Faida za kiafya za kutumia uyoga

Faida za kiafya za kutumia uyoga

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
1504988_10153947544720198_106286070_n.jpg


1468695_10153947548350198_962233413_n.jpg


10014703_10153947548980198_2100946504_n.jpg


Kwa mujibu wa mtandao wa www.organicfacts.net uyoga una vitamini na aina nyingi za madini.Baadhi ya virutubisho vilivyothibitishwa kuwemo

kwenye uyoga ni pamoja na Vitamini B2, B3, B5, B6, B Complex pamoja na madini ya Potasiamu na ‘Phosphorus'.

Uyoga ni miongoni mwa vyakula adimu sana duniani. Lakini ni miongoni mwa vyakula vyanye virutubisho muhimu sana kiafya tofauti na watu wengi wanavyodani.

Kwa mujibu wa mtandao wa www.organicfacts.net uyoga una vitamini na aina nyingi za madini.Baadhi ya virutubisho vilivyothibitishwa kuwemo kwenye uyoga ni pamoja na Vitamini B2, B3, B5, B6, B Complex pamoja na madini ya Potasiamu na ‘Phosphorus'.

Wataalamu hao wanaeleza kuwa virutubishoi vilivyomo ndani ya uyoga kuwa vina uwezo mkubwa sio tu wa kuimarisha kinga mwilini bali pia kupambana na maradhi.

Mtandao huo pia umeendelea kueleza kuwa uyoga ni chanzo kingine kizuri cha madini ya chuma na shaba yanayohusika katika uwezeshaji wa usambaza wa hewa ya oksijeni mwilini.

Vitamini B2 inayopatikana kwenye uyoga, ni tiba kwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kichwa unaojulikana kama ‘kipanda uso'.

Kwa kula kiasi kidogo cha mmea huo utajiweka kwenye nafasi ya kuwa na hali nzuri hususani kwa wale wagonjwa wa kipanda uso

Vitamini B kwenye uyoga, ina uwezo wa kuzuia uchovu wa mwili na akili hasa wakati wa kazi nyingi. Vitamin B3 husaidia kupunguza kiwango cha lehemu mwilini, wakati Vitamini B6 huondoa hatari ya mtu kupatwa na kiharusi au shambulio la moyo.

Pia, una madini ya zinki yanayoimarisha kinga ya mwili pia husaidia kuponya haraka vidonda si hivyo tu faida nyingine husaidia ukuaji mzuri wa seli za mwili, huimarisha kiwango cha sukari
mwilini na kukufanya usikie ladha , harufu ya vyakula na vitu vingine ipasavyo.

Kwa ujumla uyoga ni mboga muhimu na inapaswa kuliwa na kila mtu anayejali afya yake kutokana na faida zinazopatikana humo. Kuanzia leo, jaribu kuweka uyoga katika orodha ya mboga unazonunua kila wiki kwa ajili ya familia yako.

Bila shaka kwa wakazi wa miji midogo na vijijini, mboga hii hupatikana kwa wingi wakati wa mvua na kwa miji mikubwa kama Dar es Salaam, uyoga unaweza kupatikana kwenye masoko maalum kama, Kariakoo, Kisutu na ‘super market' mbalimbali.
 
Niliwahi kulima uyoga,kwa kweli ni chakula kizuri.Uko very sensitive,niliona wakati huo nikilima,ukiingia shambani(kwenye banda kwani ndiko unakolimwa kisasa) bahati mbaya ukajisahau na ukaingia na nguo ulojipulizia perfume,imekula kwako kwani shamba zima kila uyoga utakaochuma ukiunusa unanukia perfume.Labda ndo maana hata ule unaoota wenyewe kuna wakati mwingine watu wamejikuta wakila uyoga wa sumu japo aina walochuma ni ile ile wanayochuma mara zote inayofaa kwa chakula.Kwamba kutokana na hali ya kuwa very sensitive,mdudu mwenye sumu aliugusa na hivo sumu kusambaa ktk uyoga kirahisi. Vinginevyo ni MSOSI POA SANA.
 
Back
Top Bottom