Faida ya nchi kuwa katika uchumi wa kati ni nini?

Huu upuuzi wanatumiaga katika kutuchora tu hawa mafala wa ulaya.... Ila hauna mantiki yoyote.... Pesa haipo kwa mwananchi so kimsingi watu wanataabika..... Sasa kuwa nchi ya tatu haina faida yoyote kwetu in that case...
Kenya iko kipato Cha Kati unafikir wanatimiza hicho kigezo chako mkuu...?
Zambia,Botswana,Cameroon nazo unafikiri wako huko kama hujaenda Zambia pitia tunduma
 
Huu upuuzi wanatumiaga katika kutuchora tu hawa mafala wa ulaya.... Ila hauna mantiki yoyote.... Pesa haipo kwa mwananchi so kimsingi watu wanataabika..... Sasa kuwa nchi ya tatu haina faida yoyote kwetu in that case...
Mkuu elewa bas vigezo vinavyotumika kucategorise ndyo ulaumu au ubishe hivo vigezo vyako havitumiki....heeeh!!..

Kama unasikiliza redio jion walikua wanachambua kwene 88.1fm ungeelewa
 
Huu upuuzi wanatumiaga katika kutuchora tu hawa mafala wa ulaya.... Ila hauna mantiki yoyote.... Pesa haipo kwa mwananchi so kimsingi watu wanataabika..... Sasa kuwa nchi ya tatu haina faida yoyote kwetu in that case...
Kwa hiyo mkuu hii ni sawa na hakuna na haina faida yeyote
 
Sawa bila kujali ni vigezo gani vimetumika, kutangazwa tu kua Tz ni nchi ya uchumi wa kati ina faida gani kwa sisi wananchi wa kawaida ?,
I mean labda kama kuna exposure yeyote labda n.k
 
Uzalishaji unavyokuwa mpaka ziada ya kuuza nje kwa wingi, pato la kigeni linaongezeka na ajira kwa wazawa. Mambo yakisimamiwa vizuri kama awamu hii uchumi utazidi kuimarika
 
Uzalishaji unavyokuwa mpaka ziada ya kuuza nje kwa wingi, pato la kigeni linaongezeka na ajira kwa wazawa. Mambo yakisimamiwa vizuri kama awamu hii uchumi utazidi kuimarika
Hapa kdogo nimepata mwanga
 
Shida ya nchi yetu ni moja.

Utajiri wa kutupwa.

Na ufukara wa kutupwa.

Gap ni kubwa mno.

Anyway kimsingi kila mtu ashinde mechi zake.
 
Shida ya nchi yetu ni moja.

Utajiri wa kutupwa.

Na ufukara wa kutupwa.

Gap ni kubwa mno.

Anyway kimsingi kila mtu ashinde mechi zake.
Sifa ya ubepari
 
Nimeona wanakiengua sana hicho kipengere kwamba ni uchumi wa kati wa chini (Lower Middle Income)
Haya mambo yana diplomasia zake, diplomasia ambazo kama huzijui, unaweza kutukanwa, ukafurahia na kufanya sherehe ya kuadhimisha kutukanwa.

Wanasiasa wanajua hili, ila wanatumia habari hizi kama mtaji wa kisiasa.

Kilichofanyika ni kama wameondoa category ya nchi masikini, wakaziita nchi zinazochipukia masikini.

Fatma Karume alitoa screenshot inaelezea hili.

Zaidi, hizi figures hazioneshi ukweli wa umasikini. Rais wa Namibia analalamika nchi yake inaitwa "upper middle income" wakati utajiri mwingi unashikiliwa na 5% ya watu, kina Bakhressa wachache wa Namibia wanapandisha sana average ya nchi nzima.

Namibia ina watu wachache, idadi ya watu wa mkoa wa Dar na viunga vyake tu ni kama mara mbili ya idadi ya watu wa nchi nzima ya Namibia. Rais wao analalamika GDP per capita ya $5,700 ni kubwa sana, imepandishwa na matajiri wachache,wakati wananchi wake wengi ni masikini.

Huyu rais kama angekuwa anataka sifa, angejisifia kwa namba kubwa hii, lakini anaelewa kwamba hii average inaficha umasikini wa wengi. Sisi hata $1,500 GDP per capita hatujafikia, tunataka kusheherekea.

Na hapa Tanzania ni hivyo hivyo. Vijijini kuna watu wengi sana hata hiyo GDP Per Capita ya $1000 hawapati, wengi sana wanacheza kwenye nusu ya hiyo.

Yani pato la mtu la mwaka mzima linakuwa sawa na shopping ya weekend moja, au bajeti ya kununua uturi ya mwaka Marekani.

Marekani umeenda mbali, hata hapo Mauritius tu wametuacha mbali sana.

Halafu tunasheherekea nini hapo sasa?
 
Faida zake ni kama ifuatavyo
1. Hii level inaisaidia nchi kuwa huru kujipangia matumizi yake binafsi bila kuingiliwa na mataifa makubwa kimsingi huwa wanaweza kukuwekea vikwako lengo likiwa ni kuwaelekeza kuwa na matumiz sahihi ya rasilimali

2. Pia inaiongezea nchi thamani na kuwa na uwezo wa kukopesheka ( credit worthiness) kwani inaonyesha kuwa na ukwasi wa kutosha kujiendesha. Endapo itahitaji kukopa

3. Kuwa katika lower middle income nchi inakuwa imepunguza kiwango cha kukopa kutoka mataifa mengine ukwasi ilionao unaiwezesha kujiendesha.
Hizo nimezipata baada ya kupata balimi 4 za moto ngoja niendelee nazo mpka zifike 8 nitaongeza zingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji123][emoji123]
 

Mbaya zaidi hata hiyo daraja tumepewa tunajisifu nali ni kama tumejikuta tu.

Sawa na tulivyobahatika kutoshambuliwa na maafa ya Corona na tunajisifu tumepambana nayo na kuidhibiti.

Kwanza hii kuna baadhi ya malipo wanayofanya watu kwenye baadhi ya mambo yataenda juu kwakuwa tutawekwa kwenye kundi la nchi za uchumi wa chini wa kati.
 
Kuna vitu viwili tofauti watu wanachanganya, Economic growth( ukuaji wa uchumi) na Economic development ( Maendeleo ya uchumi): Kwa Sasa Tanzania ilicho achieve ni Economic growth ambayo hii upimwa kwa kuangalia uzalishaji wa bidhaa za ndani na upatikanaji wa huduma kama Elimu, usafiri, matibabu na kadhalika, ambapo hii ni kweli maana Kuna ongezeko la hivyo vitu ukilinganisha na miaka mitano iliyopita coz now Elimu ni bure, miunndo mbinu imeongezeka pamoja na vituo vya afya:

Economic development ( Maendeleo ya Uchumi) hiki upimwa kwa kuangalia ubora wa maisha ya watu na kipato chao, kwa Sasa Tanzania bado hatujafikia hii level maana Ukuaji wa Uchumi( Economic growth) haimaanishi watu watakua na pesa mfukoni au kua na nafuu ya maisha. Kiuhalisia kufikia Economic development bado Kuna vitu vingine inabidi tuvi achieve, hapo ndo nafuu kubwa ya maisha itaonekana.

KUMBUKA: Inawezekana kukua kiuchumi bila Maendeleo ya kiuchumi Ila haiwezekani kua na Maendeleo ya kiuchumi bila kukua kiuchumi.
 
Moja ya faida kubwa ni kwamba kwa Sasa ni rahisi zaidi kuwafikia watu tofauti kwa muda mfupi, hii ni kutokana na uwepo wa miundombinu: hivyo kwa wafanyabiashara na wasafirishaji ni rahisi kuwafikia wateja wengi zaidi ukilinganisha na hapo nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…