Faida 10 ya kufanya kazi ya ualimu serikalini

Joined
Apr 8, 2014
Posts
60
Reaction score
18
Wapo wengi wanatamani kuwa serikalini baada ya kupoteza nafasi hizo kwa dharau ya mishahara kuwa ni midogo.
Ni dhahiri kuwa kuna tofauti ya mishahara kati ya serikalini na private.. Bt lengo langu ni kuwataka wale wasiofanya maamuzi sahihi kwa kukurupuka kwenda private na kurudi Baadae kutaka kupata kazi tena serikalini baada ya kugundua kuwa walikosea.

1. Ukiwa serikalini mazingira ya kufukuzwa kazi ni magumu ukilinganisha na private, otherwise umefanya kosa kubwa sana au Una rekodi ya mfululizo wa makosa

2. Kuna utaratibu maalumu wa kupanda madaraja... Changamoto iliyopo ni Smtyme Wengne huchelewa kupandishwa bt ukiwa aware unaweka mambo sawa..

3. Shule hata ikiwa na wanafunzi wa3 serikali itakulipa kwa uhakika Mshahara wako hata kama wengine wanaona unalipwa kidogo. Na hawawezi kukosa pesa ya kukulipa.

4.unaweza kuhama kutoka kijiji,kata,wilaya,au mkoa mmoja kwenda mwingine na kuendelea kufanya kazi kwavle bosi serikali Ana shule nyingi Kila uendapo.

5. Unaweza kufanya kazi sehemu zingine ukalipwa vizuri kwakuwa unapata nafasi ya Ku"manage" ratiba yako na kufanya kazi za mabosi wengine.

6. Unaweza kupata muda mwingi wa kukaa na familia yako,kutembelea ndugu, mashamba, mifugo yako n.k

7. Unaweza kwenda kusoma ukaendelea kulipwa Mshahara wako kwa miaka hata mi3..

8. Unaweza kupata "deal" ya kuingiza pesa ukaandika barua kuomba likizo hata miaka kadhaa ukimaliza unarudi utaikuta nafasi yako...

9.hata kama kazi unayofanya ni kidogo uhakika wa Mshahara uko palepale na kadri miaka inavyosonga recruitment zinapunguza mzigo

10. Unaweza kufanya kazi zako ndani ya siku 2 au 3 kwa wiki na ukawa umemaliza majukumu yako.

Na mengine mengi sana... Coz kuna jamaa kaajiriwa mwaka huu hajaenda kuripoti kusikia asilimia 10 tu zilizoongezwa za tuhela tudogo tayri shida maana ashazidiwa 15,000 na walio serikalini na anafundisha mwanzo mpaka mwisho wa wiki.. Nadhani zipo nyingi...Lakini pia tusisahau changamoto za kufanya kazi serikalini
 
faida pekee niliyoiona majuzi ni hii:

Nilishangaa nilipokuwa napiga stori na kijana mmoja nilipokuwa shinyanga kisha akasema ngoja nikaangalie kama mshahara umeongezeka, akaingia NMB na kukuta kaongezewa elfu 25000 nikashangaa kwa kuwa najua mshahara wake unapitia benki nyingine, nikamuuliza inakuwaje?? Akanjibu , kaka apa mjini mwalimu ukishaajiriwa hautolewi kwenye database, aliaga anaenda kusoma akamaliza digrii akaanza kazi kwenye sekta nyingine tena private, ivo serikali wanatunisha kapu lake na mwajiri wake mpya anaweka kwenye benki akaunti ya benki nyingine, jamaa anakula double salary, katika kushangaa nikamuulize mwingine kama inawezekana, jamaa alijibu tu, unashangaa, mimi mwaka wa3 siko kwenye ualimu na nakula kawaida,na sio sisi tu ndo utaratibu wa kawaida serikalini, akaniambia ilo tu, jamaa yangu alikuwa mhasibu wa wilaya xxx kazi ikatazangazwa AMREF akaomba likizo, yuko AMREF anasoma masters mzumbe evening class na kote mishahara inaingia... dah nilitoka kichwa chini.... ILA MJUE YOTE NI KINYUME CHA SHERIA !!
 
Reactions: keh
hiyo ni tempo tu watafanya sensa watagundua na watafunga.
 
HASARA: Ukishastaafu unalipwa pensioni ya Tsh milion 40, na kuchekelea sana wakati mmachinga anayeuza mitumba Kariakoo, huingiza kiasi hicho kwa mwaka mmoja tu. Endelea tu kupumbazika huko serikalini....utastaafu bado unaishi kwenye nyumba ya kupanga.
 

Hao hawanaujanja hata kidogo kwani pesa zao zilizopo kwenye mifuko ya jamii zitafidia hasara waliompa mwajiri wao ambayo ni serikali.Ila baada tu ya kuhundulika na watagundulika.
 
We jidanganye tu,kwa taarifa yako waalimu wanaoajiliwa miaka hii awategemei hiyo pension unayoiwazia wewe wengi ni wajasiliamali.Sasa ubaki unajidanganya hivyohivyo.Mi kwa mwezi nafundisha mara moja na mshaara wanaonipa kwa ufundishsji huu unanitosha sana na wala sitaki waniongezee.
 
sijawahi skia mwalimu tajiri yani anamafanikio makubwa kama watu wengine yani mshahara wao unawafanya waishi wasomeshe watoto nao sio wengi ukikuta zaidi ya wawili basi full mikopo, halafu ukiwa mwalimu usitegemee utakuja kuwa na zaidi ya maisha ya kawaida tu labda usubiri kiinua mgongo ndio ufanye maendeleo utakuta mtu ndo anajenga guest sjui gari nk, ni Uchunguzi wangu tu walimu wengi wakawaida, samahan walimu ila mnatumika kama daraja tu na mnachofanya hakiendani na kazi yenu.!!
 
Hao hawanaujanja hata kidogo kwani pesa zao zilizopo kwenye mifuko ya jamii zitafidia hasara waliompa mwajiri wao ambayo ni serikali.Ila baada tu ya kuhundulika na watagundulika.

ok , ila mmmhhh kumbe inaruhusiwa kumkata mtu pesa kwenye mfuko wa jamii eheee???
 
Mie nafundisha j3 dk80 j4 dk120 na j5 dk 40 ukijumlisha ni masaa 4 kwa wiki means kwa mwezi ni masaa16 mda mwingine nafanyabusiness zangu binafsi anayeona ualimu siyo deal afanye hivyo kwa bosi wake aone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…