Faida ya kupakia mizigo kwenye gari unayo agiza nje, unapunguza gharama ya usafiri

Faida ya kupakia mizigo kwenye gari unayo agiza nje, unapunguza gharama ya usafiri

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Kwa wale wanao agiza magari nchi za Japan,China,Singapore,UK,Canada na USA kipindi unapo agiza gari kama umenunua bidhaa nyingine mfano spare,electronics,nguo na machine ni vyema ukapakia ndani ya gari uliagiza ili kupunguza gharama za kusafirisha hizo bidhaa kwenye meli nyingine.

Unachotakiwa kufanya ni baada ya kununua gari kutoka kwa dealer kwenye nchi husika, inabidi utoe taarifa kuna mizigo utaipakia kwenye gari yako. Njia sahihi na salama inabidi mizigo itayopakiwa iandaliwe parking list hii itaonyesha ni vitu gani vimepakiliwa. Kama itawezekana anayepakia aandae loading report hii itaonyesha picha ya kila mzigo kabla na baada ya kupakiwa hii usaidia endapo kuna hupotevu wa mzigo.

Changamoto inayowakumba wengi baada ya gari kufika ni kufikiri mzigo ulipo ndani ya gari hautakiwi kulipiwa port charges na kodi.

Mzigo utaopakiwa ndani ya gari unaweza ukawa una Bill of Lading au hauna. Mzigo unaweza ukaunganishwa na Bill of Lading ya gari hivyo ukimpa kazi wakala wa Forodha haitomsumbua kwenye kufatilia malipo ya kodi na bandari. Mzigo pia unaweza ukawa na Bill of Lading yake na gari pia ina Bill of Lading yake hii haina shida.

Wengi hutumia njia ya Bill of Lading ya gari kuwa documented na mizigo anayopakiwa inakuwa haipo kwenye documents ya gari (unmafested cargo) na huwa hawaweki taarifa za vitu gani vilipakiwa.

Hii sio kosa kisheria ni njia halali na inatakiwa ulipe gharama za bandari na kodi stahiki wakati wa kutoa gari yako, gari italipiwa kodi yake na mizigo iliyo ndani.

Wenzetu wa Zambia,Rwanda,Malawi na DRC hutumia njia hii kuagiza gari na vifaa vya nyumbani,spare na mizigo ya biashara. Pia siku za karibuni hata watanzania wanao agiza maroli na basi za kichina hutumia njia hii kuagiza spares na vifaa kisha kupakia kwenye gari husika aliloagiza.
 
Hairuhusiwi mkuu. Sheria hairuhusu ata spare tu mfano taa au tyre.

Unless uagize kwa container sio RORO.

Ngoja tujifunze kama kuna njia ya ujanja tufanye mambo.
Inaruhusiwa mizigo inawekwa kwenye gari ndogo, mabasi na maroli. Wengi huwa wanataka kufanya ujanja haiwi manifested ili watoe free na mtu hampi taarifa sahihi ya vilivyo kwenye gari. Gari inapokuwa tayari kutolewa Clearing Agent anakuwa kalipia kodi za Gari tu, watu wa Motor vehicles DPW humpa taarifa ya vitu vilivyo ndani na hawezi pita getini na hivyo vitu wakati release order inaonyesha gari tu ndio imelipiwa kodi. Hivyo anazuiliwa au vitu vishuke vilipiwe port charges na kodi
 
Hairuhusiwi mkuu. Sheria hairuhusu ata spare tu mfano taa au tyre.

Unless uagize kwa container sio RORO.

Ngoja tujifunze kama kuna njia ya ujanja tufanye mambo.
Shipping line chache za America na Australia ndio haziruhusu sababu ya Usalama. Na Australia sheria yao inataka ukiagiza Toyota Land Cruiser basi ndani uweke parts za gari yako na sio model nyingine hata kama ni Toyota, wenzetu pia waliweka katazo la mizigo mingine baada ya biashara haramu kushamiri.

Hapa hapa Bongo kwa RoRo gari ndogo zinakuja na TV,Engine,Bags hata ukienda kesho asubuhi unaziona.
 
Back
Top Bottom