Faida Ya Kuishi Jiji la Geneva

Faida Ya Kuishi Jiji la Geneva

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,957
Wapendwa Kwanza Niwatakie Sabato Njema Yenye Raha Na Baraka Tele.
Nimejuzwa Hivi Karibumi Na Mdau Mmoja Aliyebahatika Kusafiri Nchi Nyingi Mbalimbali Kuwa Kuishi Jiji La ''Geneva'' Kuna Faida Nyingi Sana. Mdau Huyo Alitaja Faida Hizo Kuwa Za Aina 2, Yaani Faida Kubwa Na Faida Ndogo.
Kwa Leo Nitaanza Na Faida Ndogo Kama Ifuatavyo:
1) Usafiri:- Ukijipulizia pafyumu Nyumbani Ukapanda Bus Utafika Kazini Ukinukia Pafyumu.
2) Usafiri:- Mabus Siyo Ya Kugombania Labda Upende Mwenyewe!
3) Usafiri:- Hakuna Kusimama Kwenye Mabus Labda Upende Mwenyewe.
4) Usafiri:- Siyo Rahisi Kusikia Harufu Ya
Jasho Hasa La Kikwapa Kutoka Kwa Abiria Mwingine
5) Bar/ Pub/ Grocery:- Mhudumu Hawezi Kukudai Ulipe Bill Kabla Ya Kuondoka. Bill inalipwa Mteja Akimaliza Kunywa Tena Kwa Mteja Kutoa Taarifa Kwa Mhudumu Kuwa Sasa Anaondoka.
5) Wanawaje Wa Jiji Hill Wengi Ni Warembo Sana Japo Hawako Complicated!!
6) Wanawake Wengi Wa Jiji Hilo Ni Warembo Sana Ila Hawapendi Kwenda Shule Bali Hupenda Kazi Za Uhudumu Wa Bar,Vijihotel, Uhouse Girl N.k
7) Wanawake Wa Jiji Hill Ukiwaona Kwa Mara Ya Kwanza Utadhani WanaMaisha Ya Juu Sana
8)Sio Rahisi Wadada Hao Kukupeleka Wanapoishi!
9) Wakazi Wengi Wa Jiji Hilo Hasa Vijana Hupenda Kuongea Mambo Makubwa Sana Hasa Yale Yanayohusu Mipango Mikubwa Ya Pesa Au Deal Za Hatari. Ukiwa Nae Pub Unaweza Mnunulia Bia Nyingi Sana Ukidhani Ni Tajiri Fulani Hivi. Cha Ajabu Waweza Kukuta Mfukoni Ana Buku Moja Tu Ya Bajaji Na Sio Rahisi Aagize Hata Round Moja Ya Bia.
10) Wengi Wao Hasa Kina Dada Ukiwauliza Wanaishi Wapi Watakwambia Wanaishi Njiro Au Sakina Japo Sio Rahisi Wakupeleke Wanakoishi.
10) Siasa:- Wakazi Wengi Wa Jiji Hilo Hadi Sasa Hawajui Kuwa Nchi Yao InaMfumo Wa Vyama Vingi.Wao WanaChama Kimoja Tu Wanachokijua.
11) Matembezi;- Wengi Wao Wakitembea Sana Wameishia Kwa Sadalah Na Wanaamini Hapo Ndio Mwisho Wa Mipaka Ya Nchi Yao!
12) Siasa;- Wakazi Wa Jiji Hilo Wanaamini Mawazo Yao Ndiyo Mawazo Ya Raia Wote Wa Nchi Yao.
13) Ni Jiji Pekee Ambalo Ukiwa Na Bastola Unaweza Tembea Nayo Hadi Bar,Unahakikisha Kila Mtu Anafahamu Kuwa Unayo Bastola, Ni Sifa Kubwa Watu Wakijua Kuwa Unayo Bastola.
14) Ni Jiji Pekee Hadi Leo Wakazi Wake Wanashindana Kwa Idadi Ya Bia Walizokunywa Jana Yake, Pamoja Na Fedha Walizotumia, Idadi Ya Watu Aliowanunulia Bia, Bila Kusahau Vurugu Alizozifanya Jana Usiku.
15)Tajiri Mkubwa Lazima Awe Na Land cruiser Nyingi.
16) Mwanaume Mjanja Wa Jiji Hilo Lazima Alete Story Za Mererani Ndio Ataheshimika.
17) Mjanja Wa Jiji Hill Akipotea Wiki 2 Akirudi Tu Lazima Adai Alikuwa Machimboni Mererani.
18) Wajanja Wa Jiji Hill Wanazo CV Za Matajiri Wote Wakubwa Na Pia Always Watadai Wanafahamiana Nao Na Pia Mara Nyingi Wanakunywa Nao Pamoja Kila Siku
19)Sehemu Muhimu Za Mtoko:
a) Triple A
b) PinPoint
c) Club D
d) Picnic
e) Ma,,,,,ko Bar
f) Mrina
g) Shivers
h) Babylon
I)


Itaendelea.
Karibuni.
 
pia tusisahau kuwa waswisi ni baadhi ya wazungu wachache ambao bado wanaamini mzungu na mwafrika hawawezi ku coexist,racism is real over there ref Oprah
 
Hawana jeshi lakini kila raia wa nchi hiyo ni mwanajeshi.n'gombe ni wengi kuliko idadi ya binadam nchini uswisi.wanakunywa maziwa sana lakini cholestoral level yao iko chini kuliko nchi yoyote sababu wanafanya zoezi kupita maelezo!kila raia ana zana zake za kijeshi nyumbani kikinuka ujue raia wote watakugeuzia kibao.raia wa hii nchi wana miili mikubwa kama goliath
 
wanaume kwa wanawake wanavaa nguo za kubana matako
 
Daaaah bado unaendelea na mpango wako tu.... ngoja niishie hapa
 
Kuanzia namba 14 kushuka chini nina mashaka ndugu muandishi au ulikuwa una copy na ku pest hivyo ulicopy kitu tofauti..?
 
Hawana jeshi lakini kila raia wa nchi hiyo ni mwanajeshi.n'gombe ni wengi kuliko idadi ya binadam nchini uswisi.wanakunywa maziwa sana lakini cholestoral level yao iko chini kuliko nchi yoyote sababu wanafanya zoezi kupita maelezo!kila raia ana zana zake za kijeshi nyumbani kikinuka ujue raia wote watakugeuzia kibao.raia wa hii nchi wana miili mikubwa kama goliath
Hivi uswiwi kuna triple A,matako bar,sakina,njiro au?
 
KUPITIA THREAD NIMEAMINI HUMU JF, WATU HAWASOMI THREAD NZIMA, WANASOMA TITLE TU HALAFU WANALETA UJUAJI.

MLETA MADA KAMAANISHA ARUSHA NA SWITZ
 
Umesahau Mjengoni pana mziki mtamu sanaaaa
 
OK thanks to you mkuuu lkn mmm nilikuwa napitatu nikakutana na hayo
 
Back
Top Bottom