Kyambamasimbi
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 762
- 1,597
Ndugu wanajf habari, binafsi ninaposafiri navutiwa Sana na baadhi ya maeneo japo mengine yanakera
Ninayoyapenda
Unaposafiri barabara ya Kutoka Dar kwenda Moro Kuna kasehemu kana msitu unapotoka bwawani Kuna kamsitu kazuri na kanavutia barabara yake nzuri. Pia ukifika Moro zile safu za milima ya ulugulu zaidi ukienda mjini Kati kule forest Morogoro.
Kwa Dar napenda kuona makazi ya watu mji ulivojengeka. Sehemu nyingine kutoka Mikumi Kuna vijiji vya Iyovi,Ng'apa msimba kule ambako barabara inapita kando ya mto ruaha na safu nzuri za milima zilipambwa na hifadhi ya msitu, zaidi wasiojua mto Ruaha ni moja ya mito inayojaza mto rufiji ukiwa umetokea bonde la Usangu Mbeya.
Nchi yetu nzuri nyie pia Kuna sehemu ya hifadhi ya Ardhi oevu yaani Wetlands katika msitu wa Sao hill Iringa. Wewe ulivutiwa wapi? Na wapi hukupaelewa hata wakupe bure huendi.