Uchaguzi 2020 Faida tutakazopata Watanzania NCCR Mageuzi atakapokuwa chama kikuu cha upinzani baada ya Oktoba 2020

Uchaguzi 2020 Faida tutakazopata Watanzania NCCR Mageuzi atakapokuwa chama kikuu cha upinzani baada ya Oktoba 2020

Bia yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2020
Posts
6,921
Reaction score
8,321
Tunajua NCCR Mageuzi Ndio chama ambacho upepo unakivumia vizuri baada ya kupita kwenye mawimbi mengi kwa miaka kumi mfululizo!

Kuna kila dalili hawa jamaa ndio wataunda kambi ya Upinzani wakishirikiana na Cuf au ACT Wazalendo

Faida ya NCCR Mageuzi kuwa Chama kikuu cha upinzani

1. Itaharakisha maendeleo kwani hawa watu wanasiasa za kistaarabu na hawana matusi tofauti na upinzani uliopo

2.Hawana historia ya kutumiwa na Mabeberu kuisaliti Nchi tofauti na chama Kilichopo ambacho kimekuwa kikiwatetea Mabeberu badala ya kuwapigania Watanzania

3.kina idadi kubwa ya wasomi refer Masumbuko Lamwai anatajwa kuwa mwanasheria bora kuwahi kutokea kwa Siasa za Upinzani, hivyo watashirikiana na serkali katika kuijenga Nchi

4 Vurugu na lugha mbaya zitaisha bungeni, tutakumbuka kuwa NCCR mageuzi Ndio chama chenye rekodi ya kuwa na wabunge Wengi bungeni kwa wakati moja Lakini hawakuwahi kufanya vurugu bungeni kama Wapinzani waliopo wanaofanya

5.NCCR Mageuzi ina makao makuu bora kabisa hawa waliopo Chama kimepanga kwenye nyumba ya mtu tena ndogo

6.Hakikuwahi kuwadhihaki makaada wake alipoondoka Mrema, Marando hawakumtukana Walisema ni siasa ila wasasa mwanachama akiwakimbia anatukanwa kila aina ya Matusi

7. NCCR Mageuzi kilikuwa chama cha kitaifa Watanzania wote walikiheshimu


Karibuni NCCR Mageuzi Katika ujenzi wa Taifa letu la Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu usajiliwe Jumanne naona una moto kweli. Wenzako walikuja hivihivi leo wako benchi.
Ila eleweka basi we bidada. Mara Tulia kaiteka mbeya, mara NCCR Mageuzi. Sasa tukueleweje? Mbona unakuwa kama mfuniko wa makopo ya maji?

Maana inaingilia tu liwe kopo la Kilimanjaro, liwe la uhai, liwe la Jambo sasa tukueleweje?
Baada ya kuomba Mungu atuondolee hili janga la CIRONA wewe unang'ang'ana kujitoa akili na kujivika uendawazimu tangu Jumanne
 
Neno Zuri Sana Ukiona MwanaCCM anakisifia Chama Cha Upinzani Kama huyu Jamaa gundua chama hicho ni Dhaifu na Hakina Madhara yoyote kwa Wababe wa CCM. Chama Cha upinzani Nyakati Hizi bado tu ni CHADEMA. Hiyo NCCR unayoisifiaTunajua ni CCM- b
 
Tulia nimemzungumzia kama kipenzi cha wana mbeya

Nccr mageuzi nimezungumzia km chama bora cha upinzani
Tangu usajiliwe Jumanne naona una moto kweli. Wenzako walikuja hivihivi leo wako benchi.
Ila eleweka basi we bidada. Mara Tulia kaiteka mbeya, mara NCCR Mageuzi. Sasa tukueleweje? Mbona unakuwa kama mfuniko wa makopo ya maji? Maana inaingilia tu liwe kopo la Kilimanjaro, liwe la uhai, liwe la Jambo sasa tukueleweje?
Baada ya kuomba Mungu atuondolee hili janga la CIRONA wewe unang'ang'ana kujitoa akili na kujivika uendawazimu tangu Jumanne

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NCCR Mageuzi unaijua vizuri

Nyie chadema yenu haijafikia hata nusu ya mafanikio ya Nccr mageuzi
Neno Zuri Sana Ukiona MwanaCCM anakisifia Chama Cha Upinzani Kama huyu Jamaa gundua chama hicho ni Dhaifu na Hakina Madhara yoyote kwa Mijambazi ya CCM. Chama Cha upinzani kwa karne na Karne Ni CHADEMA. Hiyo NCCR Tunajua ni CCMB

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom