Faida na changamoto za magari yanayotumia cng ( compression natural gas) part 1

Jackpiano

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2025
Posts
560
Reaction score
756
Part 1: Faida na Changamoto za Magari ya CNG

Faida za kutumia CNG:

Gharama ya kujaza ni ndogo, unaokoa hadi 50% ukilinganisha na petrol/diesel.

Inapunguza uchafuzi wa hewa — moshi kidogo, mazingira safi.

Inapunguza uchakavu wa injini kwa sababu CNG inaungua safi.

Ukiwa na dual system, unaweza kuchagua kutumia gesi au mafuta muda wowote.



---

Changamoto za kutumia CNG:

Gharama kubwa ya kufunga mfumo (milioni 1.5 – 2.5 kwa ubora wa kati hadi mzuri).

Vituo vya kujaza CNG bado ni vichache nje ya Dar na Morogoro.

Tanki linaongeza uzito na kuchukua nafasi ya buti.

Mafundi wa CNG ni wachache, hivyo matengenezo yanaweza kuchelewa.

Kwa sasa Tanzania:

Serikali inaendelea kupanua vituo vya kujazia gesi.

Makampuni ya teksi yameanza kuhamia CNG kwa kasi ili kupunguza gharama.

mwisho part 1 subiri part 2 hivi soon niandae
 
Washauri tuu wanunue Hybrid yaani umeme hata Bajaji zipo za umeme mkuu gesi zinaaribu performance ya chombo unakuwa kama unaendesha mkokoteni
 
Niliona msururu wa kujaza gesi kule karibu na Airport duh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…