Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,734
- 140,476
Watu wakikukataa usichukie au kupanga kisasi, chukulia kama kupewa changamoto ya kupambana. Usiweke vinyongo na ndugu au jamaa waliokukataa au kukudharau na pengine kukataa kuwasaidia huko mbeleni. Hapana, kukataliwa inaweza kukupa faida zaidi wewe kuliko wao, lakini tu kama utaweka jitihada na kupambana ili usiendelee kukataliwa.
Ninakupa experience ndogo.
Juzi niliunguza kifaa cha umeme. Nikampigia jamaa aliyeniuzia akaniambia kinauzwa laki 2. Nilipomuomba anipunguzie akanijibu jeuri kwamba hafanyi biashara na watu masikini. Nikabaki kumshangaa kwa sababu wakati ananiuzia awali alikuwa na customer care nzuri sana. Kiasi kwamba hata kifaa alikituma mwenyewe toka Dar mpaka Mwanza. Nikiwa namsihi awe na kauli nzuri kwa wateja akakata simu.
Nilimsamehe huyo jamaa, badala yake niliacha kikutumia kile kifaa kusubiri nipate safari ya Dar ili nikatafuta wauzaji wengine kwa sababu siwezi tena kuwasiliana na yule muuzaji jeuri. Baada ya siku 2 nikapata wazo nitafute mafundi redio labda wataweza kukifufua. Nikapata mmoja akaniambia hizi ni kazi kuna mtaalamu mmoja akishindwa huyo basi kanunue kipya tu.
Jioni ya leo nimetoka kuchukua kifaa kwa huyo mtaalamu. Kimepona kwa gharama ya 25,000 tu na kifaa kinapiga kazi. Lakini pia nikawa nimepata fundi ikiwa ile mashine itazingua siku za mbeleni.
Kwa hiyo kukataliwa kwangu imekuwa faida zaidi kwangu. Ninamshukuru sana aliyenikataa