Faida elfu 30 kwa siku

Faida elfu 30 kwa siku

Weka benki, ni more secure kuliko kwenye simu. Uwe makini tu kufuatilia balance yako maana kuna wafanyakazi benki ambao sio waaminifu. Ila wakiiba na kama wewe una data kamili kuhusiana na balance yako hupati hasara ila benki ndiyo itakuwa imekula hasara.
Na uzuri sasa hivi benki kuu (BOT) wamefungua dawati la malalamiko kama umetendewa ndivo sivyo kwenye hizi commercial banks na swala liwe linapigwa danadana
 
We mzee wa kulialia kumbe wewe tajiri mkuu.
Maana mie kijana akiweza kuingiza faida ya elfu 30 tu basi ni tajiri,maana ni pesa nyingi sana na ukiweka nidhamu basi unatusua ile mbaya.Naeleza hivyo kwakua najua nilipotokea.

Nakushauri weka Bank kama fixed vile,ili ikae huko kwa muda mrefu Halafu wakati huo unafikiria biashara ya ziada ya kufanya,yaani biashara mpya.Wakati wewe unapiga roving zako,pesa ikifikia kiasi fulani basi unaanzisha biashara hata kama ndogo ya laki mbili au tatu,ukiona inalipabasi tafuta mtu umuweke ili uwe na biashara zaidi ya moja ila iwe tofauti na unayofanya.Licha ya kwamba unaweza kwanza kuboresha hiyo uliyonayo ila kama umefika kwenye level fulani unaanzisha mpya.

Hapo akili yako itatanuka,na hata soko la upande mmoja likifa basi upande mwingine upo vizuri unawezakukaza huko
Mie miaka ya 2003 nilikuwa na banda la sim zile za kupigisha,wakati huo sim ya mkononi aisee watu kibaoo hawana,nilipiga hela balaa,na 2004 nikaoa harusi kubwa ile mbaya,maana pesa ilikuwepo,we unauza kadi zote na unapigisha sim bonge la foleni.Then baada ya kupata pesa nikamuita mdogo wangu nikawa nauza Tv na Deck natoa Zanzibar naleta Dar,nilipga hela balaa mkuu,kisha nikaanza kupeleka Mwanza.

Nilivyokuwa imara nikaanza kupeleka Burundi,ila huko nilienda round moja tu,ile round ya pili nilipeka Tv kama 200 na deck 300,basi mie na wenzangu wote tulitekwa,wakatupa kichapo cha maana,huku na silaha,wakahamisha mali zoote wakakimbia,tulikaa siku kadhaa kwenye maji ndio tukaokolewa na patrol,maana hata mashine walichukua,siisahau siku hii,sijaenda teeena na wala sifikirii kwenda

Kisha,nikaingia kwenye biashara ya kutoa Mashuka ya Kigoma kuuza hapa Zanzibar,piga hela tena hapo,leo imechupia kwenye Carry na Bodaboda,na Spices kwenda Commorro,at the same time pesa ikifika kiasi fulani naanzisha jingine,nina Idea binafsi kwenye Kitambu changu zinafikia biashara 47,na zote nimeishafanya research kwa level fulani na zaidi nashkuru saana wana JF woote na mbarikiwe saana,mambo mengi na ujasiri nimeupata humu,lazima nikiri hilo.Jukwaa hili ni msaada saana kwangu,kule kwenye Siasa tunatukananaaeee tukija humu letu lazima liwe moja.

Ni habari ndefu kiasi mkuu
Lengo nio kukuonyesha kwamba biashara zinatabia ya kubadilika sana tofauti na unavyofikiria mkuu,sasa lazima akili uifungue kwa kuwa na biashara zaidi ya aina moja.
Nisikuchoshe mzee wa kulialia
Kwanza pole kwa matatizo uliyopata lkn jambo la kushukuru mungu uzima uliyonao,
Nashukuru kwa ushauri ngoja nijitahidi kama mwanaume wa kweli
 
nenda pale UTT sukari house kama upo DSM, ukafunzwe jinsi ya kununua na kuuza hisa a.k.a kuweka akiba, ni rahisi sana hautajuta kuweka akiba yako, kujiunga ni bure kabisa pia NMB wana account ya NMB chapchap unafungua na kupewa account hapohapo kwa maelezo ni pm nikuelezee zaidi.
 
Tunza M-Pawa(Vodacom), au Tigo-Pesa.
1.Uzuri wa M-Pawa unaweza kukopa hadi laki tano(500,000/=) pale unapohitaji.
2.Uzuri wa Tigo-Pesa unapata gawio kila baada ya miezi mitatu, Mimi huwa nakula Gawio langu kila baada ya miezi mitatu, Jana tu nimepokea Gawio langu.

na mie nimepewa Jana gawio langu 320..
 
Back
Top Bottom