Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Lakini hapo pa alluminium yawekewe bawabu badala ya ku slide nimekuelewa ,
Lakini naona kama madirisha yatakuwa makubwa ie. 2M na kuendelea itakuwa ni rahisi na salama kufanya hivyo?

Nazani kwa madirisha madogo ni sawa ila kwa makubwa yaweza vunjika au?


Sent using Jamii Forums mobile app
Anayagawa mara 3
 
Concrete gutter huwa haiwezi kuziba mkuu?
Msingi wa hoja yangu kuhusu kufanya maintenance ya gutter ni endapo kama ndege au mijusi imepeleka takataka zinazoweza kuziba hiyo gutter
Mkuu ukiweka wavu/kichujio haiwezi kusaidia? Unakuwa unasafisha kwenye wavu/chujio regularly.
 
Design ya namna hii ni nzuri.
A. Faida :-
bati na mbao ni chache.
Nzuri kimazingira.
Ni vigumu kuezuliwa na Upepo.
Kwa kiasi inaongeza ukubwa wa nyumba.
Unasaidia katika uvunaji wa maji ya mvua.
B. Hasara:-
Isijengwe palipo na miti mirefu.
Huitaji uangalizi hasa katika usafi juu ya papa.
Huitaji mfumo imara wa kupitisha maji ya mvua.
Ni rafiki kwa wanyama na ndege.
Ni lazima uwe na ngazi ya kufikia paa (usafi /ukarabati).
Huitaji umaliziaji mzuri kwa nje.
Huitaji headroom kubwa ili kupunguza Jotoridi ndani ya nyumba.

Kujenga nyumba ya namna hakupunguzi gharama za Ujenzi kwani nafuu ya kitu fulani huongeza gharama ya kitu kingine.

Hata hivyo Flat roof (0-10 degree slopes) kama ikijengwa kwa zege manufaa yake ni mengi zaidi kuliko kupaua kwa bati.
Uko sawa kabisa
 
Back
Top Bottom