Hizo zote zimekubali ila ukuaji wake ndo umetofautiana nilipanda siku moja lakini zipo nilizoanza kula baada ya miezi 10 na zingine mpaka mwaka na nusuUpo sehemu gani? maana sidhani kama aina hizi zote za migomba zinaweza kustawi sehemu zote Tanzania
Mgomba una matumizi mengi sana, hujaumaliza. Yapo kama;Nawasalimu kwa jina la jamhuri
Mwaka jana mwezi wa kwanza nilipanda migomba kama 30 katikaeneo la nyumbani napoishi. Kabla ya kupanda niliwauliza wataalamu hasa watu wanaotokea maeneo ambayo wanalima sana ndizi kama Moshi, Bukoba na Tukuyu kujua aina za ndizi na matumizi yake na namna ya kupanda. Baada ya kupata maelekezo ya kitaalamu nikapanda aina zifuatazo za ndizi.
1. Mzuzu hii niliambiwa inafaa sana kukaangwa au kuchomwa
2. Bukoba hii kwa kupikwa
3. Mshale hii kwa supu
4. Malindi hii inafaa kuliwa ikiwa mbivu
5. Kisukari vile vidogo hivi navyo vinafaa kuliwa vikiwa vimeiva
6. Matoke hizi kwa kupikwa
Faida nayoipata kwa sasa;
1. Mazingira ya kuzunguka nyumba yangu yanavutia maana ni green tupu pamoja na kua tumeanza kiangazi
2. Nina chakula cha kutosha imenilazimu kununua fridge ya ziada ili ndizi zingine nizi freez humo maana zimenizia
3. Kipato changu (thamani ya shilingi kwangu imeimarika maana nimepunguza kwa kiasi kikubwa kutoa pesa nje kwa ajili ya kununua mahitaji )
4. Ninatoa sadaka hasa kwa wale ambao wanashida ya chakula angalau ninawapa ndizi kidogo kama sadaka na napata baraka kutoka kwa Mungu
NB
Kwa wale ambao tuna maeneo makubwa tumejenga basi tupande angalau migomba itatusaidia kuliko kujaza pavement na ukoka kwenye nyumba.
Kwa wale wanaotegemea kununua maeneo ya kujenga nawashauri mtoke kidogo nje ya mji mpate maeneo ambayo yatawawezesha kulima kidogo na kufuga.
ahaha ,,Kama Garagekuna wakati hua nakaa hata masaa mawili naangalia tu green iliyopo hasa wakati wa kiangazi. Nyumba hata kama ya kawaida inapendeza sana ikizungukwa na miti pamojana maua kuliko kujaza pavement maana zikifubaa panaonekana kama garage
we mama umenifurahisa sana vile umeandikaa yani watu wa mapishi hapo tunajua hicho ni kitu gani kinaenda kutoka hasa ukijumlisha na aina ya ndizi ilotumikaSiku moja chemsha utumbo utupie malindi mbichi kitunguu, hoho na pilipil mbiuz ya kishkaji
Hapo pia kuna maji, mbolea na udongo. Ulipochukua tetea ilibidi uchukue na udongo...Hongera ardhi yako ina rutuba. Kwangu migomba ipo shina moja lakini mkungu ulioko pale ni mdogo kama nanasi.
Hahaha migomba haitakiwi kuwa chini ya miti. Haizai mbee... inagoma kabisaa. Ulifanya jambo sahihi sana kuitoa.Nakubaliana na wewe..mimi awali nilipanda mipapai kama 100 hivi..ikasumbua wadudu na baadae wateja.Ila.toka nimeoanda migomba nakula.ndizi kama.kawa
KiongoziHongera ardhi yako ina rutuba. Kwangu migomba ipo shina moja lakini mkungu ulioko pale ni mdogo kama nanasi.
Umetisha mkuuMgomba una matumizi mengi sana, hujaumaliza. Yapo kama;
1. Mti wa mgomba wenyewe unaliwa, yani ile sehemu nyeupe iliyopo katikati kabisa mwa mti. Yana Potasium na Vitamini kwa wingi.
View attachment 1819383
2. Majani yale unaweza kutumia kama Foil Paper, pia kama sahani disposable.
View attachment 1819382
View attachment 1819384
3. Tafuta ndama jike apate msosi wa uhakika, chakula pendwa ukichanganywa na magadi kwa mifugo kama mbuzi na ng'ombe.
4. Magome yake hutumika kama kamba pia
ππππduh Kama nanasi Tena?Hongera ardhi yako ina rutuba. Kwangu migomba ipo shina moja lakini mkungu ulioko pale ni mdogo kama nanasi.
ππππduh Kama nanasi Tena?
Asante kwa muongozo huu.Kiongozi
Jaribu Kuchimba shimo kubwa ni seme fanya meta moja kina na upana;
Weka mbolea ya ngombe au wanyama hadi nusu au ya masalia ya mimea ila iliyo oza vizuri hadi nusu
Changanya na udongo kidogo Otesha mgomba. Kama ni kiangazi mwagilia walau Ndoo moja ya lita 20, mara mbili kwa wiki au pengine mara moja kama upatikanaji wa maji sio rafiki.
Hiyo nusu ya juu iache wazi. Hiyo mbinu niliona huko kanda ya kaskazini
Lazima kujifunza kuwa na bustani nyumbaniHongera sana, mimi pia kupitia JF kuna jamaa alianzisha uzi wa jinsi ya kupanda matunda nyumbani, niliutumia ule ujuzi...
Its five years now matunda hayakauki home, matunda kama..papai, ndizi aina zote, machungwa, miwa, mboga za majani, na nadhani next year tutaanza kula embe...
Halafu kumbe nyumba ikiwa ina greenish inapendeza na kufutia sana...
Unaweza kaa siku nzima unashangaa maua, majani, na miti ya matunda!
Ahsante kwa Jf...ilinipa idea nzuri.
Raha sana mkuu kuna kipindi unakua umefulia hatari unapitia buchani unachukua nyama ya utumbo kg moja tu buku 4 ukifika home mnakula delicious food kama matajiri
Sema utumbo sio nyama ya utumboRaha sana mkuu kuna kipindi unakua umefulia hatari unapitia buchani unachukua nyama ya utumbo kg moja tu buku 4 ukifika home mnakula delicious food kama matajiri