xmass tree nani aonekane na wewe achekwe?
mwanaume nae ashiriki katika kumpendezesha mkewe, kutokupendeza kwa mke isiwe sababu ya kushindwa kuongozana nae. swala la kuvaa na kufurahia muonekano wa miili ni jukumu la wote. kama mkeo katoka kitambi na kimeshindikana kurudi, accept matokeo tu, sio kuona aibu kuongozana nae. unamuonea nani aibu sasa wakati ndio mkeo huyo?
2.Jitahidi kuwa na kauli nzuri ili ukaribishe watu(including mumeo) badala ya kufukuza. Mwanamke ukiwa na kauli mbovu na kuropoka hovyo mwanaume hatoona fahari kukaribisha wageni nyumbani wavutiwe mdomo,wanuniwe na kuropokewa mpaka watamani kuondoka wala hatoshawishika kuwahi kurudi nyumbani.
sometimes wanaume wanachangia sana wake zao wawe na kauli mbaya. mara nyingi hasira hupelekea kauli mbaya. mwanaume anatoka kazini mapema ila kufika home mpaka sa tano za usiku na unajua kabisa hana hata kibanda cha kuuza vocha. kama mke alikuwa na kauli mbaya tangu awali ilikuwaje ukamuoa? kama amebadilika baada ya ndoa nini sababu ya mabadiliko hayo? hapo utagundua wewe mwanaume kwa namna moja au nyingine unachangia. halafu kwa maisha ya sasahvi wageni wakizidi home nayo ni kero, sometimes kauli mbaya za wanawake zinasaidia kusawazisha kiwango cha wageni.
3.Kuwa msafi. Usafi wa nyumba unamvutia mtu kuwa nyumbani, usafi wa mwili unamvutia mtu kuwa karibu na wewe. Ukishidwa kutofautisha nyumbani na kiwanda cha karatasi kwa hewa nzito/dampo kwa mvurugiko hamu ya kuwepo nyumbani inapungua.
usafi muhimu jamani, ila hata wanaume sio mnavua soksi na kutupa tupa tu hovyo kisa wife yupo atasafisha. muwajibike na nyie.
4.Angalia Watoto wako vizuri.
Kuna watoto bwana hata kama unapenda watoto namna gani huwezi kuwabeba. Utaishia kumuongelesha tu na kumshika mashavu. Usiache mtoto aonekane mchafu mchafu kila wakati.
jukumu la kulea watoto ni la wote kwa nafasi tofauti. kuna wazazi wao wanahisi majukumu yao yanaishia kwenye kumlisha na kumlipia ada ya shule tu. kuna mengi zaidi ya kumfanyia mtoto na hii inahusisha pande zote mbili,
5.Jitahidi kwenye maswala ya UPISHI. Sio lazima uwe mtaalam sana, jifunze kiasi cha kuwafanya watu wafurahie chakula chako. Badala ya mwanaume kurudi ameshiba kila mara, hata akila nje ya nyumbani bado awe na hamu ya kula/kuonja chakula cha mkewe. Na badala ya kwenda kukutana na marafiki zake kwenye nyama choma/supu za mtaani awakaribishe nyumbani kwa chakula.
Mwisho kabisa msisahau UKARIMU. Usiwe mchoyo, usiwe mroho.
tabia ya wanaume kupenda kula mtaani hata haichangiwi na mwanamke, naweza sema ni uchoyo au ubinafsi wao. mwanaume anaona akinunua kuku apeleke nyumbani wakati pale kuna watu zaidi ya tano, hatofaidi. anaona bora apite bar ajichane mwenyewe.hebu fikiria kama mkewe hawezi kuchemsha hizo supu au kuchoma nyama kwa nini asinunue nyingi akale nyumbani? ni uchoyo wao tu. mi nachukia sana mwanaume anaekula kwenye mabar wakati kwake angeweza kukuta msosi. tujitahidi na family planning pia, familia ikiwa kubwa sana kuliko kipato hamuwezi kufurahia msosi hata mama akaange vipi baadae chuzi lazma lijazwe maji ili litoshe.