Fahari ya mwanaume

Fahari ya mwanaume

Fahari wa mzazi = mtoto
Fahari wa mke = mume
Fahari na mume =mke
Fahari ya mwalimu =mwanafunzi
Fahari ya mwenye nyumba =nyumba
N.k

Hamna kitu kizuri kama mtu kuwa na kitu ambacho kinampa ufahari. Na ukiwa nacho hutoacha kuki'show off'. Sadly, familia nyingi kwenye jamii yetu zina wanaume wasioona fahari kuwa na wake walio nao, wakati mwingine hata watoto kwahiyo kuwa'show off' ni nje kabisa ya matakwa yao.

Juzi kati kuna mkaka alirudi nyumbani kwake usiku akaanza kugombana na mke wake (heeey I couldn't help it. Huku uswahilini hatuna ceilingbord wala madirisha, your business is everyones bussines). Nwy baadae jamaa akawa analalamika kwamba mwanamke wake ana kauli chafu, kila akirudi anapokelewa na makelele. Which made me think, wanawake (sio wote wala sisemi wengi) huwa wanalalamika waume zao kuchelewa nyumbani, kutopenda kuongozana nao, kutokuwa karibu na watoto na mengineyo bila kujali wala kufikiria ni kwa kiasi gani wao wame/wanachangia hali hiyo.

Wanaume huwa wanaona fahari (sifa) kuongozana na wenzi wao pia kuwatambulisha wakiwa wamependeza. Wanaona sifa kukaribisha wageni/marafiki zao kwenye nyumba iliyopangiliwa vyema, kwa mke asiye na gubu hata kwa wageni, kwa mke anaeweza kuwakaribisha chakula wakakifurahia badala ya kudanganya wameshiba,kwa watoto wanaobebeka (sio mtoto ananuka mkojo muda wote na makamasi/udenda unatiririka kama chemchem) n.k

Mwanamke anatakiwa amsaidie mwanaume wake kuona na kupata fahari kwa kuwa na mkewe huyo, familia, nyumbani n.k

1.Jua kupendeza badala ya kuchekesha. Mfanye mwanaume wako apende na afurahie kuongozana/kuonekana na wewe bila woga wala aibu. Sio mtu tumbo ni kubwa kuliko kiwiliwili cha chini lakini bado unavaa nguo za kubana na kuchora mpaka wanaokuangalia wanakuonea aibu, mumeo ataona nini? Uso umepambwa kama xmass tree nani aonekane na wewe achekwe?

2.Jitahidi kuwa na kauli nzuri ili ukaribishe watu(including mumeo) badala ya kufukuza. Mwanamke ukiwa na kauli mbovu na kuropoka hovyo mwanaume hatoona fahari kukaribisha wageni nyumbani wavutiwe mdomo,wanuniwe na kuropokewa mpaka watamani kuondoka wala hatoshawishika kuwahi kurudi nyumbani.

3.Kuwa msafi. Usafi wa nyumba unamvutia mtu kuwa nyumbani, usafi wa mwili unamvutia mtu kuwa karibu na wewe. Ukishidwa kutofautisha nyumbani na kiwanda cha karatasi kwa hewa nzito/dampo kwa mvurugiko hamu ya kuwepo nyumbani inapungua.

4.Angalia Watoto wako vizuri.
Kuna watoto bwana hata kama unapenda watoto namna gani huwezi kuwabeba. Utaishia kumuongelesha tu na kumshika mashavu. Usiache mtoto aonekane mchafu mchafu kila wakati.

5.Jitahidi kwenye maswala ya UPISHI. Sio lazima uwe mtaalam sana, jifunze kiasi cha kuwafanya watu wafurahie chakula chako. Badala ya mwanaume kurudi ameshiba kila mara, hata akila nje ya nyumbani bado awe na hamu ya kula/kuonja chakula cha mkewe. Na badala ya kwenda kukutana na marafiki zake kwenye nyama choma/supu za mtaani awakaribishe nyumbani kwa chakula.

Mwisho kabisa msisahau UKARIMU. Usiwe mchoyo, usiwe mroho.
Okkkk
 
[emoji419][emoji419][emoji375][emoji375][emoji375]
 
Back
Top Bottom