Ndugu yangu Mzizimkavu huku kwetu Bongo mambo yamekuwa mengi mno hadi tunachanganyikiwa. Mboga za majani ni muhimu kwa afya lakini tule mboga zipi? Kuna mchicha ule wa asili ambao ilielezwa ndio sahihi kwa afya, lakini leo kuna mboga nyingi zinaoteshwa kwenye maabara na zinakuwa kama kuku wa kisasa ambaye analiwa baada ya wiki kuanzia sita tu tangu kutotolewa, kuku hana ladha ya kuku. Mchicha unarefuka mchana na usiku, baada ya wiki mbili unaliwa japo hauna ladha ya mchicha tuliouzoea. Tumechanganyikiwa labda ututofautishie kipi sahihi na kipi feki.