Faida inayopatikana baada ya nesi kumpiga makofi mama mjamzito

DZUDZUKU

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2012
Posts
3,909
Reaction score
2,115
Ndugu habari,

Kuna huu mtindo wa manesi kupiga makofi wajawazito wakiwa labour (usikatae hili jambo lipo) hasa kwa baadhi ya wanawake wanaochelewa kusukuma mtoto.

Je, kuna faida gani inayopatikana baada ya wao kuwapiga makofi? Kama mjamzito anashindwa kupushi si apewe maji ya uchungu tu?

Nawasilisha..
 
Mjamzito huwa anaogopa kusukuma kwa kuhofia kuumia uke hivyo kofi linamlazimisha ili asiue mtoto
 
kofi kinasaidia ili ajilazimishe maana akizembea mtoto anaweza kufa so lazima alazimishwe kusukuma..... ikishindikana basi njia mbadala sitatumika.
 
Mjamzito huwa anaogopa kusukuma kwa kuhofia kuumia uke hivyo kofi linamlazimisha ili asiue mtoto

Na uchungu ule bana anawaza uke?
Na kwa nini watu wanalalamika kwamba manesi Ni wakali?
 
kofi kinasaidia ili ajilazimishe maana akizembea mtoto anaweza kufa so lazima alazimishwe kusukuma..... ikishindikana basi njia mbadala sitatumika.

Kofi linaongeza uchungu?
kwa nini asiongezewe maji ya uchungu badala ya makofi?
 
Nesi kupiga mama kibao hairuhusiwi kabisa, ila kuna wakati inabidi kuchapa kibao na kukoromea sana, haiongezi uchungu ila inaongeza usikivu na mtulivu kwa mama mwenye maumivu mpaka anakua kama kachanganyikiwa! Mfano unakuta njia imefunguka vizuri, Mtoto ameshuka vizuri na tayari sehemu ya kichwa cha Mtoto imeshaonekana! hapo uchungu unakua mkubwa sana! mama anabana mguu wakati nesi anasubiri kupokea Mtoto!

Hapo kibao lazima kihusike ili mama awe mtulivu na kusaidia kupata mtoto asiyekua na matatizo kwenye ubongo! Kwani kina mama wengi ambao wanakua wakorofi wakati mtoto anataka kutoka huwa wanaharibu sehemu za ubongo wa watoto wao bila kujua! Madhara yataonekana miaka ya mbele na mama hatajua ni kwa nini!
 
Kofi linaongeza uchungu?
kwa nini asiongezewe maji ya uchungu badala ya makofi?

Sio kila mama ana qualify kupewa maji ya uchungu. Kuna sababu za zinazopelekea mama kupewa hayo maji
 
Waendelee kupiga,mtoto akifa lawama kwa nani?
 
Hata mimi majuzi nilibonda mtu,sitaki upuuzi kwenye mambo ya msingi,wakati unachetua viuno ujue iko siku utaitwa mama,na kuitwa mama si lelemama,kaa vizuri niku pv,unaruka juu kama swala.sikuachi,
 

Umeeleza vema,kunaumuhimu wa makofi just to gain mothers attention, ila inategemea Na mazingira.

Swali, je mama akishajifungua Na kuamua kumshitaki nesi inakuwaje hapo?
 
Mkuu niliwahi kumuuliza swali hili nesi mmoja
alinijibu kuwa kuna wanawake hawataki kufuata maelekezo
wanayopewa na manesi ili kujifungua salama,
sasa kama unatoa maelekezo mtu anafanya kinyume
na wewe nesi unajua fika kitendo anachokifanya mgonjwa
ni hatari kwake na kwa mtoto pia,ukimtia kofi
anazinduka anajua kwamba siyo utani,unachomwambia
ndicho unachomaanisha.

Hasara kwa manesi kama unazalisha watoto wamekufa
kuna namba unayohesabiwa,ikifika kazi huna
hivyo kama mtu analeta masihala wakati wewe
uko serious ukimtia kibao naye anakuwa serious
na hatimaye yeye anapata mtoto,nawewe unabakia na kazi yako.

Alikili kuwa kuna wanaotumia vibaya mwanya huo
pia alikiri kuwa siyo lengo lao kupiga mgonjwa
ila inapobidi wanafanya.
 

Baada ya kujifungua, huyu mama akimshitaki itakuwaje?
 
Na wapigwe tu ili mtot abak salama

Mh.....ndugu we acha Tu, kazi ya kuzalisha Ni ngumu, unaweza ukamtia makofi baadae akakushitaki kwamba umemshambulia.
 
Baada ya kujifungua, huyu mama akimshitaki itakuwaje?

Not in tanzania na kama atashtakiwa basi lazma mgomo wa manesi utokee au wategemee kupatata watt wafu na wenye mtindio wa akili kwa wingi. Kwa kosa tu la mama kutokutii masharti ya nesi. Au basi waanze kusupply epidural ili kumpunguzia mama maumivu kama wafanyavyo nchi za wenzetu.
 
Baada ya kujifungua, huyu mama akimshitaki itakuwaje?
Nadhani sheria inachukua mkondo wake,
kama polisi asivyoruhusiwa kumpiga mharifu kama hajafanya
fujo,mharifu akipigwa akashtaki sheria inachukua mkondo wake
akinyamaza kimya ndo mwisho wa kesi.

Ila cha kujiuliza ni kwamba atashtaki kwa kusaidiwa kujifungua
salama au kwa kupigwa kibao ili asimsababishie mwanae madhara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…