MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Jikumbushe kwanza huu uzi;
www.jamiiforums.com
Nia yangu ilikuwa kusaidiana bila kujali kupata chochote baada ya hapo ila katika hali ya kushangaza baadhi ya wachina ambao tumeshakuwa marafiki sana wakanijulisha kuwepo kwa wateja wapya kutoka Tanzania. Nami nikawapasulia jibu kwamba niliwapa namba zenu. Walijikuta wanafurahia na kunishukuru sana. Na wakaenda mbali zaidi na kusababisha nipate faida zifuatazo;
1. Baadhi walinitumia zawadi ambazo bado ninazisubiri. Sijajua walichokiweka ila wameniambia ni "digital devices"... natarajia kulipa usafirishaji karibu Tsh 800,000/= kwa kampuni ya Yoonek cargo. Inaonyesha sio zawadi haba.
2. Wote wamenipa punguzo maalum kwenye vitu vyote nitakavyonunua. Ni punguzo ambalo hata mimi mwenyewe sijawahi kutegemea. Kwa mfano supplier wangu wa mabegi ya shule kanipa punguzo la karibu 50%.
3. Uhusiano wetu umeimarika zaidi kiasi kwamba hata machimbo ya vitu vingine pia wameshaanza kunisaidia kuyapata.
Nimeandika huu uzi makusudi ili kuwapa moyo watu kuwa tusaidiane tunapoweza kusaidiana. Mungu anaona unachokifanya... hakuna mtenda mema ataachwa ateseke. Mimi ni shuhuda wa hili.
Ninajitolea kutoa namba za machimbo ya China kwa wapambanaji wenzangu
Ili kuunga mkono ilani ya uchaguzi ya CCM leo nami nimeona nichangie angalau connection ya machimbo kadhaa ya vitu mbalimbali huko China. Haya ni machimbo ambayo nimekuwa nikifanya nayo kazi kwa miaka kadhaa sasa. Ninatumaini itasaidia kwa wapambanaji ambao wanahangaika kupata connection hadi...