Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kenya iko kipato Cha Kati unafikir wanatimiza hicho kigezo chako mkuu...?
Zambia,Botswana,Cameroon nazo unafikiri wako huko kama hujaenda Zambia pitia tunduma
Kuna tofauti kati ya uchumi wa kati na uchumi wa kati wa chini.
Mkuu elewa bas vigezo vinavyotumika kucategorise ndyo ulaumu au ubishe hivo vigezo vyako havitumiki....heeeh!!..Huu upuuzi wanatumiaga katika kutuchora tu hawa mafala wa ulaya.... Ila hauna mantiki yoyote.... Pesa haipo kwa mwananchi so kimsingi watu wanataabika..... Sasa kuwa nchi ya tatu haina faida yoyote kwetu in that case...
Kwa hiyo mkuu hii ni sawa na hakuna na haina faida yeyoteHuu upuuzi wanatumiaga katika kutuchora tu hawa mafala wa ulaya.... Ila hauna mantiki yoyote.... Pesa haipo kwa mwananchi so kimsingi watu wanataabika..... Sasa kuwa nchi ya tatu haina faida yoyote kwetu in that case...
Sawa bila kujali ni vigezo gani vimetumika, kutangazwa tu kua Tz ni nchi ya uchumi wa kati ina faida gani kwa sisi wananchi wa kawaida ?,Hilo ndilo la kustaajabisha. Unajua katika kupima level ya maendeleo kuna namna tofauti. Wapo ambao hupima shughuli za ukuaji wa miundombinu kama barabara, reli, viwanja vya ndege, bandari, majingo ya kutolea huduma mfano hospitali, mashule, na maofisi, na kadhalika.... Hii inaweza kuiweka nchi katika daraja aidha la nne, tatu, pili au moja kutokana na namna wanawekeza pesa yao au thamani ya mtaji katika hizo miundo mbinu.
Lakini pia kuna namna wanakadiria level ya uchumi kwa kupima kipato cha wastani. Mfano wanachukua kiwango cha pato la jumla la taifa wanagawanya kwa idadi ya nguvu kazi wanapata kipato cha wastani ambacho ndicho hutumika kukadiria pato la mtu kwa wastani na kusema ana uwezo ama la. kimsingi hii me sikubaliani nayo sababu tunaweza katika watu 100,utajiri umeshikwa na watu watano tu sisi wengine tunaganga njaa tu.... Hapo huwezi sema tumefaidika....
Haya mambo yana diplomasia zake, diplomasia ambazo kama huzijui, unaweza kutukanwa, ukafurahia na kufanya sherehe ya kuadhimisha kutukanwa.Nimeona wanakiengua sana hicho kipengere kwamba ni uchumi wa kati wa chini (Lower Middle Income)
[emoji123][emoji123]Faida zake ni kama ifuatavyo
1. Hii level inaisaidia nchi kuwa huru kujipangia matumizi yake binafsi bila kuingiliwa na mataifa makubwa kimsingi huwa wanaweza kukuwekea vikwako lengo likiwa ni kuwaelekeza kuwa na matumiz sahihi ya rasilimali
2. Pia inaiongezea nchi thamani na kuwa na uwezo wa kukopesheka ( credit worthiness) kwani inaonyesha kuwa na ukwasi wa kutosha kujiendesha. Endapo itahitaji kukopa
3. Kuwa katika lower middle income nchi inakuwa imepunguza kiwango cha kukopa kutoka mataifa mengine ukwasi ilionao unaiwezesha kujiendesha.
Hizo nimezipata baada ya kupata balimi 4 za moto ngoja niendelee nazo mpka zifike 8 nitaongeza zingine
Sent using Jamii Forums mobile app
Haya mambo yana diplomasia zake, diplomasia ambazo kama huzijui, unaweza kutukanwa, ukafurahia na kufanya sherehe ya kuadhimisha kutukanwa.
Wanasiasa wanajua hili, ila wanatumia habari hizi kama mtaji wa kisiasa.
Kilichofanyika ni kama wameondoa category ya nchi masikini, wakaziita nchi zinazochipukia masikini.
Fatma Karume alitoa screenshot inaelezea hili.
Zaidi, hizi figures hazioneshi ukweli wa umasikini. Rais wa Namibia analalamika nchi yake inaitwa "upper middle income" wakati utajiri mwingi unashikiliwa na 5% ya watu, kina Bakhressa wachache wa Namibia wanapandisha sana average ya nchi nzima.
Namibia ina watu wachache, idadi ya watu wa mkoa wa Dar na viunga vyake tu ni kama mara mbili ya idadi ya watu wa nchi nzima ya Namibia. Rais wao analalamika GDP per capita ya $5,700 ni kubwa sana, imepandishwa na matajiri wachache,wakati wananchi wake wengi ni masikini.
Huyu rais kama angekuwa anataka sifa, angejisifia kwa namba kubwa hii, lakini anaelewa kwamba hii average inaficha umasikini wa wengi. Sisi hata $1,500 GDP per capita hatujafikia, tunataka kusheherekea.
Na hapa Tanzania ni hivyo hivyo. Vijijini kuna watu wengi sana hata hiyo GDP Per Capita ya $1000 hawapati, wengi sana wanacheza kwenye nusu ya hiyo.
Yani pato la mtu la mwaka mzima linakuwa sawa na shopping ya weekend moja, au bajeti ya kununua uturi ya mwaka Marekani.
Marekani umeenda mbali, hata hapo Mauritius tu wametuacha mbali sana.
Halafu tunasheherekea nini hapo sasa?
Kuna vitu viwili tofauti watu wanachanganya, Economic growth( ukuaji wa uchumi) na Economic development ( Maendeleo ya uchumi): Kwa Sasa Tanzania ilicho achieve ni Economic growth ambayo hii upimwa kwa kuangalia uzalishaji wa bidhaa za ndani na upatikanaji wa huduma kama Elimu, usafiri, matibabu na kadhalika, ambapo hii ni kweli maana Kuna ongezeko la hivyo vitu ukilinganisha na miaka mitano iliyopita coz now Elimu ni bure, miunndo mbinu imeongezeka pamoja na vituo vya afya:Habari wakuu!
World Bank wametangaza kua Tanzania kwa sasa ni nchi ya uchumi wa kati, sasa kutokana na taarifa hii sisi kama wananchi taarifa hiyo inaweza kuwa na faida gani kwetu kiuchumi (kwa mtu mmoja mmoja) ?
Na je, sisi kama vijana tunaweza kufanya nini cha kutusaidia kujikwamua kiuchumi kutokana na taarifa hii?