Faida ya kula Matunda

Faida ya kula Matunda

muzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,457
1293a6ea678dcba2318f16bfe77d55fe2284c335.jpeg

Matunda yana faida nyingi sana za kiafya mwilini. Ukiachana na ladha tamu inayotokana na kula matunda, kila mtu anashauriwa ale matunda tofauti yasiyopungua matano (5) kwa siku ili kupata faida zote mwilini. Faida kuu za matunda ni kuzuia maradhi, kurutubisha kinga ya mwili, kupunguza sukari kwenye damu, kungarisha ngozi, kuleta nguvu na kuleta mafuta asilia kwenye mwili.

Watu wanaopendelea kula matunda na mboga za majani kama sehemu yao kubwa ya mlo wa kila siku hujenga kinga madhubuti za mwili dhidi ya magonjwa. Matunda yana virutubisho asilia ambavyo ni mahususi katika kujenga mwili na kuufanya kuwa na afya njema. Matunda hubeba virutubisho muhimu kama potasiam, vitamin C, vitamin A, nyuzi nyuzi (fiber) na folic acid.

Ulaji wa matunda unasaidia mwili hukufanya kupata faida zifuatazo:

Yanapunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi
Yanakinga mwili dhidi ya aina za saratani
Nyuzi nyuzi (fiber) za kwenye baadhi ya matunda kama maembe zinasaidia kulinda dhidi ya magojwa kama mshituko wa moyo (heart attack), fetma na kisukari. Lakini pia inasaidia kupunguza madhara ya uvimbe unaotokana na kuwa na chumvi nyingi mwilini.

Kula matunda yenye potasiam kama ndizi na apricot kwa wingi yanasaidia kupunguza magonjwa ya shinikizo la damu. Matunda aina hizi husaidia pia kupunguza mawe kujaa kwenye figo.

Vitamin C ni muhimu katika mwili kwasababu inasaidia ukuaji na utengenezaji wa tishu za mwili. Mfano ni meno na fizi. Vitamic C inasaidia pia uchocheaji wa uponaji wa vidonda kwa haraka. Vitamin C inapatikana kwenye matunda mengi machachu, mfano machungwa, limao n.k

Folic acid inasaidia kutengeneza chembe hai nyekundu za damu mwilini. Wanawake wajawazito au walio kwenye umri wa uzazi wanashauriwa sana kula vyakula vyenye folic acid kwa wingi ili kusaidia ukuaji wa mototo tumboni na kudhibiti dhidi ya magonjwa.

Ni wazi kuwa huwezi kupata matunda ya aina yote kwa wakati mmoja, vilevile matunda mengi uanapatikana katika kipindi fulani za msimu wa mwaka. Matunda aina fulani kama sio msimu wake basi huwa yanuzwa kwa bei ya juu sanaa.

Hivyo inashauriwa kwa kipindi/msimu ambacho matunda fulani yanapatika, kula kula kwa wingi, tukihamia msimu mwingine na matunda mengine kula kwa wingi. Hi husaidia mwili kuwweka reserve mwilili hata ukikosa kipindi fulani lakini kuna madini akiba yaliyohifandhiwa mwilini.

"KULA MATUNDA WAKATI WOTE USISUBIRI KUAMBIWA NA DAKTARI"
 
matunda pia yanauwezo w kukupa ugonjw wa kisukar sababu yanaingia kwenye damu haraka bila kumengenyw sana mkibisha nitafafanua kula kias tafadhali
 
matunda pia yanauwezo w kukupa ugonjw wa kisukar sababu yanaingia kwenye damu haraka bila kumengenyw sana mkibisha nitafafanua kula kias tafadhali
M nabisha em fafabua tufaidike tusikalili
 
fafanua ni matunda yapi au unazungumzia juisi
kuna kitu kinaitwa bloodsugar crush hii ni hali inayotokana na kiwango kikubwa cha sukari kuingia kwenye damu kwa gafla ikitokea hali hii mwili unapambana ili kuondoa sukari hii haraka ndani ya damu kwani sukar ikijaa kitu cha kwanza ni uchovu usingiz au uvivu weng wanajua hii kitu wakishakula kwani hiona hali hii maana sukar imepanda ukienda kulala au kukaa ndio kongosho inatoa insulin ili kuondoa sukar sasa kongosho itatoa insulin kila siku mpaka itachoka na kupata ugonjwa wa kisukari

mwili wako kimiminika pekee kitachoingia bila kuleta madhara ni maji tu kwan hayana sukar juisi ni harakati za wazungu kuraisisha mambo ila side effect ni kujaza sukar kwa pamoja hivyo mwili inapata tabu kuiondoa

ndiz ina gram 15 za sukar
tikiti gram 25
chungwa gramu 18
karot gram 2
na nk soda ina gram 40 sawa na vijiko kumi vya sukar vya chai
mtu anaetumia soda kila siku baada ya miaka tano atakua na hatar ya kupata ugonjwa huu wa sukar
sababu ataingiza zaid ya gramu 50 au 45 kila siku ukijumlisha na za chakula cha kawaida

sasa chukulia umekula chakula na kula machungwa mawili jumla 36 gramu kisha ndizi mbili jumla 30 plus 36 ni 66 ukipata na tikit itakua ni zaid ya 70 sasa wewe tunasema hutosubir miaka tano bali itabidi uchukue miak mitatu tu kuanza kupata ugonjwa huu kwani utakua umeingiza gramu zaid ya 70 sawa na vijiko 20 vya sukar..
 
Mmmmhh mkuu kweli ndo sayansi lakni sasa inakanganya sana uleje sasa???
kula kias na usichanfanye matunda kula chungwa moja mchana jion tunda lingine sio meng kwa pamoja otherwise ule kisha ufanye mazoez kwa nusu saa ili kuchoma sukar ipungue japo tatu au nne
 
kuna kitu kinaitwa bloodsugar crush hii ni hali inayotokana na kiwango kikubwa cha sukari kuingia kwenye damu kwa gafla ikitokea hali hii mwili unapambana ili kuondoa sukari hii haraka ndani ya damu kwani sukar ikijaa kitu cha kwanza ni uchovu usingiz au uvivu weng wanajua hii kitu wakishakula kwani hiona hali hii maana sukar imepanda ukienda kulala au kukaa ndio kongosho inatoa insulin ili kuondoa sukar sasa kongosho itatoa insulin kila siku mpaka itachoka na kupata ugonjwa wa kisukari

mwili wako kimiminika pekee kitachoingia bila kuleta madhara ni maji tu kwan hayana sukar juisi ni harakati za wazungu kuraisisha mambo ila side effect ni kujaza sukar kwa pamoja hivyo mwili inapata tabu kuiondoa

ndiz ina gram 15 za sukar
tikiti gram 25
chungwa gramu 18
karot gram 2
na nk soda ina gram 40 sawa na vijiko kumi vya sukar vya chai
mtu anaetumia soda kila siku baada ya miaka tano atakua na hatar ya kupata ugonjwa huu wa sukar
sababu ataingiza zaid ya gramu 50 au 45 kila siku ukijumlisha na za chakula cha kawaida

sasa chukulia umekula chakula na kula machungwa mawili jumla 36 gramu kisha ndizi mbili jumla 30 plus 36 ni 66 ukipata na tikit itakua ni zaid ya 70 sasa wewe tunasema hutosubir miaka tano bali itabidi uchukue miak mitatu tu kuanza kupata ugonjwa huu kwani utakua umeingiza gramu zaid ya 70 sawa na vijiko 20 vya sukar..
Nafikiri tupate wataalamu wengine watusaidie hasa kwenye hili la matunda tuachane na juice na soda ambazo zipo wazi. Watujibu kula matunda mengine kunaweza kuletea kupata kisukari???? wapi@mzizimkavu, kongosho etc.??
 
ni vizur waje tufanye debate hapa unajua hivi vitu watu hawaambiwi side effect kwa sababu za kibiashara na waafrika weng hawapend kusoma au kujifunza
 
Back
Top Bottom