Safi sana mkuu,umenikumbusha mbali sana,nyanya pori,matecha,chikanda,masuku,mabungo,mbula,ntalali,makangala,nyimbwa,ndagu(matunda). Kantasila (big g za kifipa). Hali ya hewa safi huku,kibaridi cha hapa na pale. Gharama za maisha ziko chini. Unaweza kuwa na mtaji kidogo na ukatoka kimaisha kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali zinazoweza kukupa kipato halali. Nasikia barabara za Sumbawanga- Mpanda na Sumbawanga-Matai-Kasanga na Kasesya mpakani wakandarasi wameingia kuanza ujenzi wa barabara hizo kiwango cha lami. Barabara ya Sumbawanga-Tunduma mkandarasi anaingia mwezi ujao wa 4. Hakika maboresho ya miundombinu yataleta changamoto kubwa mkoani Rukwa na tunategemea mkoa huo sasa utaruka kimaendeleo.