We mzee wa kulialia kumbe wewe tajiri mkuu.
Maana mie kijana akiweza kuingiza faida ya elfu 30 tu basi ni tajiri,maana ni pesa nyingi sana na ukiweka nidhamu basi unatusua ile mbaya.Naeleza hivyo kwakua najua nilipotokea.
Nakushauri weka Bank kama fixed vile,ili ikae huko kwa muda mrefu Halafu wakati huo unafikiria biashara ya ziada ya kufanya,yaani biashara mpya.Wakati wewe unapiga roving zako,pesa ikifikia kiasi fulani basi unaanzisha biashara hata kama ndogo ya laki mbili au tatu,ukiona inalipabasi tafuta mtu umuweke ili uwe na biashara zaidi ya moja ila iwe tofauti na unayofanya.Licha ya kwamba unaweza kwanza kuboresha hiyo uliyonayo ila kama umefika kwenye level fulani unaanzisha mpya.
Hapo akili yako itatanuka,na hata soko la upande mmoja likifa basi upande mwingine upo vizuri unawezakukaza huko
Mie miaka ya 2003 nilikuwa na banda la sim zile za kupigisha,wakati huo sim ya mkononi aisee watu kibaoo hawana,nilipiga hela balaa,na 2004 nikaoa harusi kubwa ile mbaya,maana pesa ilikuwepo,we unauza kadi zote na unapigisha sim bonge la foleni.Then baada ya kupata pesa nikamuita mdogo wangu nikawa nauza Tv na Deck natoa Zanzibar naleta Dar,nilipga hela balaa mkuu,kisha nikaanza kupeleka Mwanza.
Nilivyokuwa imara nikaanza kupeleka Burundi,ila huko nilienda round moja tu,ile round ya pili nilipeka Tv kama 200 na deck 300,basi mie na wenzangu wote tulitekwa,wakatupa kichapo cha maana,huku na silaha,wakahamisha mali zoote wakakimbia,tulikaa siku kadhaa kwenye maji ndio tukaokolewa na patrol,maana hata mashine walichukua,siisahau siku hii,sijaenda teeena na wala sifikirii kwenda
Kisha,nikaingia kwenye biashara ya kutoa Mashuka ya Kigoma kuuza hapa Zanzibar,piga hela tena hapo,leo imechupia kwenye Carry na Bodaboda,na Spices kwenda Commorro,at the same time pesa ikifika kiasi fulani naanzisha jingine,nina Idea binafsi kwenye Kitambu changu zinafikia biashara 47,na zote nimeishafanya research kwa level fulani na zaidi nashkuru saana wana JF woote na mbarikiwe saana,mambo mengi na ujasiri nimeupata humu,lazima nikiri hilo.Jukwaa hili ni msaada saana kwangu,kule kwenye Siasa tunatukananaaeee tukija humu letu lazima liwe moja.
Ni habari ndefu kiasi mkuu
Lengo nio kukuonyesha kwamba biashara zinatabia ya kubadilika sana tofauti na unavyofikiria mkuu,sasa lazima akili uifungue kwa kuwa na biashara zaidi ya aina moja.
Nisikuchoshe mzee wa kulialia