Mimi ni Simba,ila natofautiana na wewe kwa maandishi yako ya kuwatukana mashabiki wenzako na kuwadhiaki kwa kuwaita wajinga!! si lugha nzuri na yenye staha!!
Simba ni taasisi ya michezo ina mashabiki wa kila rika,kila jinsia,kila umri, wenye mtazamo tofauti na style tofauti,kuna ambao hawana elimu hizi za kisasa ndio wengi wao uko nyuma walishiriki bega kwa bega na wengine kuanzisha hii club yetu pendwa,
Kuna wenye elimu walitumia elimu yao kuisaidia na wengine kuiibia club yetu pia,kuna wale wasio jua lolote kuhusu modern football hawajui sijui Asenal,sijui Manchester!!hawajui kama kuna Fifa wala CAf,wao wanachojua ni Simba SC tu,na wanaipenda kufa wananunua jezi,wanawanunulia jezi watoto na ndugu zao,wanakata tiketi kuingia uwanjani kila mara,na Simba ikifungwa wanalia machozi hawajui neno kupoteza au matokeo matatu!!
Wengine wanazimia,na wengine wanakufa kabisa,kuna mashabiki wengine waliwahi kuwa wahaini lakini wametoa mchango mkubwa sana kwa club yao wanayoipenda sana,hivyo kila mtu anastahili heshima na kuchukuliwa kama ni mtu mwenye mchango kwa club yake.
Kuna wengine hawapendi kuona club yao na viongozi wao wanaojitolea pakubwa, kutukanwa na mtu yeyote,wanajitoa kujibu mashambulizi kwa kila namna ili kulinda viongozi na timu yao,tutumie lugha nzuri tunapokuwa tunawaongelea Simba ni yetu na Simba ni nguvu moja as long as ni burudani tu za duniani na tukifa tutaziacha hapa duniani.