Faida ya kuishi na mfanyakazi kama rafiki wa karibu

De Opera

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Posts
780
Reaction score
1,664
Mfanyakazi.jpg
Habari za muda huu Wapwa?, ninaimani mnaendelea vizuri. Leo nitazungumza kuhusu kuishi na mtu hasa mfanyakazi awe ni House maid au office worker. Japo hata kwa mtu wa kawaida naye itamgusa pia.

Kuna watu huwa wanalalamika juu ya kutendwa vibaya na wafanyakazi wao, kama vile kutelekezwa(Kutorokwa), na kuibiwa ama hata kufanyiwa jambo baya. Katika tafiti zangu na nilichokiona ni kwamba bosi wengi hawana care nzuri kwa wafanyakazi.

Ukitaka uishi vizuri na mtu/mfanyakazi chakwanza futa dhana ya kumuita, kumchukulia au kumtambulisha kwa watu kuwa 'Huyu ni mfanyakazi wangu', utamfanya awe perfect na afanye kila kitu kwa roho moja.

Huwezi kutendewa au kufanyiwa ubaya naye abaki akitabasamu. Usiishi naye kama yeye ni adui yako. Mjali hata kwa kile asichokuomba kutoka kinywani mwake. Fikiria kuwa kuna muda anahitaji kitu fulani kama wewe ambavyo kunawakati unahitaji kitu fulani.

Mjali kwa matumizi madogo madogo, usingojee apate mshahara tena kwa masimango ile hali ni haki yake.

Faida ya kuishi na mtu/mfanyakazi kama mtu wako wa karibu/rafiki.

1. Hawezi kukuibia

Kuna baadhi ya watu hulalamika na kuwalaumu watu/wafanyakazi kuwa ni wadokozi, wanaficha pesa.

Niseme tu kuwa mazingira kama haya yanatengenezwa na bosi mwenyewe. Ndio, kuna baadhi ya wafanyakazi ni tabia yao ila kwa asilimia 2% tu. Wengi ni wale wanaojitafutia maisha tu wala hawana makuu.

Kama ulivo wewe kuna muda unahitaji vocha, kuvaa upendeze hata yeye anahitaji pia. Mjali tu hutosikia anaficha pesa au kukuibia.

2. Hawezi kuwa kibaraka wa watesi wako.
Muda wote kumbuka, unapokuwa unaishi na mfanyakazi kwa asilimia 80% anafahamu mambo yako na maisha yako ya siri. Tabia zako anafahamu vizuri tu.

Sasa kama kuna watu wabaya/adui wanaweza kukudhuru au kuharibu mambo yako kupitia yeye, lakini kama unaishi naye vizuri, aah! utajuzwa kila kinachoendelea.

3. Atathamini na kujali vitu kama vyakwake.
Kiukweli kama unataka vitu vyako viwe katika mikono salama, basi kitu cha muhimu ni kuishi na mfanyakazi kama rafiki wa karibu sana. Atatunza na kujali kila chochote chako.

4. Ni ngumu kufanya ukatili dhidi ya watu wako
Unapoishi na mfanyakazi kama mko vitani naye hutengeneza spiritual reply attacks sasa hii ni mbaya sana kwa sababu itaathiri ikiwa ni sanjari na kufanya ukatili kwa watoto au hata wageni wanaokutembelea.

Fikiria wewe unaondoka nyumbani unamuacha na wanao, unadhani atamakinika nao? Kila jambo atakalokuwa akilifanya, atalifanya kwa kisasi.

Mimi natamatisha hapa leo, ila kumbuka kupiga stori za hapa na pale. Jaribu kumueleza hata huwa unajihisije juu yake (simaanishi kimapenzi).

Mfano, unaweza msifu tu kwa kile anachokifanya ili naye ajisikie kuwa yuko sawa, hajakosea. Usikae tu kimya atashindwa kujiamini na kujiuliza kichwani mwake kuwa je anachofanya ni sahihi kweli?.

Mimi nakutakia siku njema.
 
Kuna kunguru pori mmoja nilimfanyia yote hayo ila mwisho wa siku aliniletea wahuni wakanisafisha mpaka vijiko
Huyo alikuwa mwizi wa kuzaliwa. Na hao ndio huwa wanasababisha hata waliowema waonekane ni wezi pia.

Mi pia nilikuta vijana wameosha ofisi nzima. Nilichobakisha tu ni email na password. Vijana nimewafundisha mambo ya IT. Nikaona wameiva, nikawaachia ofisi nikarudi Tz. Mara wakaacha kupatikana. Ikabidi nirudi ofisi ilikuwa Nairobi. Kukuta wameosha kila kitu. Ila niliwapata. Walivotupa sim card zao wakajua wamemaliza. Mimi nikadeal na IMEI na uzuri kwenye vifaa nilikuwa nimefunga Tracker.
 
Kuna kunguru pori mmoja nilimfanyia yote hayo ila mwisho wa siku aliniletea wahuni wakanisafisha mpaka vijiko
Hajui huyu....mi nikiongeza mtoto atakuwa ndiyo begi langu...muda wa kazi vingirisha kwenye box...piga kazi huku uachungulia.... walimu wanaosubiri vipindi vyao waendelee kubembeleza....nikifika home najibebisha nae.Mabinti hapana
 
Dah, mabinti wenye tamaa wameharibu sifa za mabinti wema. Ila kuna binti wa kazi unaweza kubahatisha ukaishi naye yaani kama ndugu. Hadi watu wanakuwa wanakuuliza huyo ni nduguyo.
 
Ni kweli kabisa,wema wapo mkuu
 
Ni kweli kabisa,wema wapo mkuu
Kuna kipindi nilipata binti kutoka interior kule alikuwa poa sana. Msafi balaa ila sasa usiku kasheshe. Unaamka asubuhi unakuta umegeuzwa. Kichwa miguuni, miguu kichwani. 😂
 
🤣🤣🤣🤣🙌 Maji ukaita mma
 
Habari za muda huu Wapwa?, ninaimani mnaendelea vizuri. Leo nitazungumza kuhusu kuishi na mtu hasa mfanyakazi awe ni House maid au office worker. Japo hata kwa mtu wa kawaida naye itamgusa pia.

Kuna watu huwa wanalalamika juu ya kutendwa vibaya na wafanyakazi wao, kama vile kutelekezwa(Kutorokwa), na kuibiwa ama hata kufanyiwa jambo baya. Katika tafiti zangu na nilichokiona ni kwamba bosi wengi hawana care nzuri kwa wafanyakazi.

Ukitaka uishi vizuri na mtu/mfanyakazi chakwanza futa dhana ya kumuita, kumchukulia au kumtambulisha kwa watu kuwa 'Huyu ni mfanyakazi wangu', utamfanya awe perfect na afanye kila kitu kwa roho moja.

Huwezi kutendewa au kufanyiwa ubaya naye abaki akitabasamu. Usiishi naye kama yeye ni adui yako. Mjali hata kwa kile asichokuomba kutoka kinywani mwake. Fikiria kuwa kuna muda anahitaji kitu fulani kama wewe ambavyo kunawakati unahitaji kitu fulani.

Mjali kwa matumizi madogo madogo, usingojee apate mshahara tena kwa masimango ile hali ni haki yake.

Faida ya kuishi na mtu/mfanyakazi kama mtu wako wa karibu/rafiki.

1. Hawezi kukuibia

Kuna baadhi ya watu hulalamika na kuwalaumu watu/wafanyakazi kuwa ni wadokozi, wanaficha pesa.

Niseme tu kuwa mazingira kama haya yanatengenezwa na bosi mwenyewe. Ndio, kuna baadhi ya wafanyakazi ni tabia yao ila kwa asilimia 2% tu. Wengi ni wale wanaojitafutia maisha tu wala hawana makuu.

Kama ulivo wewe kuna muda unahitaji vocha, kuvaa upendeze hata yeye anahitaji pia. Mjali tu hutosikia anaficha pesa au kukuibia.

2. Hawezi kuwa kibaraka wa watesi wako.
Muda wote kumbuka, unapokuwa unaishi na mfanyakazi kwa asilimia 80% anafahamu mambo yako na maisha yako ya siri. Tabia zako anafahamu vizuri tu.

Sasa kama kuna watu wabaya/adui wanaweza kukudhuru au kuharibu mambo yako kupitia yeye, lakini kama unaishi naye vizuri, aah! utajuzwa kila kinachoendelea.

3. Atathamini na kujali vitu kama vyakwake.
Kiukweli kama unataka vitu vyako viwe katika mikono salama, basi kitu cha muhimu ni kuishi na mfanyakazi kama rafiki wa karibu sana. Atatunza na kujali kila chochote chako.

4. Ni ngumu kufanya ukatili dhidi ya watu wako
Unapoishi na mfanyakazi kama mko vitani naye hutengeneza spiritual reply attacks sasa hii ni mbaya sana kwa sababu itaathiri ikiwa ni sanjari na kufanya ukatili kwa watoto au hata wageni wanaokutembelea.

Fikiria wewe unaondoka nyumbani unamuacha na wanao, unadhani atamakinika nao? Kila jambo atakalokuwa akilifanya, atalifanya kwa kisasi.

Mimi natamatisha hapa leo, ila kumbuka kupiga stori za hapa na pale. Jaribu kumueleza hata huwa unajihisije juu yake (simaanishi kimapenzi).

Mfano, unaweza msifu tu kwa kile anachokifanya ili naye ajisikie kuwa yuko sawa, hajakosea. Usikae tu kimya atashindwa kujiamini na kujiuliza kichwani mwake kuwa je anachofanya ni sahihi kweli?.

Mimi nakutakia siku njema.
Somo zuri sana kwa mabosi makatili
 
Tatizo kuna baadhi ya watu, ukiwatendea wema sana anakuona mjinga.
Kuna siku mida ya saa saba usiku nikakutana na binti wa miaka 7 hivi, anaomba msaada hana pakwenda. Nikafikiria dunia ya sasa imeharibika, ikabidi nimpeleke kwa mwenyekiti. Mwenyekiti naye anasema nenda naye tu, wewe sio ndio umemuona huko. Ikabidi nimpeleke kituo cha polisi. Kiukweli sahivi hata utende wema namna gani.
 
Back
Top Bottom