Faida na hasara za East Africa Community (EAC)

Faida na hasara za East Africa Community (EAC)

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Ndugu wana JF naomba kiwasilisha.

Naomba tujikite kujadili kwa kina faida na hasara za kuungana na kuwa jumuiya ya Afrika mashariki.

Kwa historian muungano huu uliwahi kuwepo na ukavunjika kwa sababu kadha wa kadha.

Je, zile sababu zilizosababisha kuvunjika kwa Afrika mashariki ya zamani tunazijua? Kama tunazijua tunazitatua vipi?

Naomba tujikite kujadili kwa kina faida na hasara za kuwa na muungano huu katika nyanja zifuatazo:-

1. Kiuchumi
2. Kisiasa
3. kiutamaduni na kijamii

Haya ndiyo mambo makubwa yanayochagiza watu kuwa pamoja.

Je, mifumo yetu ya uchumi inaweza kuunganishwa na kuwa mfumo mmoja? Sera za kiuchumi kwenye nchi zetu zinakaribiana!?

Kwa maoni yangu tungebaki kuwa washirika tu, na siyo kuwa na community. Hii inatokana na kwamba Tunatofautina sana kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Baada ya wakoloni kuondoka walikuwa wametengeneza tamaduni tofauti baina ya nchi zetu hizi.

Nawakaribisha tuchangie mawazo na ushahidi.
 
Tanzania haiwezi kuungana na Kenya na Rwanda hata siku moja. Ile tume iliyoundwaga kipindi cha kikwete ilipata majibu mujarab. Kenya alikuwa anapush for political federation mahsusi kwa suala la ardhi. They wanted to grab Tz land then we said NO.

Kama wako serious na kuchukua ardhi waanze na ile ya familia ya bwana mkubwa, wachukue na ile ya ma settlers..wakimaliza ndio waje mezani tuongee.
 
Hii integration ilikufa sababu ya ideology differences, IDD amin alikuwa muumini wa imla, nyerere mjamaa, na Kenya walikuwa mabeberu so muungano ulikufa kwa sababu hizo na mpaka sasa utofauti wa ideology bado upo ndomana integration imedumaa
 
Masuala ya kijamii

Kwa sasa jamii za Afrika mashariki zinatofautiana sana. Baadhi ya nchi hapa Afrika mashariki zinajiona kwamba zimeendelea kiasi ya kujiona miamba.

Hili jambo linapitishwa kwa wananchi wa jamii hizo kuwafanya wananchi wawe makatili wasiojali wengine.

Kwangu ukiniuliza leo nitasema hasara ni nyingi mno kuliko faida. Bado naadhi ya nchi uongozi unaenda kwa makabila. Na nchi hizo zimewagawa watu katika madaraja. Kwahiyo itakuwa ngumu katika nchi zilizoamua kuwaweka watu wote wawe sawa.
 
Mimi nakubaliana nawe kabisaa. Hadi kuna baadhi ya nchi zingine kwa kujichokea na uvivu wa kujituma tuu hawajambo. Hata wakiwa na kila raslimali wao ni kujikokota kama manyumbu mzee. Ni bora wenye kulala wakatandike malazi kwao wasije kudandia migongo ya wachapa kazi. Kibinafsi hata mimi ningependelea hali ibakie hivihivi!. 🤣🏃🏃
 
How can you call somebody lazy wakati hajawahi hata kukuomba au kuomba chochote sehemu yoyote!?

This is the mentality mnayofumdishwa about Tanzania.
 
Baadhi ya nchi Kenya in particular are so selfish. Wabinafsi mno yaani. Ndo maana hata ukabila hauondoki kwao. Huu ndo ukweli ambao hata nafsi zao zinawashuhudia.
 
You
How can you call somebody lazy wakati hajawahi hata kukuomba au kuomba chochote sehemu yoyote!?

This is the mentality mnayofumdishwa about Tanzania.
Loooolest! You are so predictable. Nilijua utaangukia mtego. Hata mimi naweza dai kile ulichokiandika hapo awali ni zile hadithi za alfu lela ulela mumeaminishwa dhidi ya Kenya. Lakini kwa vile hukuitaja Kenya singekushutumu. Sasa wewe ni kwa kigezo gani unaweza dhibitisha nilimaanisha Tanzania licha ya kuwa sikuitaja?. 🤣🤣
 
Hii community imefeli na inaenda kufa tena, hakuna muungano wa mlengo wa kushoto na mlengo wa kulia na pakawa na amani milele. Itakuwa ni mivutano mwanzo mwisho, Africa ni mpaka iungane yote sio huu uhuni unaoendelea. Watu wanakula tu mishahara na maposho ila hamna kitu hapo.

Tutaishia tu kwenye uadui kama Nesta na Tosh.
 
Baadhi ya nchi za East Africa eg Rwanda na Kenya wameruhusu free movement baina ya member wa East Africa. Hakuna Viza. Hii inaweza chagiza maendeleo . Ngoja tuone nchi nyingine watarespond vipi.
 
Back
Top Bottom