Kumbukumbuyatorati !!
Mahesabu uliyopigiwa juu yote hayo ni porojo tu! Sio kwamba huwezi kutengeneza 1B (TZS) kupitia Youtube, inawezekana sana lakini sio rahisi kiasi hicho!
Na wala mapato hayatokani na idadi ya views, kwa maana X Views = US$ Y, HELL NO, ingawaje pia ni kweli kadri unavyokuwa na Views wengi zaidi uwezekano wa kupiga zaidi unaongezeka!!
Aidha, YouTuber X wa Tanzania anaweza kuwa na Views 5M wakati YouTuber Y wa Japan akawa na Views 3 M na Viewers wa Japan wakawa wamengalia matangazo yale yale yaliyoangaliwa na Viewers wa Tanzania kwa urefu ule ule wa muda lakini at the end, usishangae YouTuber wa Japan akawa ameingiza mapata hata mara 3 ya YouTuber wa Tanzania!
Hapo juu inatokana na game of chance!
Kwamba, kama ni tangazo la iPhone X, basi kuna uwezekano wa kila 100 Views za Japan zikafanikisha ununuzi wa iPhone X hata 5 wakati zile Views 100 za Tanzania zikaishia kuangalia mapicha picha tu!
Kutokana na hapo juu, Advertizers wanaweka viwango tofauti vya thamani ya tangazo, na geographical position, ina-matter sana kwenye kufanya maamuzi!
Tuje kwenye swali la msingi! Unapata vipi mapato!
Njia ya kwanza ndo hiyo ya matangazo maarufu kama Google Adsense! Hapa kazi yako kubwa ni kuwa ni kutengeneza contents ambazo unaamini zitavutia watazamaji, and that's it!
Kwavile utakuwa na Adsense code, ina maana Viewer akifungua tu video yako, atakutana na tangazo... lile ambalo baadae unaambiwa SKIP!!
Utakachopata kutokana na tangazo husika itategemea Viewer aliendelea ku-entertain hilo tangazo kwa muda gani! Na itoshe tu kusema kwamba, kuna formula tofauti tofauti hutumika hapa!
Aidha, usishahau suala la kila region kuwa na thamani yake kwa tangazo lile lile!
Njia ya pili ya mapato ni local contracts! Ukishakuwa na YouTube Channel ambayo inatembelewa sana, basi una uwezekano mkubwa wa kupata matangazo ya ndani (sio Adsense)
Hapo juu ni kama unavyoona mfano wa wimbo wa Diamond wa Utanipenda ambao video yake inatanguliwa na tangazo la Dr. Mwaka!
Matangazo ya aina hiyo hapo juu ni maarufu sana kwa mtu kama Millard Ayo!!
ALL IN ALL, kazi ngumu ya YouTube Channel ni content! Suala la content ukilichukulia poa, utaishia kuwa mtu wa copy and paste!!
Ujinga wa copy and paste ni kwamba, idadi ya views lazima iwe ndogo kwa sababu video moja inakuwa iko posted kwa channels zaidi ya 10!
Isitoshe, kadri watu wanavyoona umuhimu wa Adsense, ndivyo wanavyozi kufanya protection kwenye videos zao!!
Ndo hapo unakuta umepakia video saa 2, lakini ukija saa 7, Google wameiondoa kwa sababu kuna mtu ka-report copyright violation!